Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo tarehe 04 Oktoba, 2024.
WhatsApp Image 2024-10-04 at 15.19.46_d14b76c3.jpg


RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.

RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Akizungumza wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mchakato wa ulipaji kodi unatakiwa kuwa rafiki ili kumwezesha mlipa kodi kukamilisha zoezi hilo ikiwemo mifumo inayotumika.

Amesema kuna umuhimu wa kutoa elimu zaidi kwa walipa kodi ili wajue wanamlipa nani na kiwango gani, akitoa mfano amesema alikutana na changamoto Mkoani Ruvuma ambapo alisema kuna Mama Lishe waliokuwa wakilalamika kuhusu kulipishwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


=========================

RAIS SAMIA: HATUA MPYA KATIKA MABORESHO YA MFUMO WA KIKODI TANZANIA

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza tangu Rais Benjamin Mkapa kuboresha mfumo wa kikodi nchini Tanzania, baada ya kuunda Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi. Tume hii ina lengo la kuangazia changamoto mbalimbali zinazokabili mfumo wa kodi na kutoa mapendekezo yanayoweza kuboresha ukusanyaji wa kodi na ufanisi wa matumizi yake.

Moja ya mambo makuu ambayo Rais Samia anatarajia kuyatekeleza kupitia tume hii ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa kodi. Hii ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa serikali na mfumo wa kodi, ambao mara nyingi umekuwa ukikabiliwa na malalamiko kuhusu ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma.
WhatsApp Image 2024-10-04 at 15.19.44_18df1727.jpg

WhatsApp Image 2024-10-04 at 15.19.45_e759522e.jpg
Pia, tume hiyo inatarajiwa kuzingatia njia mpya za kukusanya kodi ambazo zitasaidia kuongeza mapato ya serikali bila kuweka mzigo mzito kwa wananchi. Hii inaweza kujumuisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji wa kodi, kama vile mifumo ya kielektroniki inayorahisisha malipo ya kodi na kuondoa urasimu usio wa lazima.

Aidha, Rais Samia amesisitiza katika ushirikiano na sekta binafsi ili kuboresha mfumo wa kikodi. Ushirikiano huu unaweza kuleta mawazo mapya na mbinu za kisasa katika ukusanyaji wa kodi na pia kutoa fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Kwa kufanya hivi, Rais Samia atasaidia kukuza mazingira ya biashara yanayovutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi. Hii ni muhimu katika kipindi ambacho uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto, na Tanzania inahitaji kuongeza mapato yake ya ndani ili kufikia malengo yake ya maendeleo.
WhatsApp Image 2024-10-04 at 15.19.48_f82a85a6.jpg

WhatsApp Image 2024-10-04 at 15.19.47_014035a8.jpg

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo tarehe 04 Oktoba, 2024.


RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.

Mnatuchosha
na habari za mtu aliyechokwa
 
RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.

Si aliwambia Jamaa wale kwa urefu wa Kamba zao.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo tarehe 04 Oktoba, 2024.


RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.

Kodi ya kwanza kurekebishwa waanze na ile ya magari ya mtumba toka Japan. Haiwezekani gari inunuliwe $3500 halafu kodi iwe $4000!
 
Ujinga mtupu

Unawezaje kuwa na tume ya marekebisho ya kodi?

Msingi wa kodi ni maamuzi ya dira ya uchumi na mipango ya budget ya serikali.

Hakuna mtu anaeweza amua maswala ya kodi zaidi ya waziri fedha.

Na maamuzi yake (yaani, viwango vya kodiz) ni sera za nchi inataka ku-achieve nini.
 
Upumbavu wa nchi is beyond me,

Hivi huko duniani mnaonekana ni wajinga wa kiasi gani.

Mnaelewa hata uhusiano wa kodi na budget na mipango ya budget au hata budget ya nchi inavyotengenezwa.

Ni matahahira tu yanaweza tengeneza simema kama hii.

Na haya nasema kama ‘financial’ hii ni kujidharaulisha kwa dunia. Yaani hata mzungu akiwatukuza ni kwa kuwan’gon’ga.

Hakuna mtu anaepanga budget duniani zaidi ya waziri na budget Ina kanuni zake.

Tume ya marekebisho ya kodi ujinga uliopita kiasi.
 
Ni jambo jema

Jumaa Mubarak 😀🌹
Wapendwa,

Kwanza, nawashukuru nyote mlionifariji. Pili, nawaomba radhi niliowakosea kwa sababu at times, I became emotional, and sometimes even more so kutokana na mauaji ya Korogwe.

