Rais Samia umetusahau wana Shinyanga hatuna Mkuu wa Mkoa mpaka sasa

Rais Samia umetusahau wana Shinyanga hatuna Mkuu wa Mkoa mpaka sasa

Tangu Sophia Mjema ateuliwe kuwa Mwenezi wa CCM, mkoa hauna mkuu wa mkoa, badala yake RC Simiyu anakaimu. Hii ya Kukaimu muda mrefu inachelewesha mambo, mipango ya maendeleo na utekelezaj wake.

Teua mama, majembe yako mengi tu mtaani hayana kazi.
Atamleta, ila muache uchawi, mjadili maendeleo, Ina kahama inawapita mbali, na ikitoka kahama, huo Mkoa mi dampo la umasikini. Sinza baada ya nyumba mbili baa, shinyanga Kila nyumba hukosi mwanga
 
Tangu Sophia Mjema ateuliwe kuwa Mwenezi wa CCM, mkoa hauna mkuu wa mkoa, badala yake RC Simiyu anakaimu. Hii ya Kukaimu muda mrefu inachelewesha mambo, mipango ya maendeleo na utekelezaj wake.

Teua mama, majembe yako mengi tu mtaani hayana kazi.
Hayo ya mtaani yasiyo na kazi yaache yakae tu maana yakishaonjeshwa asali yanalewa yanaanza kuwambia vijana wajiajiri wakati yenyewe yamejiriwa
 
Unataka kusemaje vyeo vya rc vifutwe ama? inabidi katba ibadilike maana wanateuliwa kwa mujibu wa katba tuliyo nayo iv sasa.na kama mikoa mingine wapo bas na shy aletwe.

Vifutwe ni vya hisani ,havina maana yeyote ,hao ma rc/dc/ras/das na vinavyofanana na hivyo vipelekwe ndani ya ccm na si serikalini....yaani wawe mkuu wa ccm wilayani,mkoa etc kama tayari kuna mwenyeketi wa ccm wilaya/mkoa basi wagawanywe madaraka.
 
Ccm wana zaidi ya miaka 46 ni lini mipango ya maendeleo na utekelezaji umefanikiwa kwa ufanisi. Ata aje nani shughuli ni ngumu
Usiwadogoshe namna hiyo Ccm wataonekana wachanga ukisema miaka 46 bhana.

Wana zaidi ya miaka 60 wapo madarakani.

Kilichobadilishwaga ni majina na rangi ya bendera, lakini viongozi na sera ni zile zile!

Ni kama ilivyokuwa kwa Jeshi la Tanganyika Rifles kuitwa Jwtz.

Ama nyoka baada ya kujivua gamba, hubakia nyoka huyo huyo.

Hawa wako madarakani miaka yote ya uhuru lakini ni failuers kabisa!
 
Back
Top Bottom