Rais Samia unajua kuwa wanaohujumu Kilimo ni hizi Benki za Biashara?

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana Jf

Nimefanya sana harakati za kilimo chenye tija ili kuinua pato la taifa pamoja nami mwenyewe kupata fedha za kujikimu.

Nilichokutana nacho ni kile buraha buraha za vijana wa benk wasio na ujuzi wowowte kuhusu kilimo.

Katika kilimo kuna mazao ya muda mrefu kama michikichi, embe, kahawa, chai, avocado, minazi, vanila na mapera.

Mimi kama mkulima wa kawaida, nimewahi kuhudhiria makongamano mengi ya kilimo, na yale makongamano ya elimu ya ujasilia mali.

Tuliwahi kudhaminiwa masomo na EU, ITC, ILO kusoma elemu ya ujasilia mali lakini ukija kwenye utendaji unakutana na banker ambaye ni mkopeshaji akiwa hajui gharama halisi za mazao hata uandaaji wa shamba.

Mtu huyu anashindwa kutoa mkopo hata aelezwe vipi matokeo mema yatakayopatikana kwenye kilimo husika.

Jambo baya sana ambalo mkulima wa chini awezi kufanikiwa kukopa ni kwamba dhamana anayotakiwa kuweka inakindhana sana na matakwa yao.

Wao wanataka nyumba tu wakati hata shamba la kudumu ni mojawapo ya dhamana.

Kwa kadhia hii Mama Samia nchi haitajikomboa katika kilimo ikiwa benki wamekalilishwa kuweka nyumba kama dhamana.
 
Kazi kweli kweli..sera zimebaki kwenye makaratasi ofsini mwao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwani benki za serikali?
Hata kama benki ziwe za serikali vijana wanaotumwa hawajui kitu, pia urasimu mwingi kwenye ukopeshaji. Wenye viwanda ndio wanaofaidi lakini wenye kilimo kinachochukua miaka mitatu wako kwenye mkwamo mkubwa. Ukienda bukoba hamna benk ya kilimo zaidi ya blabla za nyumba na nyumba wanataka za mjini zenye hati.
 
Wakulima waunde umoja wajitetee.
 
Wakulima waunde umoja wajitetee.
Serikali inajinasibu kuwa kilimo ni uti wa mgongo alaf mkulima akilima kwa nguvu zake bila mkopo mazao yanapangiwa bei. Umoja ni mgumu kwa kuwa wananchi wengi hawakusoma waliosoma wanakuwa wanyonyaji. Ukiitisha washa wa wakulima anakuja wale ambao wana maestate, ikitokea hela awa ndio wanazifinya wa kwanza kwa kuwa wana cha kuweka pengine hawaweki kitu wanaaminiwa tu.
 
Anaelewa Sasa? Kilimo bongo fanya tu kwa mipango yako, ukitegemea serikali unafeli
 
Sasa waache kututamanisha na mikopo ambayo haitolewi wakati wanaiandikia kuwa inaenda kwa walengwa ambao ni wakulima wa size zote.
 
Kuna mtu aliniambia kuwa BENKERS wote hapa TANZANIA wamefundishwa kuwa mteja akiingia Benki muangalie rangi yake kama ni mweupe,(mzungu,mwatabu,mhindi ,mburushi) mpe huduma anayotaka fasta usimwache atoke mikono mitupu,lakini kama mwafrika , jitahidi ufanye uchunguzi ukiridhika sawa lakini unaweza kuachana nae TU Angalia Kuna Rostam safari ya royal your america mwenzetu kishaenda kwenye kilimo Cha ngano.
 
Yaani kakwambia ukweli mimi imenitokea. Nimeenda NBC Muleba nikapeleka document zangu kuonyesha mradi fulani ambao nimejifunza Madagascar pamoja na hatua ambazo nimeshafikia kwa gharama zangu mwenyewe. Nilijibiwa mtaalum anayejua kilimo yupo mwanza hivyo huwa anakuja kutembelea wateja mara moja au mbili kwa mwezi. Nikaomba anipe numba nimfuate mwanza, basi akanipa numba , nilipofika mwanza nikakutana naye, mambo aliyoniambia utakaa chini ulie. Kitu cha kwanza bila kujari ukubwa wa shamba, thamani ya mazao , lazima niwe na mali isiyoamishika iliyothibitishwa na ardhi ambayo ni nyumba. Kama nyumba haijaisha unapewa mkopo lakini si kitu kingine. Basi nikaona tangazo kuwa wamepewa hela tena na B.OT kwa ajiri ya wakulima wadogo. Nikawafuata tena akaniambia nikwambie ukweli. Benk zinawaogopa sana wakulima kitokana na kilimo Chao kuwa cha mashaka hivyo bila nyumba no mkopo.
 
