Maswa Yetu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2023
- 1,398
- 2,619
Rais Samia ujue kabisa ya Ndugai hayapo kanda ya ziwa, askofu Gwajima na Mpina hawatakuomba msamaha hata ni kwa gharama ya kuwafukuza ccm watakuwa tayari.
Malezi ya watoto kanda ya ziwa na malezi ya watoto kanda ya Pwani ni vitu viwili tofauti.
Kanda ya ziwa baba ndiyo kiongozi wa familia na akishatoa maagizo lazima yatekelezwe na yasipofuatwa mtarajie adhabu kali sana, wakati huko kanda ya Pwani mama ndiyo kiongozi wa familia na watoto wanafuata maagizo ya mama huku baba akibaki kama pambo tu ndani ya nyumba. Kwa hiyo mtu wa kanda ya ziwa( ondoa mkoa wa Kagera) akishamini jambo lake hageuki nyuma tena hata umtishe na kitu gani. Namtaarifu tu Rais Samia kuwa hatakaa aombwe msamaha na hao watu wawili maana wanaamini kupinga utekaji na ufisadi ndiyo jambo linalotakiwa kufanywa na serikali au mtu yoyote mwenye akili timamu. Sasa inapotokea wanaopinga utekaji na ufisadi ndiyo wanaandamwa na serikali hilo ni jambo la ajabu na mtu wa kanda ya ziwa hatakubaliana nalo.
Yani ukosee wewe alafu uombwe msamaha wewe? Hilo halipo.