Rais Samia, unda Tume kuchunguza kupigwa risasi Tundu Lissu

Mkulima

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Posts
1,236
Reaction score
1,546
Mama Samia, Rais wetu mpendwa,

Unda Tume ya watalaam wetu wa ndani na nje kuchunguza kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, kupotea kwa Saanane Pamoja na watu wengine.

Kama nchi tunaonekana wa hovyo sana kuwa na serikali ambayo haiko tayari kujua kilichowapata raia wake.

Tunafananishwa na Kenya ya hovyo ya miaka ya 80 wakati wa Moi.

Hivi unajisikiaje ukisikia kilio Cha Mamake Saanane? Kijana maskini ambaye aliamua kujipa elimu mpaka kukaribia kuwa Dr wa Ph.D kwa faida ya familia yake?

Sisi sio wanyama, ni binadamu, haiwezekani tukawa Linda watu waovu. Jisafishe mikono yako kwa kuruhusu vyombo vya dola kutoa Majibu ya haya matukio.

Watu wanaweza kukaa kimya Lakini kwa ujumla unaonekana Huna Huruma kwa mwanamke mwenzako, Mamake Saanane Pamoja na wengine wote waliopotezwa. Kukaa kimya maana yake na wewe ulikubaliana na unyama huo.

Mama Mimi nakupenda sana Lakini kwa kukaa na uchafu huu, hapana, Hata Siwezi kukusogelea. Mikono yako ina damu za hao waliouliwa.
 
Aliyepigwa risasi amesema aliyempiga ni Maghufuli , sasa Kwa nn msiende Moja Kwa moja kumkamata mtuhumiwa , mnaunda time ya kupeana posho wakat mhusika anajulikana mhanga amemtaja
 
Why Lissu na Saanane? Tuna watu wengi wameuawa kama wakina Dkt Mvungi, wakina Amina Chifupa, Chacha Wangwe, Akwilina, Azory na wengine wengi akiwamo kijana wa NCCR Mageuzi alitoweka hapa majuzi na kukutwa kapigwa na watu wasiojulikana! Kwanini Lissu na Saanane tu?
 
Hoja maridhawa mh rais kumbuka Kuna chawa wa ccm huku mitandaoni wanasema lisu alijipiga risasi mwenyewe na wengine wanasema ni mbowe na wanaenda mbali kutengeneza conspiracy theories za kijinga eti chachawangwe aliuliwa na mbowe na lisu pia Sasa mama hebu wapruv wrong Hawa chawa wako! Ujitenge nao!
 
Hii serikali utafikiri ya Moi iliyowachoma moto mashambani akina Ouko.

Ni Aibu sana kwa nchi inayoheshimu sheria na kujali Utu, kukaa kimya wakati wananchi wake wamepotezwa.

Namuonea Huruma sana Mamake Saanane.
 
Why Lissu na Saanane? Tuna watu wengi wameuawa kama wakina Dkt Mvungi, wakina Amina Chifupa, Chacha Wangwe, Akwilina, Azory na wengine wengi akiwamo kijana wa NCCR Mageuzi alitoweka hapa majuzi na kukutwa kapigwa na watu wasiojulikana! Kwanini Lissu na Saanane tu?
Acha unafiki akiguswa jiwe unawashwa sio!?
 
Why Lissu na Saanane? Tuna watu wengi wameuawa kama wakina Dkt Mvungi, wakina Amina Chifupa, Chacha Wangwe, Akwilina, Azory na wengine wengi akiwamo kijana wa NCCR Mageuzi alitoweka hapa majuzi na kukutwa kapigwa na watu wasiojulikana! Kwanini Lissu na Saanane tu?
Soma vizuri post. Ni Lissu, Saanane Pamoja na wengine wote waliopotezwa au kuumizwa.
 
Rais Samia anapenda haki ila anashindwa afanyeje Mana wahusika hata yeye anawafahamu kwa nafasi aliyopo Sasa alishapewa a,b,c za hilo tukio na vyombo vya usalama ndo Mana kafanya na mageuzi ktk vyombo vya usalama. Ukweli anaujua wote waliohusika kupoteza watu anaogopa kufanya maamuzi ukizingatia ni mwanamke hawezi kuunda tume ya uchunguzi
 
Mama Samia, Rais wetu mpendwa,

Unda Tume ya watalaam wetu wa ndani na nje kuchunguza kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, kupotea kwa Saanane Pamoja na watu wengine.

Kama nchi tunaonekana wa hovyo sana kuwa na serikali ambayo haiko tayari kujua kilichowapata raia wake.

Tunafananishwa na Kenya ya hovyo ya miaka ya 80 wakati wa Moi.

Hivi unajisikiaje ukisikia kilio Cha Mamake Saanane? Kijana maskini ambaye aliamua kujipa elimu mpaka kukaribia kuwa Dr wa Ph.D kwa faida ya familia yake?

Sisi sio wanyama, ni binadamu, haiwezekani tukawa Linda watu waovu. Jisafishe mikono yako kwa kuruhusu vyombo vya dola kutoa Majibu ya haya matukio.

Watu wanaweza kukaa kimya Lakini kwa ujumla unaonekana Huna Huruma kwa mwanamke mwenzako, Mamake Saanane Pamoja na wengine wote waliopotezwa. Kukaa kimya maana yake na wewe ulikubaliana na unyama huo.

