Rais Samia, unawajua Wakenya?

Akili hizi, Kenya ndio wanaongoza kwa uwezaji hapa Tanzania kwa Bara la Africa, hao unaowaita wabinafsi, na ni wa 5 kwa dunia, zaidi ya 1.7b usd wamekeza.
 
Jirani akusaidie kuzuia mwizi kwako, mwizi anayeshirikiana na wanao Huyo jirani anaanzaje? Tanzanite haiwezi kuibiwa bila wa TZ wenyewe kubariki mkenya wacha afaidi mpaka tutakapo amka kweli. Tumelala sana bana nasi.
 
Hakuna nchi duniani, isiyojali raia wake kisa kuwekeza. Mataifa makubwa uangalia kuwapa uwezo raia wake wawekeze. Hakuna nchi iliyoendelea kwa uwekezaji toka nje. Si mara ya kwanza Kenya kuwekeza. Angalia miradi walio wekeza mfano kiwanda cha maziwa Arusha. Maziwa yanachukuliwa na wanaandika made in Kenya. Parking inafanyika Kenya. Kisha wanarudi kutuuzia.
Wameuwa general tyre. Kuna Insurance agency moja. Miaka ya nyuma kuanzia mkurungezi hadi karani walikuwa wakenya. Na huyu boss alikuwa rafiki yangu. Wote walofanya kazi walikuwa wakikuyu. Wanaukabila sana.
Nilishuhudia balozi wa Kenya waki lobby na kuongea na wafanya biashara kutumia bandari ya Mombasa bila balozi kutoa taarifa kuwa atakuwa na maongezi sehemu fulani ktk mkoa husika. Wakenya ni wajanja sana.
Mara ngapi wameingiza watalii wengi ktk mbuga na mlima kilimanjaro. Miaka fulani nimekutana na watalii wakanambia walipanda mlima Kilimanjaro kupitia Kenya na kutembelea Serengeti.
Tulipoteza kodi kiasi gani na hao wakenya wenu. Uwezi fungulia milango kiasi hicho. Kikubwa nchi yetu iangalie kuwawezesha wananchi waweze wekeza ndani. Hii inawezekana.
Angalia nchi ilovunja umoja wa Afrika Mashariki ilikuwa Kenya kwa tamaa zao. Wakakatalia baadhi ya mali za Afrika mashariki. Kenya inajua Tanzania ndo mshindani wake. Hivyo hawatatupenda toka moyoni. Sikatai uwekezaji lakini tuwe makini. Uwezi mfurahisha kila mtu. Wakenya si mara ya kwanza kuwa na tofauti. Tumekuwa nao tofauti toka kipindi cha Nyerere. Kuna wakati tulikuwa na vita ya maneno. Hadi kuitana Nyang'au. Tulikuwa na vita ya maneno na Malawi hao wote jirani. Uwezi kumchekea kila jirani ati diplomasia. Uchumi wa kidiplomasia si kuchekeana. Angalia Marekani na China.
 
Utaitwa sukuma gang sasa ivi na vijana wa bongo flava 😂😂
 
Sasa Malisa ana akili kweli?

Kama hayo akiyosema anaona ndio maslahi unategemea nini?

Mtu anaewaza mataga kukomolewa unafikiri ana akili tena huyo?
 

Ni WaTz wangapi wanakula na kushiba democracy na katiba mpya kama siyo hao wachache wanaotaka madaraka?

Hushangai wanaanza kumpamba Mama kwa lugha yenye kila pambio?

Ukiona adui anajipendekeza kwako ujue umenasa.
 
Wewe wasema nchi ni tajiri, hivyo hutofautiani na Rais aliyesema WaTz hawana mitaji ya kuwekeza kwenye ardhi na madini. Ila kumbuka Hayati alisisitiza nchi ni tajiri akaanza kujenga mazingira ya kuwawezesha WaTz kuwa mabilionea.

Kwa kufungua milango wazi ya uwekezaji, hata kwenye rasmali za nchi (ardhi, madini, mbuga za wanyama, nk - ndio utajiri wenyewe) ndoto hiyo ya hayati inayeyuka.
 
Mtanzania katika ubora wake wa kuishi na uoga na wasiwasi usio na sababu.

Tukumbuke kuwa mahindi yetu yamepatiwa ruhusa ya kuingia Kenya baada ya kukaa pale mpakani kwa miezi kadhaa.

Kenyatta katoa agizo mzigo uingizwe, Kenya ni soko la uhakika la mazao ya chakula.

Mzigo ungekwama maana yake huu unaoendelea kulimwa ungekosa pia soko. Umaskini kwa mkulima ungeendelea kuwepo na kukata tamaa kungefuatia.

Diplomasia ni muhimu sana na ni silaha ya mdomo kuliko ile hatari yenye kuambatana na watu kubeba bunduki.

Mama Liberata kapewa mambo ya nje na mojawapo ya kazi zake ni hii ziara ya Kenya.

Jirani yako huwezi kumkwepa cha muhimu ni kutafuta maarifa ya kuishi nae.
 
Hayati huyo huyo alisema kuwa hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu peke yetu.

Alisema maneno hayo mbele ya viongozi wa sekta ya madini na viongozi wa dini.