Hata hivyo, sina maneno sahihi ya kuelezea uzito wa maumivu yangu, na kwa kweli, sikukusudia kuandika bali nimejikuta nimeshika tu simu nikaanza kuandika. Nimeandika mengine mengi, na nikayafuta kwa wingi huo huo, lakini nimeona hili la sasa nisilifute. Siku kama ya leo, Jumatatu iliyopita, Septemba 23, saa 3:30 usiku, ndipo watu wasiojulikana walimteka dada yangu na familia yake nyumbani kwake, wakaenda kuwaua. Ni siku ambayo sitapenda kuikumbuka kamwe, lakini najua sitaweza kuisahau hadi hapo ubongo wangu utakapokuwa haufanyi kazi tena.

Nimewahi kusikia habari nyingi za watu kutekwa na kuuawa, lakini siku zote nilidhani ni mambo ya mbali, yasiyoweza kunigusa familia yangu moja kwa moja. Niliishi na imani hiyo ya uongo, nikidhani kuwa mimi na watu wangu wa hatuwezi kamwe kuhusika wala kuhusishwa katika matukio haya ya kikatili. Lakini sasa, nimeujua ukweli huu, ambao umeniumiza kuliko nilivyowahi kufikiria. Ni wazi sasa kuwa maovu haya yako karibu zaidi nasi kuliko tunavyodhani na kutaka kuamini.

Dada yangu Jonais, ulikuwa dada rafiki yangu wa karibu, na ulinitazama kwa macho yenye upendo usiojificha, usio na unafiki. Sisikitiki sana kwamba ulikufa, lakini Zaidi ulikufa kifo cha kikatili, mikononi mwa watu waovu walioamua kuua ndoto zako na za mwanao Dedan, mtoto asiye na hatia wala makosa.

Mpwa wangu, Dedan, ulikuwa na miaka minane tu, mtoto mdogo usiyejua lolote kuhusu uovu wa ulimwengu huu. Walikuangamiza bila huruma. Niliona machozi ya kaka zako, Bright na Derick, yakituacha wengi katika huzuni kuu. Niliona wanafunzi wenzako wa Shule ya Msingi Good Foundation, Korogwe, wakikulilia kwa uchungu usio na kifani. Walimu wako walilia kwa uchungu mkubwa, machozi yao yakiwa kama ujumbe wa masikitiko kwa kila aliyeshuhudia. Nakuhakikishia, kwa Imani yangu, machozi haya hayajapotea bure. Kama inavyosema Zaburi 56:8, Mungu huhifadhi machozi ya waja wake kwenye chupa Yake.

Ni vigumu sana kuelezea maumivu niliyopata nilipoona kuona miili yenu ikiteremshwa kwenye makaburi yenu. Sauti ya udongo ulipokuwa ukiwagubika ndipo nikawa na hakika huo ni mwisho wa kila kitu, mwisho wa matumaini, mwisho wa ndoto zenu. Wao waliwaua, sisi tumewazika, lakini tutaendelea kuishi na upendo wenu. Iliniumiza sana kiasi kwamba siwezi kuelezea kwa maneno, lakini moyo wangu ulivunjika. Nawe mpwa wangu Dedan, sauti yako ya furaha bado inazunguka kichwani mwangu, sauti niliyoisikia kwa mara ya mwisho mwaka jana nilipokuja kusabahi nyumbani, ukanikimbilia ukipiga kelele za "Mjomba Willy! Mjomba Willy! Mjomba Willy!" Hakika, ni sauti nitakayoikumbuka maisha yangu yote hadi hapo ama kumbukumbu zitakaponitoka au nitakapoondoka katika maisha ya dunia hii.

Kuna wakati nilichukulia kwa wepesi fulani habari za kutekwa na kuuawa kwa watu. Sasa maumivu haya yananiambia hazipaswi kuchukuliwa kwa wepesi, maana leo ni kwetu, kesho inaweza kuwa kwa mtu mwingine. Watu wengi wanapuuza, wakidhani hawahusiki, lakini dhambi ya kutokujali inaweza kumrudia yeyote.

Mithali 17:15 inatufundisha kuwa wale wanaoona waovu kuwa wana haki, na wale wanaowahukumu wasio na hatia, wote wawili ni chukizo kwa Mungu. ”Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa Bwana.” Na haya yanayotokea sasa ni wazi kuwa ni maovu yanayofumbiwa macho na baadhi ya watu katika jamii yetu. Tunakumbushwa pia katika Isaya 5:20 kuwa "Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!" Na kila nikiitafakari aya hiyo, naona maovu yaliyomwangamiza dada yangu na mpwa wangu.

