Rais Samia umekubali kutukuzwa hivi? Yanayofanyika shuleni siku yako ya kuzaliwa siyo sawa

Hapo hajatukuzwa, bali wameonyesha mshikamano nae tu. Ni wachawi na wanga tu wasiokuwa na shukrani humu mitandaoni na wasioona anachokifanya katika elimu. Ukweli ni kuwa huku elimuni tunamheshimu sana
 
Utukufu wa mama na aabudiwe.
 
Hapo hajatukuzwa, bali wameonyesha mshikamano nae tu. Ni wachawi na wanga tu wasiokuwa na shukrani humu mitandaoni na wasioona anachokifanya katika elimu. Ukweli ni kuwa huku elimuni tunamheshimu sana
Ni sawa hao wanafunzi wa benjamini mkapa leo kuwa nje kusheherekea birthday?
 
Mi nafurahi kishenzi ninapoona dua za chuki za walioshindwa sababu baraka zake zimo ndani chuki za maadui......kadiri wanavyomchukia na kumuombea dua mbaya, ndivyo atakavyopona na kufanikisha malengo kwa uwezo wa Muumba!

Sawa Dear Leader!
 
Mambo ya Kim Jong Un hayo…
 
Ni sawa hao wanafunzi wa benjamini mkapa leo kuwa nje kusheherekea birthday?
Kama limeamuliwa na walimu na wameshapanga namna ya kufidia vipindi vya leo, halina shida yoyote. Raisi ni mtu mkubwa mno na anasakamwa na mengi kutoka kwa wachawi na wanga hivyo kutumia masaa machache kumpa moyo ili aendelee kuuvaa ujasiri wa kusonga tu mbele katikati ya matusi, kashfa, uzushi, chuki na maneno meengi yenye lengo la kuudhi na kuleta hasira ni jambo sahih8 kabisa. Au we unaonaje mdau?
 
Mkuu haya mbona hayakufanyika kwa maraisi wengine waliopita?
Au pia mbona sijaona nchi yoyote ikifanya haya hata Sasa?
 
Wakuu wana jf nikitambo tu naomba picha za birthday za marais wengine lakini kama hamuon comment au nianzishe uzi au na mm najipendekeza[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo hajatukuzwa, bali wameonyesha mshikamano nae tu. Ni wachawi na wanga tu wasiokuwa na shukrani humu mitandaoni na wasioona anachokifanya katika elimu. Ukweli ni kuwa huku elimuni tunamheshimu sana

Wewe na walimu wenzio waliobariki huo utoto mna akili za kitoto sana
 
Hapo hajatukuzwa, bali wameonyesha mshikamano nae tu. Ni wachawi na wanga tu wasiokuwa na shukrani humu mitandaoni na wasioona anachokifanya katika elimu. Ukweli ni kuwa huku elimuni tunamheshimu sana
Kama kweli uko elimu basi unafaa kuishia ngazi ya mfagiaji tu, tena ufagie nje ya ofisi. Unashangilia watoto wa wenzio kuacha masomo kwenda kusherehekea birth day? Mwalimu gani wa ovyo kiwango chako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…