Mi nazan makosa ni yako mwenyewe umekosea bank na kwa uelewa wangu mm najua Tz bank nyingu ni bank za biashara na sio bank za kilimo na km sijakosea tz bank za kilimo ni chache au hamna kabsa au hazina mitaji
Sasa ukipeleka na proposal yako ya kilimo bank ya biashara unategemea utakutana na nn zaidi ya kukasirika na kumeza Sumu tu

Na hii ishu serikal inajua kbsa ila unakuta inamwambia mkulima akakope sa sjui anaenda kukopa bank gan? Na kwa masharti yapi

Ni sasa sawa na suala la ujenzi tanzania akuna bank za ujenzi ila kuna bank za biashara ukienda bank ukakopa mkopo wa ujenzi ndio watakupa ila km unaakili masharti yao hayaendani na ujenzi ila yanaenda kibiashara ata mda wao wa ulipaji haujakaa km mkopo wa ujenzi ila umekaa km mkopo wa biashara
 
NMB, CRDB na Benk ya Kilimo mwaka juzi zilianzisha vitengo vya kuhudumia mikopo ya wakulima wadogo na wakati ambao mkulima mdogo anakopa kuanzia million tano mpaka miamoja. Kuna matangazo kibao benk nilizokutajia zimepewa hela na B.o.T chini yapango wa serikali kuinua wakulima wadogo. Mimi mwenyewe nimeudhuria warsha na semina mbali mbali amba?o tulikuwa tunaandamana na benkers, wataalum wa kilimo na watu wa mawasiliano hasa vodacom ambao nao wanahamasisha kilimo cha mtandao. Lakini mkwamo kamili ni kwamba wanataka kijana aliyejiajiri kwenye kilimo awe na nyumba yenye thamani. Huo ni uchuro kwa serikali kuamini hizi benki za biashara zitainua wakulima wakatiwasimamizi wa mikopo ya kilimo hawana uelewa kabisa na masuala ya kilimo. Kuna mikoa ambayo kilimo sio risk sana kufuatana na mazao yanayolimwa humo lakini serikali imewaweka kando.
 
Inasikitisha sana wale benki ya kilimo kupeleka fedha za benki ya kilimo ,kwenye benki hizo zisizo kuwa na mentality ya kilimo,nilisikia Hilo nikasikitika sana,Hawa NBC,CRDB hawana akili ya kuinua kilimo Cha Tanzania kupitia mikopo ya benki,nakupa mfano hatari sana hapa iringa,benki zote ukitaka mkopo unaambiwa nyumba himilivu kwa mikopo yao lazima iwe maeneo ya kuanzia kichangani (fieldforce) mpaka mitaa ya Samora wakati nyumba za mitaa hiyo asilimia 80 ni nhc na majengo ya taasisi za umma,wakija jamaa zako wa benki mtaani kwako wanazuga tu mitaa kama frelimo,ilala,isoka nk ukiwa na nyumba wanasema sio himilivu kwa mkopo,niambie mkulima anayeweza kuwa na nyumba maeneo hayo Iringa.
 
Wana Jf

Nimefanya sana harakati za kilimo chenye tija ili kuinua pato la taifa pamoja nami mwenyewe kupata fedha za kujikimu.

Nilichokutana nacho ni kile buraha buraha za vijana wa benk wasio na ujuzi wowowte kuhusu kilimo.

Katika kilimo kuna mazao ya muda mrefu kama michikichi, embe, kahawa, chai, avocado, minazi, vanila na mapera.

Mimi kama mkulima wa kawaida, nimewahi kuhudhiria makongamano mengi ya kilimo, na yale makongamano ya elimu ya ujasilia mali.

Tuliwahi kudhaminiwa masomo na EU, ITC, ILO kusoma elemu ya ujasilia mali lakini ukija kwenye utendaji unakutana na banker ambaye ni mkopeshaji akiwa hajui gharama halisi za mazao hata uandaaji wa shamba.

Mtu huyu anashindwa kutoa mkopo hata aelezwe vipi matokeo mema yatakayopatikana kwenye kilimo husika.

Jambo baya sana ambalo mkulima wa chini awezi kufanikiwa kukopa ni kwamba dhamana anayotakiwa kuweka inakindhana sana na matakwa yao.

Wao wanataka nyumba tu wakati hata shamba la kudumu ni mojawapo ya dhamana.

