Rais Samia, unawajua Wakenya?

Mpaka mama aamke usingizini na kuijua rangi halisi ya wakenya itachukua muda. By that time atakuwa ameshajijengea upinzani wa kutosha nyumbani. Viongozi wetu mahili, Mwalimu Nyerere na JPM waliwapotezea wakenya, mama asifikiri kuwa walikuwa wajinga kiasi hicho. Mtu yeyote anayeipenda Tanzania hawezi hata siku moja kuikabidhi kwa wakenya. Au hajui ni kwa nini enzi zile waliitwa nyang'au?
 
Boris mwenyewe kapeleka meli za kijeshi Jersey kupambana na wavuvi wa kifaransa
Wacha Mama acheze mziki wanaotaka kwanza ila akija kushtuka atapanga jeshi mpakani
 
wakenya sio watu poa kbsa kwanza ni wabinafsi , wajuaji na wana figisu sana na kama watawekeza tanzania hawana tofauti na wachina maana kwenye maslahi pia wanajijali wao kama wao kwanza, suala la hujuma pia wako vizuri mbona mifano ipo mingi tu yaani ni bora kufanya kazi na watu wa uganda kuliko wakenya
 
Asante kwa kutujulisha kuwa umeoa mkikuyu wa Kenya mliyekutana Australia. Ila kama haya mengine ndiyo mawazo yako basi nachelea kusema kuwa bado unaishi kwenye zama za miaka ya uhuru (sixties) tuliyokuwa tukiwaita wakenya manyang'au na exposure yako haijakusaidia kitu.

Huwezi kutoa lawama kwa taifa zima lenye watu milioni 50 bila kuwa na tuhuma dhahiri. Kwa hiyo kwa mtazamo wako huna shida na mzungu wa kutoka Canada na Australia kuja kuchimba madini ila shida yako ni hao wakwe na mashemeji zako ndio wana matatizo na wasije huku. Umesahau kabisa kuwa unaongelea wakwe zako, mashemeji zako, wajomba na mama wadogo wa watoto wako waliopo au wajao. Kwa akili hizi sisi tutaendelea kulalamika wakati wakenya wanawekeza kwetu.
 
hata wawekezaji wa tanzania walioko kenya ambao wamewekeza kwenye masuala ya madini hasa kwenye mambo ya elution na plant bado wanakutana na hujuma sana hapo kenya
 
Uwoga wa Watanzania ndiyo umaskini wao. Ni vizuri ufanye interaction na mtu mwerevu aliyekuzidi ndiyo utaona udhaifu wako.

Rais SSH yuko focused na well guided kuliko Mwendazake ambaye aliona Rwanda ndiyo role models wa Tanzania.
 
Marekani yenyewe unayoisema ndio inaongoza kuwa na wafanyakazi wa kigeni kuliko nchi zote duniani

Ndio nchi inayoongoza kununua bidhaa toka China kuliko nchi zote za America.

We jamaa vipi wewe uwekezaji gani unautaka?
Je, wajua kuwa wamarekani ndo wenyewe hivyo viwanda huko China, na walivihamishia huko ili kupa 'cheap labour' wa kichina katika kuzalisha bidhaa zao kwa wingi?
 
Kwenye ubinafsi ndio hapo napohofia tu maana sie watanzania ni social beings ila hawa wenzetu watakuja kutumia ile generous calibre yetu kutuumiza! It has nothing to do na uoga ila curiosity tu maana tulishaliona hili hata kwenye professionalism.

That is what selfish guys do na ndio maana wazee Jakaya na Magu waliamua kuwakazia at some point. Ngoja tuone tukiwakaribisha mpaka sebuleni hali itakuwaje maana kuna kundi linataka kuonja sumu kwa kuilamba ila nachowaza kwa ukabaji wao mpaka kwenye box la penati wakiingia kila sector watakao survive watakuwa akina Rostam, Dewji, Bhakresa and the like!
 
Inaonesha tunawaogopa Sana wakenya. Kama wanamitaji ya kuwekeza, Kama watazingatia Sheria yetu ya nchi, Kama watalipa Kodi na kutoa ajira kwa watanzania, Kuna haja gani ya kumuita mwekezaji wa mbali huko wakati majirani wetu wapo. Au tunawaonea wivu wakenya? Kama watacheza rafu na sisi si tutabadili msimamo wetu, maana lengo ni wote tufaidike, watanzania wanaoiona fursa Kenya waende wakawekeze na wakenya wanaoiona fursa Tanzania waje wawekeze. Tuache woga
 
Mama anapotoshwa, Yaani wenyewe wanabaguana kwa ukabila, ndio waje waelewani na Watanzania
Jamaa watakuja kubeba kila kitu na kuki brand made in Kenya hata viwanda vikiwa bongo! Nasubiria around 2025 matusi kwa mama Samia kuwa alikaribisha Nyang’au zilizopora fursa na kupeana mashavu wao kwa wao!

Mkenya anaweza pambana na mtu strong kama Mchagga labda ila sie milenda milenda wa pwani huku itabaki story! Nasubiria kusikia korosho zetu ziwe branded made in Kenya😅😂😂😅😅
 
Marekani yenyewe unayoisema ndio inaongoza kuwa na wafanyakazi wa kigeni kuliko nchi zote duniani

Ndio nchi inayoongoza kununua bidhaa toka China kuliko nchi zote za America.

We jamaa vipi wewe uwekezaji gani unautaka?
Jamaa unadanganya mno, yaani wafanyakazi wengi wa marekani ni wachina, marekani Ina import Sana toka China,
 
Tutaogopa Wakenya mpaka lini? Waje tujifunze maarifa, wakitushinda tunawaondoa.

Mhubiri 11:4 inasema "Anayengoja upepo hatapanda mbegu, anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu."
 
Tutaogopa Wakenya mpaka lini? Waje tujifunze maarifa, wakitushinda tunawaondoa.

Mhubiri 11:4 inasema "Anayengoja upepo hatapanda mbegu, anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu."
Sawa ngoja tuone
 
Umeoa mkenya alafu unasema sio watu, tushike lipi?
 
Nimekuelewa zaidi ya sana
 
msoga wanatuharibia hii nchi.

sijui ni viumbe kitoka sayari gani hawa!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…