Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Hiyo Miaka 10 au 15 ni ya marejesho. Inaonekana umezaliwa miaka ya 2,000. Hivyo vyote vilikuwa enzi za Nyerere, ila vilikosa mwendelezo. Bomba la mafuta la Zambia, Reli ya Tazara, ndege nyingi, viwanda vya kutosha vilikuwepo enzi za Nyerere. Mabwawa ya umeme pia yalikuwepo na bado deni halikupanda kwa hivi. Umepigwa propaganda juzi ukaona ndio hivyo, hata uwezo wa kujiuliza uwiano wa deni na miradi huna, umebakia kunitajia miradi kwa wingi, lakini hata thamani yake
MKUU PESA ZIPO TENA NYINGI SANA.
Tazama huko bungeni na BOT wanavyokula helza zetu kwa kulipana mabilioni....
Watu waumize vichwa namna ya kujitoa kwenye tatizo hili la matibabu, other wise ukizungumzia serikali tu na kodi zinaweza kumaliza hili tatizo,tutasubiri sana!

hivi kama kila mtanzania (60m) akichangia bima ya afya kwa sh 1000 tu kwa mwaka, hizo ni sh ngapi (6Tr) , haziwezi kweli kusaidia matibabu, au tuna umaskini mkubwa namna hiyo kiasi kwamba hata sh 1000 ni tatizo kwa familia zetu? Mimi siamini, nadhani bado kuna tatizo kubwa la kukuna vichwa kwa tunaowatedemea
 
Nashukuru umenijibu ila nadhani hujaelewa swali langu vizuri.
Achana na mambo ya riba,mfano ni huu
Kama mwaka 2010 nimekopa dola 20,000 za kimarekani (kwa thamani ya tsh labda 40,000,000) na miaka mitano mbele thamani ya dola dhidi ya pesa za ndani (tsh) ikapanda. (ile dola 20,000 inathaminishwa kama 50,000,000). Je,kwanini upandaJi wa deni la taifa unathaminishwa katika tshi (inayoshuka thamni kila siku) wakati tumekopa in terms of dollar?
Umekopa dolla elfu 2,absa benki usd ikiwa 2000Tsh,imefika 2030,usd ipo 3000Tsh,.......by the way kwa muda huo deni lako ni USD 2000X3000.
========
Haya 2030,1 usd imekua 1000Tsh......deni lako litakua 2000X1000.
==========
Note.
Nyerere hadi JK walikopa Trillioni 40,kwa miaka 50,JPM peke yake amekopa Trillioni 27 kwa miaka mitano ,,sawa na 60% ya deni lote
 
Naomba kueleweshwa kidogo kuhusu ukubwa wa deni la taifa.
Hili deni huwa linathaminishwa kwa Tsh au USD?
Hoja yangu iko hapa; mwaka 2015 wakati JPM anaingia madarakani thamani ya tsh ilikuwa 1800+ kwa dola moja ya marekani na kufikia 2021 thamani imepanda hadi 2300+. Je,kama 2015 mlidaiwa tsh 38T za kitanzani,thamani yake itaendelea kuwa hiyo hiyo au itabadilika kulingana na kupanda ama kushuka kwa dola ya marekani?
Samahani kama niko nje kidogo ya mada ila kuna utata kuhusu nani amelikuza hili deni parefu kati ya marais 3 waliopita.

Tazama ni kipi kimefanya hiyo $ kupanda, majibu yako humo boss.
 
Upo sawa kabisa. Sijajua huwa wana hesabu vipi. Ngoja nifuatilie. Maana tunakopa kwa USD ila tuna hesabu ka TSh wakati interest rate ni tofauti.
Interest rate ya riba ni ile ile tu ........sema inflation rate ya Tsh ni kubwa mno[emoji16]........
Note.
Africa rais anataka historia liwe somo la lazima kuanzia chekechea,[emoji16]baada ya uchumi,......matokeo yake ndio haya degree holder hajui tofauti ya interest rate na inflation rate[emoji119][emoji3][emoji3]
 
Tuongeze vyanzo vya mapato hapo ndipo tutaweza kusema wazee na watoto wote matibabu bure.....umasikini mkubwa sana vijijini huko hata buku kwa siku mtu hapati...ni shida sasa Rais atafanyeje ? Kwa sasa hana ubavu wowote hata aje nani ....labda siku tukipata pesa za mafuta uganda zitasaidia sana mno boast revenue ....kupunguza makali umasikini ....masna watalipa pesa kubwa sana mwaka 75% bajeti yetu sasa....hapo tutajidai kidogo kupambana umasikini lakini sio kwa bajeti hii 65% tunasaidiwa donors.....
Upo sawa kabisa. Ni lazima kuja na vitu kadhaa
1. Kupunguza matumizi kwa kuhakikisha matumizi mazuri na sahihi kwa fedha tulizo nazo.