Hatuwezi kuishi kama visiwa, tunawategemea wa nje na wa nje wanatutegemea sisi.
 
Sababu, hakuna venye Wakenya watakuja Tz kuchukua tu biashara hiyo bila rukhusu, vibali au hata kuzuiwa kabisa sababu ya sheria mlizonazo ju ya migodi,
Tatizo lenu mna janja janja nyingi sana.

Unakumbuka kipindi cha nyuma Kenya ilikuwa inaongoza kwa kuuza tanzanite, vipi mna machimbo ya hayo madini huko kwenu?

Tunataka kufanya biashara na nyie ila kwa umakini wa hali ya juu...sio kwa ulegevu aliouonyesha mama.
 
Tunatengeneza reli hadi ili kumfaidisha kale kajamaa kamodo kaswahiba ka Shujaa halafu hata kwenye msiba hakuja 😀😀😀😀

Ila tuachage upumbavu Watanzania kwa hiyo Wakenya wakiingia TZ watachukua ardhi? Kwani sheria ya umiliki wa ardhi ipoje? Kenyatta mwenyewe mbali ya kuturuhusu kwenda Kenya lakini kasisitiza lazima iwe kwa vigezo vya kisheria vya Kenya. Tuache hizi mindset za kijamaa za miaka ya 70 zilizokua zinapigiwa chapuo na jiwe, tutalalamika milele tu. Tubadilike aisee

NB: Heko kwa Mwendazake mama anajimwambafy angani na kaka yake Bombardier aka Airbus, kitu kimenunuliwa kwa Cash
 
Mama anafanya kazi nzuri Sana, huu ulioweka hapa ni uchochezi.
Chapeni kazi achana na propaganda
#nipo na mama# kazi iendelee#
Enzi ya nyerere walivunja muungano, enzi ya kikwete walimuona si chochote na kijfanya wanajitenga kufanya yao, enzi ya magufuli kila siku wanafunga mipaka mara wazuia magari mara vyakula bila sababu
Unategemea kwa samia wataheshimu kitu hawa?

Wao wametoa ofa ya kufanya biashara na kazi bila vibali kuwatega, kisha nyie nao mjichanganye muone.

Kenya wewe utawekeza wapi kama kila sehemu zinamilikiwa na watu,
Je nyie watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kenya mpo wangapi?
Na matawekeza kwenye nini?

Tanzania kila sehemu tuna vitu vya kuwekeza kuanzia madini ardhi maziwa na mito, kisha wawekeze na nwao watake wafanyakazi wao wapewe vibali vya kazi bila mashart uone kama mtanzania atapata kazi kwenye huo uwekezaji labda awe anatumika tu kwa maslahi yao,

Mtaingizwa force king kisha mnauliwa kweupe.
Wacheza draft wanajua.
 
Mijitu mingine hewa kabisa ,eti mama unaijua Kenya?, we kweli akili yako imekosa oil,hivi unafikiri samia ni kisoda kama wewe au aliamka tuu akajipodoa akaamsha popo kwenda Kenya , unafikiri anafanya maamuz kama wewe ulivyofanya maamuz ya kutupia huu Uzi bila kushirikisha halmashaur,bichwa kubwa akili ya kuku
 
Hayati huyo huyo alisema kuwa hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu peke yetu.

Alisema maneno hayo mbele ya viongozi wa sekta ya madini na viongozi wa dini.

Hatuwezi kuishi kama visiwa, tunawategemea wa nje na wa nje wanatutegemea sisi.
Hakika hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu pekee au kuishi kama kisiwa, lakini vile vile hatuwezi kushindana pasipo na mazingira yaliyo ya usawa na rafiki. Ni jibu tosha la hoja yake Phillipo Bukililo, kwamba tuwe makini na Wakenya ambao hadi kesho wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani. Wayatendayo kwa jirani zao mipakani (Uganda, Tanzania, Somali) yanatosha kueleza jinsi walivyo. Isitoshe tuna majirani zaidi wa kufanya nao biashara kuliko Kenya.

Swali la kujiuliza ni kwa nini Uhuru ghafla alimwarika Rais SSH mara tu baada ya kuhutubia Bunge letu? [emoji848]
 
Marekani haina wafanyakazi wa Kigeni wa machinga, inachukua cream kutoka kwenye mataifa mengine.
Hizo "krimu" ni pande moja tu, wana mamilioni ya watu kutoka Meksiko, Amerika ya Kusini wanaovuna matunda kwenye mashamba kwa mishahara duni , kufanya kazi ya mtumishi wa nyumbani . . .. .
 
Mkuu yani inauma sana.....kwenye madini hapo ndo kule tanzanite ya Tz lkn nchi inayoongiza kuuza ni keny,s.africa.....oh mara india....ujinga huu hauvumiliki kwa kweli
 
Mnaosema wakenya wabinafs , sijui wanakuja kuchukua madini haya tuoneshen taifa ambalo halina hizo sifa
 
Mkuu, kenya ni Hatari sana, yaani hatutakubali eti waje washike vitalu vya madini, yaani hawa tukiwaruhusu Watanzania watabaki maskini wa kutupwa
Ajira wazitajazo zitokanazo na uwekezaji ni politics tu and short consideration......tunaacha long run consideration....du very painful
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…