tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Chini ya utawala uliopita tumeshuhudia matukio mengi ya ovyo yenye kulifedhehesha taifa kwa kiasi kikubwa.
Ni katika utawala huo kulikuwa na matukio ya watu wengi kupotea katika mazingira ya utata, na hawajawahi kuonekana hadi leo. Na kibaya zaidi, hata miili yao haijawahi kupatikana ili ndugu zao wawazike kwa heshima. Tukio la kutisha zaidi lilikuwa jaribio la kumuua Tundu Lissu mchana kweupe akiwa maeneo ya bunge.
Wakati akihojiwa kupitia runinga ya ITV, IGP mstaafu, Simon Sirro alijiteta kwamba watu hawa wanaodhaniwa kupotea wameenda kutafuta riziki mahali kusikojulikana, wakishamaliza shughuli zao watarudi nyumbani bila kuchelewa. Kutafuta riziki kwa zaidi ya miaka 10 na wasiwasiliane na ndugu zao? Labda hiyo riziki wameenda kuitafuta mbinguni!
Katika mahojiano hayo Sirro alisema ili kuthibtisha mtu amekufa mpaka mwili wake upatikane na kufanyiwa vipimo kufahamu chanzo cha kifo. Kama Lissu angefariki, kama ilivyokuwa imekusudiwa, huenda naye mwili wake ungepotezwa ili kupoteza ushahidi. Hii ndiyo njia nzuri inayotumiwa na wauaji kupoteza ushahidi.
Nina hakika baadhi ya wauaji waliojaribu kumuua Lissu pamoja na aliyewatuma huenda wamekufa. Hivi wale wauaji waliosalia hapa duniani wakimuona Lissu anachechemea, hata kama walisukumwa kumuua, wanajisikiaje lakini?
Si mauaji tu yaliyotawala kipindi cha kwanza, bali pia tumeshuhudia utawala wa kiupendeleo. Mtawala aliyepita alisikika akimataja Mungu mara kwa mara na kusema maendeleo hayana chama. Lakini alidiriki kufanya upendeleo wa ovyo kwa kutumia fedha za umma kuimarisha mkoa aliotokea, hasa jimbo lake la zamani, ambamo alijenga kiwanja cha ndege, kuanzisha mbuga ya wanyama, kujenga VETA na kununua kivuko kwa kutumia fedha za umma. Wakati akifanya hivyo, maeneo mengine ya nchi yalikuwa taabani, kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha, huku kila siku akijinasibu nchi ipo uchumi wa kati. Tukisema Rais Samia naye apeleke maendeleao kwao Makunduchi, kama mtangulizi wake, hii nchi itakuwaje?
Kana kwamba hayo yote hayatoshi, tukio la mwisho la ovyo kufanyika katika nchi hii lilitokea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020. Sitaki kueleza hili kwa kuwa kila mtanzania mwenye akili zilizotimia alishudia kilichofanyika.
USHAURI KWA RAIS
Inapotokea njaa kwenye familia kwa sababu ya ukame, anayelaumiwa ni baba hata kama hajasababisha huo ukame. Vivo hivyo, nchi inapoingia kwenye maovu anayelaumiwa ni Rais, hata kama hahusiki moja kwa moja. Kadhalika, dhambi zikizidi kwenye nchi, wa kwanza kulaumiwa ni Rais.
Nashukuru Rais Samia ni kiongozi mahiri na msikivu. Baada ya kuingia madarakani ameweza kuondosha maovu mengi yaliyofanyika kipindi kile. Tuna imani hatarudi nyuma. Amewalipa mafao wafanyakazi wa drs la saba na wenye vyeti feki waliofukuwa kazi kiuonevu. Pia ameanza mchakato wa kutafuta katiba mpya na kurekebisha uovu mwingi uliofanyika kipindi kile.
Namsihi sana Rais Samia ahakikishe dhambi za aina ile zinabaki kuwa historia katika nchi hii. Mshahara wa dhambi ni mauti. Na mauti yatonayo na dhambi adhabu yake ni jehanamu. Kwa hiyo, ikiwa Rais Samia ataendelea kuongoza nchi kwa unyenyekevu na kuepuka dhambi zote zilizotokea kipindi cha nyuma ataingia peponi moja kwa moja.
Nawasilisha.