2. Tufanye miradi ambayo itaongezea taifa mapato. Mfano, mradi wa umeme wa maji tuta wauzia nchi za SADC.

3. Kuhakikisha mali asili zetu kama taifa zina tusaidia. Vitu kama madini, mbuga na bahari.

Bila hivyo, hatuvuki. Tutabaki kulalamika miaka nenda radi.
 
Naomba kueleweshwa kidogo kuhusu ukubwa wa deni la taifa.
Hili deni huwa linathaminishwa kwa Tsh au USD?
Hoja yangu iko hapa; mwaka 2015 wakati JPM anaingia madarakani thamani ya tsh ilikuwa 1800+ kwa dola moja ya marekani na kufikia 2021 thamani imepanda hadi 2300+. Je,kama 2015 mlidaiwa tsh 38T za kitanzani,thamani yake itaendelea kuwa hiyo hiyo au itabadilika kulingana na kupanda ama kushuka kwa dola ya marekani?
Samahani kama niko nje kidogo ya mada ila kuna utata kuhusu nani amelikuza hili deni parefu kati ya marais 3 waliopita.
Uwe unasoma soma na kusikiliza media nani kamwambia 2015 dollar moja ilikuwa 1800 ,hizo takwimu umetoa wapi ndugu
 
Uwe unasoma soma na kusikiliza media nani kamwambia 2015 dollar moja ilikuwa 1800 ,hizo takwimu umetoa wapi ndugu
Hawa ndio wananchi wazalendo wa Tanzania.....waliosoma shule za uchumi wa kati[emoji3][emoji16][emoji16]
 
Interest rate ya riba ni ile ile tu ........sema inflation rate ya Tsh ni kubwa mno[emoji16]........
Note.
Africa rais anataka historia liwe somo la lazima kuanzia chekechea,[emoji16]baada ya uchumi,......matokeo yake ndio haya degree holder hajui tofauti ya interest rate na inflation rate[emoji119][emoji3][emoji3]
Actually nilitaka kuandika Exchange rate. Maana kwa maelezo niliyo toa, siyo inflation rate kama unavyo sema na pia siyo interest rate kama nilivyo andika.
 
Actually nilitaka kuandika Exchange rate. Maana kwa maelezo niliyo toa, siyo inflation rate kama unavyo sema na pia siyo interest rate kama nilivyo andika.
Enhe andika sasa vizuri ili tundeleee kuweka data mezani,ndugu mtanzania mzalendo[emoji16][emoji3]
 
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
Well said. Watu hawana Nyumba lakini tunambiwa estapelekewa umesema. I just don’t get it mukuchika et al wakiugua wana ends nje kwa kodi yetu. Mimi mkulima naenda hospitali ya wilaya na malolactic when I have no income. Hata kuzikana, wao wanazikwa kwa hela zetu. Eti uchumi wa kati. Haya wana siasa wana akili ya kuku, ndiyo maana bunge likajengwa karibu na Milembe hospitali. Kila kitu imekuwa Mungu mungu, just to fool us, Kama kweli kuna Mungu mbona hawaogopi kuiba hela za serikali au kunitumia ovyo see majumba wanayopeaana, those 2 houses could build a school in each village, they deserve it, really? Has anyone checked how much money they have in foreign countries. Ex presidents not to be prosecuted, that is sheria, wamefanya mambo ovyo, wizi etc Waikijua wana kinga. It makes me sick hata wanapoapishwa eti maadili. Where?
 
CWR2016 umetoa hoja nzuri na inayohitaji tafakuri. Mojawapo ya chanzo cha ufukara unaozungumzia na ambao ni kweli kabisa ni UFISADI (sio kwa maana ya 'kamusi' ya CCM) bali katika maana halisi ya dhana ya kleptocracy ('wizi' wa mali ya umma uliohalalishwa na walioshikilia madaraka). Kwa mfano ni mishahara na posho za waheshimiwa wabunge.

BUNGE ni kleptocracy iliyosukwa wakati wa awamu ya Mkapa. Hii ningeiita SUSTAINABLE KLEPTOCRACY ambapo wanasiasa watawala wanajihakikishia wao na familia zao zinaneemekea (chukua mfano wa Jakaya Kikwete, leo hii anapata mafao ya ustaafu wa urais, mtoto ni mbunge, mke ni mbunge,na soon hata mjukuu atakuwa mbunge; Hayati Sitta, alikuwa mbunge na mama mbunge, kama sikosei wanamwandaa mtoto kuja kuchukua mikoba). Haya marupurupu watu wanayolalamikia, hayakutokea kwa bahati mbaya!

