Rais Samia unatupa wakati mgumu wanachama wa CCM

Rais Samia unatupa wakati mgumu wanachama wa CCM

Takataka yule na Nchi maskini usitumie kujenga hoja unajiaibisha.
Wewe msomi unafahama #Dutch disease or #Resource Course … Kama wapenda kusoma nakusihi soma ..

Hali ya Burkina Faso, ambapo Kapteni Ibrahim Traoré alichukua uongozi mwaka 2022 kupitia mapinduzi, inaweza kutazamwa kwa mtazamo wa “Laana ya Rasilimali” na changamoto zinazokumba nchi zenye utajiri wa madini. Burkina Faso, taifa lenye utajiri mkubwa wa dhahabu, limekumbwa na changamoto za umasikini, ukosefu wa utulivu wa kisiasa, na usalama duni, hali ambayo inatoa muktadha muhimu wa kupanda kwa Traoré madarakani.

Kutafakari Hali ya Burkina Faso na “Laana ya Rasilimali”:

1. Utajiri wa Madini na Umasikini:

Licha ya kuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa dhahabu barani Afrika, Burkina Faso bado ni moja ya nchi maskini zaidi duniani. Hii inaakisi “Laana ya Rasilimali,” ambapo utajiri wa madini hauleti maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya ufisadi, utawala duni, na utegemezi mkubwa kwenye sekta moja ya uchumi.

2. Ukosefu wa Utulivu wa Kisiasa na Changamoto za Utawala:

Mapinduzi yaliyomuweka madarakani Kapteni Traoré yalichochewa na kutoridhika kwa wananchi na serikali zilizopita, ambazo zilishindwa kukabiliana na vitisho vya usalama kutoka kwa makundi ya wanamgambo. Kushindwa kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya wananchi pia kulidhoofisha imani ya umma kwa viongozi wao, ambao walionekana kuweka mbele maslahi ya kigeni badala ya mahitaji ya kitaifa.

3. Kutoridhika kwa Vijana na Mgogoro wa Uongozi:

Idadi kubwa ya vijana nchini Burkina Faso imekumbwa na ukosefu wa fursa, hali inayoongezeka kwa sababu ya ukosefu wa usawa na huduma duni za msingi. Hali hii ilitoa nafasi kwa mabadiliko ya uongozi, huku Traoré akionekana kama kiongozi wa mabadiliko, ingawa changamoto za kuongoza taifa lenye mgawanyiko na changamoto za kiusalama ni kubwa.


4. Mchango wa Nguvu za Kigeni:

Kama mataifa mengine yenye utajiri wa madini barani Afrika, Burkina Faso imekumbwa na ushawishi mkubwa wa kigeni katika sekta yake ya uchimbaji madini. Mara nyingi, utajiri huo umekuwa ukinufaisha mashirika ya kimataifa badala ya jamii za wenyeji, hali inayochochea hasira na hamu ya kujitegemea.


5. Njia ya Mbele kwa Burkina Faso:

Ili uongozi wa Traoré uvunje mzunguko wa “Laana ya Rasilimali,” hatua muhimu zinapaswa kuchukuliwa:

• Utawala Jumuishi: Kuhakikisha kuwa mapato yanayotokana na dhahabu na rasilimali nyingine yanawanufaisha wananchi wote kupitia uwekezaji kwenye elimu, afya, na miundombinu.


• Kukabiliana na Changamoto za Usalama: Kurejesha utulivu na kulinda maeneo ya uchimbaji madini dhidi ya makundi ya wanamgambo ili kuunda mazingira salama kwa maendeleo.


• Kupambana na Ufisadi: Kuwajibika na kuwa wazi katika usimamizi wa utajiri wa madini ili kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa maendeleo ya taifa.


• Kuboresha Uchumi: Kupunguza utegemezi wa uchimbaji madini kwa kuwekeza kwenye sekta nyingine kama kilimo na viwanda ili kuunda ajira na kukuza maendeleo endelevu.



###Hali ya Burkina Faso inaonesha changamoto pana zinazokumba mataifa mengi ya Afrika yaliyo na utajiri wa rasilimali lakini yanayokumbwa na usimamizi mbovu####
 
1.Samia anajenga hactarws 500k za umwagiliaji Nchi nzima,na Bajeti ya 1.2 wengine wamewahi fanya?

Nionyeshe nataka twende kimoja baada ya kingine.Na nataka ushahidi Mimi ninazo nitakupa hapa.
Bei ya nyama imepanda sana, imekuwa kama anasa.
 