Mama Mimi nakupenda sana Lakini kwa kukaa na uchafu huu, hapana, Hata Siwezi kukusogelea. Mikono yako ina damu za hao waliouliwa.
Ni ushauri mzuri na akifanya hivyo atapaswa aongezewe degree nyingine kubwa ya udoctor naamini moyoni mwake anayo hofu ya Mungu lazima tutamuita mama wa Taifa kwakuwa tayari tuna baba wa Taifa hivyo nguzo ya taifa itaimarika
 
Yaliyopita si ndwele. Tugange yajayo.
Shetani anafanya mambo yake kwa siri
Lakini pia Shetani anapenda sifa,anataka watu wajue amefanya nini.
Kwa hiyo hao jalili huwa wanajitaja.
 
Why Lissu na Saanane? Tuna watu wengi wameuawa kama wakina Dkt Mvungi, wakina Amina Chifupa, Chacha Wangwe, Akwilina, Azory na wengine wengi akiwamo kijana wa NCCR Mageuzi alitoweka hapa majuzi na kukutwa kapigwa na watu wasiojulikana! Kwanini Lissu na Saanane tu?
Soma vizuri. Nadhani mleta mada amesema, amemtaja Lisu, Sanane, halafu akasema pamoja na wengine ambao waliuawa, kushambuliwa na kutekwa na hao wanaoitwa wasjojulikana, japo ukweli ni kwamba wanajulikana.

Kuhusu baadhi ya uliowataja, naona pia labda hukuwepo Tanzania, umefanya kusimliwa.

Amina Chifupa hakuuawa wala kushambuliwa. Kilikuwa kifo cha kawaida.

Wangwe kifo chake kilikuwa ni ajali, na kesi ilifika mahakamani, na aliyehusika na ajali alihukumiwa. Bahati mbaya kifo chochote kinachotokana na ajali ya gari ni traffic offence siyo murder case, hivyo adhabu yake siyo kubwa sana.

Akwilina inafahamika aliuawa na Polisi. Hapa tuitake Serikali kuwashtaki Polisi waliohusika na mauaji yale.

Azory Gwanda, upo sahihi. Hakuna taarifa yoyote rasmi. Pia yupo Kanguye, wapo madiwani wawili kupitia CHADEMA. Hawa wote, ukifuatilia, mikasa yao inatokana na kuikosoa Serikali au kumkosoa Rais Magufuli. Swali linakuja pia kuwa je, kushambuliwa, kutekwa au hata kuawa kwao yalikuwa ni maagizo ya moja kwa moja ya Rais Magufuli au wahusika waliyatenda hayo kumfurahisha mtawala? Kama yalikuwa ni maagizo yake, tujue yalikuwa maagizo yake ya jumla au specific kwa mtu fulani halafu watekelezaji wakaendelea na kwa watu wengine?

Pia kuna kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka. Hakuna taarifa rasmi. Huyu naye inaaminika ni kazi ya hao hao wasiojulikana. Pamoja na mauaji ya kule Arusha, mauaji ya Mawazo, yote yanaendana na harakati za kisiasa. Kukiundwa tume, lazima yatazamwe haya yote. Uovu ni uovu tu bila ya kuangalia ulitendwa wakati wa utawala upi.
 
Aanzishe tume kuchunguza ufisadi mkuu unaondelea nchini kwetu na achukue action, alafu aipende na kuionea huruma hii nchi yetu, maana wageni wengi wamepata fursa za ajabu sana!
Awaonee huruma vitukuu vyetu jamani!
Hayo mambo ya lisu tumshukuru Mwenye Enzi Mungu kwamba amepona na mambo yaishe tujenge nchi, sio kila siku ni “kupigwa risasi kwa lisu kupigwa risasi kwa lisu” tumesha choka na hiyo taarabu walahi loooo[emoji35]
 
Makaburi yafukuliwe, maziwa, bahari, mito, mifereji, visima vikaushwe tujue ukweli....kuna vifo vingi vilivyojengewa njama. Itakuwa vyema tujue ukweli. Nakiri kusema mwanahudhuri mmoja katika posti yake juu ameweza kunena vizuri bila ya njama njama na kuonyesha vidole moja kwa moja...lazima watu wajirudi na kutubu.

Hatahivyo Tusianze kuanzisha Tume kwa Huruma peke yake.
 
Mama Samia, Rais wetu mpendwa,

Unda Tume ya watalaam wetu wa ndani na nje kuchunguza kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, kupotea kwa Saanane Pamoja na watu wengine.

Kama nchi tunaonekana wa hovyo sana kuwa na serikali ambayo haiko tayari kujua kilichowapata raia wake.

Tunafananishwa na Kenya ya hovyo ya miaka ya 80 wakati wa Moi.

Hivi unajisikiaje ukisikia kilio Cha Mamake Saanane? Kijana maskini ambaye aliamua kujipa elimu mpaka kukaribia kuwa Dr wa Ph.D kwa faida ya familia yake?

Sisi sio wanyama, ni binadamu, haiwezekani tukawa Linda watu waovu. Jisafishe mikono yako kwa kuruhusu vyombo vya dola kutoa Majibu ya haya matukio.

Watu wanaweza kukaa kimya Lakini kwa ujumla unaonekana Huna Huruma kwa mwanamke mwenzako, Mamake Saanane Pamoja na wengine wote waliopotezwa. Kukaa kimya maana yake na wewe ulikubaliana na unyama huo.

Mama Mimi nakupenda sana Lakini kwa kukaa na uchafu huu, hapana, Hata Siwezi kukusogelea. Mikono yako ina damu za hao waliouliwa.
Apotezee tu kwani Mungu ameshatoa hukumu yake tayari aliyeagiza Lissu auwawe sasa hivi amekuwa kuni za kuwachomea waovu wenzake huko jehanam
 
Back
Top Bottom