Kwa kadhia hii Mama Samia nchi haitajikomboa katika kilimo ikiwa benki wamekalilishwa kuweka nyumba kama dhamana.
Upo sahihi kabisa
 
Uzi mzuri kabisa huu !

Serikali kllimo inaichukulia juu juu tu

Ova
 
Inasikitisha sana wale benki ya kilimo kupeleka fedha za benki ya kilimo ,kwenye benki hizo zisizo kuwa na mentality ya kilimo,nilisikia Hilo nikasikitika sana,Hawa NBC,CRDB hawana akili ya kuinua kilimo Cha Tanzania kupitia mikopo ya benki,nakupa mfano hatari sana hapa iringa,benki zote ukitaka mkopo unaambiwa nyumba himilivu kwa mikopo yao lazima iwe maeneo ya kuanzia kichangani (fieldforce) mpaka mitaa ya Samora wakati nyumba za mitaa hiyo asilimia 80 ni nhc na majengo ya taasisi za umma,wakija jamaa zako wa benki mtaani kwako wanazuga tu mitaa kama frelimo,ilala,isoka nk ukiwa na nyumba wanasema sio himilivu kwa mkopo,niambie mkulima anayeweza kuwa na nyumba maeneo hayo Iringa.
Tanzania tupo kwenye giza Nene wakulima wadogo wanazulumiwa na watu wa lumbers bila kujali kuwa mkulima ametumia pembejeo za maafa na mbolea ya mangumashi. Itoshe tu kusema benki za kilimo hazipo tanzani mama anadanganywa na akina Bashe tu. Mimi niliwahi kumwandikia Bashe apitie kila kijiji apete taarifa za mwendendo wa mikopo kwamba wakiwa wachache wanakwamishwa na nini? Na wamekopa wangapi? Waliofanikiwa kimkopo wamepata changamoto na misukosuko gani pengine wameongo ili bender wajitoe muHanga.
 
BASHE mungu amekupa hicho cheo Ili uwafamyie kitu wakulima na hiyo nafasi itawasaidia hata ndugu zako wasomali waliokuwa wanaonekana ni MAJANGILI waonekane kumbe sio,na wewe BASHE upo kwenye mkoa ambao wabunge wake na raia wake wengi ni wakimbizi wa kongo,Rwanda,burundi,ambao jamii ya Kitanzania imekosa Imani nao katika UONGOZI wa Taifa hili,hatutarajii kuona na wewe unashindwa kuongoza hiyo wizara ya kilimo kwa kuwa unataka kuogelea bwawa la matope na wakimbizi wenzako wa Tabora,na nyie wenye uraia pacha tatizo lenu IPO siku mtafurumushwa na watz og,Kuna waziri wa kilimo mmoja enzi za MAREHEMU Nyerere alitokea Tabora ni Profesa,alifukuzwà uwaziri kisa wakati wa MSIMU WA kuvuna ikaonekana Kuna uhaba wa mazao ya chakula,kutafuta sababu ikaonekana wakulima hawàkuwa na mbolea ,akaomba pesa kwa Raisi kutàtua tatizo akapewa yeye akaenda kununua mbolea mwezi julai wakati wa mavuno ,huku marehemu Nyerere alimpa atununulie chakula. Cha msaada,huyu waziri kazi iliishia hapohapo.
 
Ila kumpa mtu mikopo akalimie inataka moyo
Yaani maoni haya unanikumbusha Kuna Rais wa hapa Tanzania aliwahi unganisha wizara ya kilimo na wizara. Ya maliasili na utalii ,sijui Nia yake ilikuwa nini Kama ukichunguza benki za nje nyingi zilizopo hapa Tanzania zinafuatilia sana wafanyakilimo wa dengu,korosho,ukwaju,u buyu na wanatoa mikopo kwa wale wanoweza tengeneza add value chàin kama kina mo,Manji nk mtu kama mo avac ya korosho akiitikisa tu tunatafutana hapa tz mpaka jeshi linatumika kubangua korosho lakini ujanja wote mtaalamu wake kamtoa wizara kilimo naye ni Mshindo Msola,ukijiuliza Kwanini Msola serikali ilimwacha unakuta ni SIASA chafu.
 
Ila kumpa mtu mikopo akalimie inataka moyo
Labda kilimo cha mboga mboga(green house).
Lakini hiki kilimo cha asili cha kutegemea mvua....ni ngumu sana kuaminika.

Mfano halisi ni kama huu mwaka na jinsi mvua zilivyokataa. Ni ngumu haswa!
 
Back
Top Bottom