Shida sio kwamba Marekani hawamtaki mwanamke ila je ni mazingira yapi yamemfanya huyu mwanamke akose ushawishi

Bahati nzuri wenzetu marekani hawana mahaba niue katika chaguzi zao bali wanafanya maamuzi kutokana na sera za wagombea wao,yani ubora na uzur wa mgombea utategemeana na maono yake ya sera zake

Sasa kwa bahati mbaya sana mtangulizi au sera za democrat kwa kipindi fulani hazikuwa pendeza wamarekani wengi hivyo alivyokuja bwana Trump na sera mbadala na zenye mashiko watu wamemkubali

Kwahiyo ni swala la sera na dira ndio huamua hatima ya raisi wa marekani lakini sio jinsia,na weka kumbumbuku sawa kwamba ipo siku Amerika itatawaliwa na mwanamama

Kama ambavyo iliitwa white house ikulu yao kama code ya mtu mweupe kuwa ikulu lkn historia ilitupa Obama kama mtu mweusi ndani ya white house,stay tuned panapo majaaliwa inshallah mwanamke atakuwa pale white house
Kwa nini Wamarekani walimkubali Biden wakawakataa Kamala na Hillary Clinton??
 
CCM isitoboe Kwa nini? Kwa mfano tunaanza na wewe hapo unadhani hutaipigia kura ccm Kwa sababu zipi?

Sisi tunaeona mambo kama haya Kwa nini tusiwapigie kura? 👇👇

View: https://x.com/sisiniTanzania/status/1882053855451533568?t=eV2yMi4fcUBA5uLrFEI4xA&s=19

Juzi babati huko kuna mama kafariki baada ya kutopatiwa huduma hospital kisa mumewe kachelewesha tsh 150k ya matibabu. Huyo mama aligongwa na nyoka. Unaleta vituo vya afya lakini usimamizi zero na wahudumu ni hakuna, we unakua unaakili timamu?
 
Wewe sio mwanaume wala wewe sio mwanamke

Nadhani umenielewa

Mi 5 tena na Samia Suluhu Hassan

CCM YA SAMIA MBELE KWA MBELE
Nadhani hamjamjibu mleta uzi; anauliza Wasukuma, Wajita, Wakulya, Wayao na hata makabila mengine ya kihafidhina, yanaweza kumpigia KURA mwanamke? Makabila aliyataja, hayaamini katika uongozi wa mwanamke. Mjibuni hilo ili tuendelee mbele
 
Juzi babati huko kuna mama kafariki baada ya kutopatiwa huduma hospital kisa mumewe kachelewesha tsh 150k ya matibabu. Huyo mama aligongwa na nyoka. Unaleta vituo vya afya lakini usimamizi zero na wahudumu ni hakuna, we unakua unaakili timamu?
Sasa Huduma za Bure zinatokewa wapi? Kuna sera hiyo hapa Tanzania?
 
Ufisadi gani na hospital imejengwa na inaiona?
Kwa taarifa yako mimi nimeshasimamia miradi kadhaa chini ya uongozi wa Samia nayajua madudu ya CCM nje ndani kaa Kwa kutulia. Usimamizi mbovu, pesa zinaliwa hovyo miradi haiendani na pesa inayotolewa. CCM shida ni ninyi ma chawa mnamuangusha Rais Kwa ubinafs wenu na UFISADI
 
Siyo bure mtu kachelewesha kidogo tu PESA mnashindwa kumpa hata huduma ya kwanza. Haya nikuulize angekuwa ni mwenyekiti wa CCM asingepewa huduma?
Hiyo taarifa haijatoka Hadharani so Haina uhakika, taarifa za hivyo zimetoka sehemu zingine na mamlaka zikachukua hatua.

So acha uzushi
 
Kwa taarifa yako mimi nimeshasimamia miradi kadhaa chini ya uongozi wa Samia nayajua madudu ya CCM nje ndani kaa Kwa kutulia. Usimamizi mbovu, pesa zinaliwa hovyo miradi haiendani na pesa inayotolewa. CCM shida ni ninyi ma chawa mnamuangusha Rais Kwa ubinafs wenu na UFISADI
Nani hajasimamia miradi na lini pesa haijawahi liwa?

Swali , hospital mumejenga au hamjajenga? Wewe ulikuwa sehemu ya wezi si ndio?

Chadema huko hujasikia wamechagiana Kwa rushwa?
 
Nani hajasimamia miradi na lini pesa haijawahi liwa?

Swali , hospital mumejenga au hamjajenga? Wewe ulikuwa sehemu ya wezi si ndio?
Siwezi kufanya wizi Kwa wananchi wanyonge mimi it's better kujiweka pembeni wale wenyewe wenye roho za kishetani.

Machawa kama nyie mnatakiwa muuwawe
 
Ufisadi upo tena upo kweli kweli… Ndo yake tunasema mahaba na Chama ndo yanatupotosha … Mi Bus 🚎 30 na Mi posho ya ajabu…. Taarifa ya habari hapa tunaangalia Makada wanatoa ufafanuzi kila siku kisa nini … Naangalia Hapa Vijana vs Wazee wote wamepindisha maneno … Yani sisi tunakosea wapi “Ya Rabbi(أتُنصُرُنا)(يا رب، أتُنصُرُنا) … YANI NIKIMUANGALIA MH MWINYI, MH MAJALIWA, MH DOTTO nachoka 🤲🏽
 
Back
Top Bottom