Rais Samia ungana na upepo wa Paul Makonda

Uzalendo sio lazima uvae bracelets, scarf, tie n.k vyenye rangi ya bendera ya taifa.
Unachokifanya ndio uzalendo, wala sio limbwata. Hatuna chaguo, ispokuwa kumpenda na kumlinda kwa ajili ya taifa.
Amiina
 
Mhe. Mwenyekiti wa CCM Ndugu Samia Suluhu. Kwanza nikupongeze kwa kumpa nafasi Makonda. Umefanua jambo kubwa pengine zaidi ya kile ulichokilenga.

Wengi wanaamini kuwa umerudhisha fadhila kwa kijana aliyepanda mbegu ya fikra ya uteuzi wako kama mwanamke wa kwanza kwa nafasi ya Makamu wa Rais. Kwa ni fadhila pia hongera maana sio wote wenye moyo wa shukurani.

Sasa Kijana ameanza kazi kwa kasi na style tofauti na yako.

Jambo la kusikitika ni pale kijana anafanya kazi ya kuibua maovu katika mikutano yake na wakati mwingine inahitajika mamlaka za juu au za uteuzi ili kushughulikia changamoto.

Kwa mamlaka ya MAKONDA, hawezi kutumbua au kumsimamisha kazi mtumishi wa umma.

Ni vema Rais ukajitokeza katika mikutano hiyo kwa njia yaaamuzi. Piga simu moja kwa moja au uweke access ya kufikia maamuzi ya haraka ili kuonesha kuwa Makonda yupo kukuwakilisha.

Labda kama hutambui jambo moja ambalo watanzania wanataka kuona ni uwajibikaji.

Panapotokea Shaka yoyote katika utendaji wa mtu Serikalini, angalau basi chukua hatua za kumsimamisha apishe uchunguzi.

Sasa Kila Kona Makonda anakutana na kero na uonevu, lakini hana malaka.

Itafikia hatua Makonda atakua maarufu kuliko aliyemtuma kazi.
Tusi kubwa kwa Rais hilo.
 
Wassukuma hamna akili,japo ni watani zangu
 
😂😂hawezi
Miaka sabini mchezo🤣🤣
Mwili ushachoka harakati zako
 
Makonda anafanya kazi sana nafurahishwa na upepo aliokuja nao kijana acha akipaishe chama cha mapinduzi, mazimgira yake ya kazi ni magumu lakini amejitahid kufanya kazi kamilifu
Mazingira yake ya kazi ni magumu, wakati msafara wake una magari zaidi ya 100 tena mengi yakiwa ya serekali?!
 
Makonda anafanya kazi sana nafurahishwa na upepo aliokuja nao kijana acha akipaishe chama cha mapinduzi, mazimgira yake ya kazi ni magumu lakini amejitahid kufanya kazi kamilifu
Nyie mnaona anakipaisha Chama chake?
Kwa wenye akili wanaona jinsi gani anavyo kivua nguo za ndani chama chake! Hivi wale mamia ya wanao kusanyika na kumsikiliza akiwapopoa watumishi wa serikali watakapo patabuelewa kuwa serikali hii ambayo Makonda anaonyesha ilivyo dhaifu, haiwajibiki, ufisadi mwingi na haijali wananchi imeundwa na Chama hicho hicho cha CCM anachokiwakilisha huyo Msanii watakichukuliaje?
Watakidharau na kukichukia huku wakiungana na waliyokuwa wakisikia yanasemwa na Wapinzani siku zote.
Unaweza kuwadanganya watu wote wakati fulani, lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote.
Na mkumbuke mitaani wamejaa graduates wa vyuo na shule za sekondari wanaelewa upi ukweli ipi Sanaa
 
Back
Top Bottom