Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

sisi sio wajinga, tumeona ulichokuwa ukikitetea humu. wewe ulikuwa fan mkubwa sana wa chadema, alipoingia msukuma mwenzako ikulu hukuwahi kuona kasoro zozote juu yake, kila alichofanya ulitetea isipokuwa vichache sana ambavyo ulikosoa kinafiki. msukuma mwenzako (kama ilivyokuwa kwa JK) alifanya mengi mazuri lakini yapo pia mabaya mengi tu aliyofanya; during JK era uliona mabaya tu yake, but was opposite during msukuma's era. so we know who you are.
either, in a rare case, unaweza ukawa mkatoliki uliyepindukia; pale mkatoliki mwenzako slaa alipoondoka chadema na mkatoliki mwengine kuingia ikulu uliambatana nao! (this goes to mwanakijiji pia)

kwa hiyo we kosoa tu (constructive criticism) that's not a problem and we'll still take it, but at least some of us knows your mwelekeo!
Weka ushahidi wa hayo madai yako!

Ukishindwa kuweka ushahidi, wewe ni mzushi na nyumbu.

Na si mzushi uliye nyumbu tu. Ni mzushi uliye zuzu, zumbukuku, na juha kama jiwe.

Na najua huwezi kuweka ushahidi wowote ule wa hayo madai yako kwa sababu umezusha.
 
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
Asante kwa uchambuzi mzuri na makini.
 
1. Fikra ni huweza kubadilishwa kupitia elimu

2. Tukiweza kubadilika hapo kwenye nambari 1, ina maana nambari 2 haitakuwa kikwazo
Nakubali,
....Kwa hiyo mfumo wa Elimu yetu ufumuliwe wote kabisa!

Unashauri vitu gani ktk mfumo wetu wa elimu?
 
Upo sawa kabisa. Ni lazima kuja na vitu kadhaa
1. Kupunguza matumizi kwa kuhakikisha matumizi mazuri na sahihi kwa fedha tulizo nazo.

2. Tufanye miradi ambayo itaongezea taifa mapato. Mfano, mradi wa umeme wa maji tuta wauzia nchi za SADC.

3. Kuhakikisha mali asili zetu kama taifa zina tusaidia. Vitu kama madini, mbuga na bahari.

Bila hivyo, hatuvuki. Tutabaki kulalamika miaka nenda radi.
Hapa nakuunga mkono, lazima twende KIMKAKATI
 
Nchi ambayo 75% ya watu wake ni wakulima wa kujikimu ndani ya uelewa mdogo! maarifa na sayansi katika kilimo ni ndogo sana.
Kiujumla ujinga ni mwingi.
Kuisogeza hii nchi mbele ni lazima ulete mapinduzi makubwa kwa walio wengi yaani wakulima. Elimu yao, teknolojia, masoko ...
Uongozi si lele mama.
Naishi mjini na pia nakaa kijijini km 60 kutoka mjini pasu kwa pasu. Kuna tofauti kubwa sana.
Kuna shida
 
Nashukuru kwa kuchangia mjadala huu.
Tena heri wewe unashuhudia ya vijijini.
Mimi nimekulia kijijini, na ndugu zangu 90% wapo vijijini.
Japo nipo mjini ila hutembelea wilaya mbalimbali.

Anayeona ile hali hawezi kupuuza kwamba hali sio nzuri.

Na kwa nini sekta muhimu za kuwainua Watanzania zinaonekana ni ziada kwa serikali?

Mfano Kilimo.

Je, viongozi wetu wanachukuliaje?

Tutavuka kweli?
 
Wewe ndio haupo serious na mambo madogo kama hayo,
Hivi wewe unaweza kumnunulia mtoto biscuit au pipi ukitoka kazini kweli???

watu wengine bwana, kama huna cha kuongea kaa kimya na chuki zako
kwa hiyo kununua mashuka na kugawa hospital kwako wewe unaona ni ajabu? acha umang'aa wewe
 
Hakuna popote Duniani, Rais wa nchi anaweza kufanya kitu kama hicho.

Ni Tz tu, na atapata Chawa kama wewe wa kusema hewala!!

Cc: Mwitore
 
Mimi huwa naamini ili tuendelee si lazima sana kuwa na Rais wa haja ya mioyo yetu au mchapakazi sana n.k.

Ili waafrika tuendelee tunahitaji
1. Kubadili fikra zetu kutoka kuwa tegemezi na kuwa na fikra vumbuzi/tatuzi...

2. Kutunza rasilimali tulizonazo, na kuhakikisha zinatufaidisha, hili lilipaswa kuwa ni jukumu la kila mwenye dhamana...kama madini tuliyonayo yangelikuwa managed vizuri pengine leo hii tusingekuwa hivi tulivyo...
Ulichokisema nakiunga mkono kwa 100% lakini ili hayo yote yatimie ni lazima tuwe na kiongozi mwenye uthubutu,asiyeyumbishwa,jasiri na asiye na ubinafsi .Tatizo linatukabili sisi Wa Afrika viongozi wetu wengi Ni wabinafsi wanapoingia madarakani wanaishi wakilinda nafasi zao na mali zao hawajitoi kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.viongozi wengi wa nchi zetu wanayatengeneza matatizo kwa wananchi ili waje wayatumie Kama mtaji wa kisiasa.
 
Umenifanya nikumbuke vijiji fulani mkoa wa Morogoro (navihifadhi kwa majina) magari hayafiki huko na watoto wadogo wanasikia tu kuna vitu vinaitwa magari hawayajui. Pia kwenye vijiji vya delta ya mto Rufiji hali ndio hiyo. Kwenda shule na hospitali lazima uvuke mto, hamna umeme pia. Na hawa kipindi cha uchaguzi wanapelekewa masanduku ya kupigia kura.

Tuli Daslma tunaona mambo ni swafi kabisa...!!
uli Daslma tunaona mambo ni swafi kabisa...!!
Na Dar inategemea maeneo gani unaishi. Ukipita Mbezi, Masaki, Obey tofauti kabisa na Vingunguti bom bom, yombo nk.
yaani umasikini ni wa hali ya juu sana.
Hii nchi inahitaji ukombozi kwa mara ya pili
 
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
I cannot say more!
 
Ulichokisema nakiunga mkono kwa 100% lakini ili hayo yote yatimie ni lazima tuwe na kiongozi mwenye uthubutu,asiyeyumbishwa,jasiri na asiye na ubinafsi .Tatizo linatukabili sisi Wa Afrika viongozi wetu wengi Ni wabinafsi wanapoingia madarakani wanaishi wakilinda nafasi zao na mali zao hawajitoi kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.viongozi wengi wa nchi zetu wanayatengeneza matatizo kwa wananchi ili waje wayatumie Kama mtaji wa kisiasa.
MAy JPM Rest In Peace! Amen!
 
Back
Top Bottom