Nyie ndio mnashangilia Kuuza mahindi alafu muuziwe unga
Nitakueleza maana huwenda hukielewi unacho zungumza, tuchukulie mfano uliotoa wa tz kuuza mahindi kisha ketewa unga. Kwakua tuna mahindi lakini hatuna viwanda serikali sasa imeona tuite wenye viwanda(au walau wenye uwezo wakuwa navyo) lakini hawana mahindi ,ambayo ni malighafi ya viwanda hivyo. Tutakapopata viwanda hivi maana yake
1. Hatutasafirisha mahindi nje badala yake tutakuwa na unga uliozalishwa hapa hapa nchini, kitu ambacho wewe ndio unakitaka sio ?
2. Wakileta viwanda hivi watakuwa wameleta mtaji wao kwetu sio ? Maana yake pale kwenye kiwanda hicho patapata chanzo kipya cha pesa kwa shughuli ha ujenzi tu wa kiwanda husika.
3. Watu wetu watapata ajira, zote rasmi na zisizo rasmi, za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja hivyo serikali kwa namna fulani itakuwa imepunguzs chamgamoto ya ajira. Ajira hizi zipo za namna nyingi tumezowea za moja kwa moja lakini zipo nyingine ambazo si za moja kwa moja, hizi zitatoka katika sekta zote ambazo kwa namna yeyote zinagusika na uwepo wa kiwanda hichi, kama mabenki, sheli, huduma za kijamii nk.
4. Serikali itapata kodi, kila mwisho wa mwaka wa hesabu serikali itapata 30% ya faida ya kiwanda hicho (bila kuweka mtaji!) Hii hiwa ni kodi, lakini pia serikali itapata kodi nyingine kama kodi ya ongezeko la thamani, kodi ya mapato ya wafanyakazi na masurufu mengine mengi.
5. Wazawa watapata uelewa na uzoefu wa uendeshaji na utawala wa viwanda vya aina hiyo, hivyo kurahisisha ongezeko la viwanda vya namna hiyo.
6. Kuongezeka kwa uzalishaji nchini, kukua kwa pato la taifa na kukuza sekta nyingine kama usafirishaji. Faida nyingine lukuki nimeacha kuzitaja,.
Umepata mwanga wa kuelewa japo kidogo kwanini tunataka waje tuu kiwekeza na kufiata taratibu zetu na sheria ??