Katika kitabu cha Waefeso 5:11, tunaambiwa tusishirikiane na matendo ya giza, bali tuyakemee. "Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee..." Na ni lazima tuyakemee matendo haya kwa nguvu zetu zote, kwa sababu kifo cha Jonais na Dedan si cha kwanza, na labda hakitakuwa cha mwisho kama tusipokemea haya sasa.

Kwa wale wanaodhani matendo haya hayawahusu, wakumbuke historia inatufundisha kuwa ukimya mbele ya dhuluma huleta maangamizi kwa wengi, kama alivyosema Mwanatheolojia wa Ujerumani enzi za Adolf Hitler, Mchungaji Friedrich Gustav Emil Martin Niemoller, alipowakumbusha watu jinsi walivyokuwa wakipuuzia matendo ya unyanyasaji mpaka yalipowafikia wao wenyewe—na yeye mwenyewe.

Shairi lake lasomeka hivi: "First they came for the socialists, and I did not speak out — because I was not a socialist. Then they came for the trade unionists, and I did not speak out — because I was not a trade unionist. Then they came for the Jews, and I did not speak out – because I was not a Jew. Then they came for me — and there was no one left to speak for me."

Maumivu haya ninayoyahisi leo, yanaweza yakamgusa mwingine leo, au kesho, au keshokutwa. Na kwa wale wanaoamini kuwa hawawezi kukutwa au kuathiriwa nayo, nawapa changamoto waangalie historia na kuyasoma maandiko. Wakati huponya, lakini kumbukumbu ya uchungu na maumivu haya haitaondoka milele.

Dada yangu Jonais, mpwa wangu Dedan, na binti wa kazi aliyeuawa pamoja nanyi, mlidhulumiwa maisha yenu na watu wasiojulikana, lakini ninatumaini kuwa Mungu amewapokea kwa amani. Haya ni maombi yangu, hata wakati maumivu yanapokuwa hayavumiliki.

Rest in peace.

William Shao
Septemba 30, 2024
 
NDUGU ............MENEJA WA TRA MKOA WA KODI KINONDONI ANAKUHIMIZA KULIPA KIASI CHA SH. 912,400.00 AMBAYO NI MALIPO YA KODI YA PAYE YA MWEZI AGOSTI 2024. LIPA KODI HII KABLA YA TAREHE YA LEO 30/09/2024 KUISHA. RIBA NA ADHABU ZITAJUMUISHWA KWA KUSHINDWA KULIPA KWA WAKATI.
"PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU"
 
NDUGU ............ MENEJA WA TRA MKOA WA KODI KINONDONI ANAKUHIMIZA KULIPA KIASI CHA SH. 93,418,445.29 AMBAYO NI MALIPO YA VAT YA MWEZI AGOSTI 2024. LIPA KODI HII KABLA YA TAREHE YA LEO 30/09/2024. RIBA NA ADHABU ZITAJUMUISHWA KWA KUSHINDWA KULIPA KWA WAKATI.
"PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU"

Waaaambie silipi hata kwa fimbo, waniue! Hii ni Kodi au ni laana?
 
Rais Samia Suluhu akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi, amesema kuwa kodi tunayokusanya hailingani na idadi ya watu.

“Uchumi wetu unakua sana, lakini haulingani na tunachokikusanya. Tunakusanya kidogo sana, kingi kinaingia mifukoni kwa watu bure bure tu. Shughuli za kiuchumi zinazoendelea nchini na idadi ya watu hailingani na mapato tunayoyapata.”

My Take: Naunga mkono hoja, na huu ndio ukweli. Ukiangalia utajiri wa Watu na miradi wanayofanya na kile tunapata ni vitu 2 tofauti.

Serikali inawaonea Watumishi tuu ambao hawawezi kukwepa Mapato lakini huko Mitaani wafanyabiashara wanalipa robo ya wanachostahili au wanakwepa kabisa.👇👇


Pamoja na Kulalamikia kwamba watu ni wengi ila hawalipi Kodi ni lazima ujue kati ya hao watu mil.65 ,,ukiondoa under 18 na maskini,wanafunzi,wazee Je Nguvu kazi halisi ni kiasi gani?


Soma hapa: LIVE - Rais Samia akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Ikulu - Dar, Oktoba 4, 2024
 
Back
Top Bottom