Wakati ule wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoambiwa hapa JF kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CDM - TL -aliomba apelekewe maswali ambayo angekuja kuyajibu (hatukupewa mrejesho), mimi nilimuuliza swali moja kuwa je akipata nafasi ya kuwa rais alikuwa na mpango gani wa kufutilia mbali UFISADI unaopitia katika hiki kitu kinaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz? Kinachofanywa na hii institution inayoitwa BUNGE katika dimbwi la ufukara wa waTz ni laana!
But how do we stop this, Jakaya was resources minister -angalia hiyo mikstaba ya madini. Leo tunampa hekalu na marupurupu for life. Did he build anything significant? The guy was so corrupt and spent his time visiting other countries. Ex presidents should be made to account on what they did! But hawser I kushitakiws maana wabunge wetu walipitisha sheria hiyo- akili ya kuku kabisa!
 
Hebu twende taratibu kisha ujipime. 2014 kabla ya Magufuli kuwa rais tulikuwa tunaimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas, wakati huo Magufuli alikuwa waziri na yeye alibariki suala la umeme wa gas. Tukakopa $1.3b sawa na 3t kujenga bomba la gas toka Mtwara, tuliambiwa kwenye umeme wa Gas tutazalisha 5,000m, na kweli bomba liko hapa Dar na uzalishaji umeanza kiwango 450mg kama sikosei, ukichanganya na umeme wa vyanzo vingine tuna umeme 1,500m+. Inakuwaje Magufuli awe rais aanze mradi mpya wa maji wa 6.5t utakaozalisha 2,115m aache wa gas utakaozalisha 5,000? Tena anatumia maji, ambapo akiwa waziri alikuwa ni mmoja ya waliotumanisha tatizo la umeme wa maji ni mabadiliko ya tabia nchi? Je angeweka 2.5t asingeweza kuzalisha 2,115m hapo kwenye gas ambapo tayari bomba liko hapa Dar, na fedha zinazobaki zikiingia kwingine? Hilo ni moja.

Tuje kwenye hilo la ndege, sina popote ninapobeza kuwa na ndege, ila ndege zilipaswa kuwa kipaombele cha mwisho dhidi ya vipaombele vingine. Ama ni bora angenunua ndege nyingi ndogo za ndani kuwezesha safari za ndani, kuliko hizo za masafa marefu wakati ushindani wa biashara hiyo kimataifa kwetu ni mdogo. Kuliko kuwekeza 1.8t kwenye ndege alizonunua, angeweza kujenga viwanda vya kimkakati kwenye maeneo yalimayo pamba, korosho, kahawa, tumbaku nk vya wangalua 50b@, kisha atoe ajira. Ama basi angejeja shule za VETA kila mkoa ymza 10b@ vijana wapate ujuzi. Kama una akili nzuri ulipaswa kujiuliza mambo hayo, na sio kusubiri kulishwa propaganda na kuanza kusifia kama kipofu.
Hilo la gas wala usizungumze, labda umesahau, tulishaambiwa tulipigwa!! Haina faida yoyote kwetu,
Na tulismbiwa mchana kweupe na hakuna mtu yeyote aliyepinga au kutaka ufafanunuzi wowote,

aliyetuambia alikuwa bungeni wakati huo na ni waziri, ushahidi gani zaidi unataka,
Yeye Ana akili na ndio aliamua ujengwe umeme wa maji.kiufupi (gas tulipigwa).

hivyo viwanda vilikuwepo mkaviua, yeye alikuwa anaanza upya kabisa, maana hatukuwa na nchi wakati huo, ndio maana alianza na umeme wa uhakika kwanza,

kwa akili yako kwa umeme ule wa majenereta ungeweza kuendesha hivyo viwanda?
Kuhusu shule za Veta, unafikiri tuna uhaba wa mafundi kiasi hicho, mbona tunao wengi tu na hawana ajira yeyote, au umeshawaandalia ajira, wengi tu tunao mtaani huku.

kuhusu ndege ndogo, wewe unafsiri vipi ndege ndogo, mbona zito, au Bombardier kwako ni ndege kubwa,

hivi unavyosema zingesubiri kwanza, ulitaka tusubiri mpaka lini mwenzetu, maana tumesubiri miaka 30 hakuna ndege, kwa hiyo neno kusubiri wenzio tulishachoka.

hata kama zidingenunuliwa leo unafikiri hiyo pesa ungeiona, zingekuwa zimeshachotwa, bora ndege zetu tunaziona.
Ooo pole sana MAGUFULI,
Watu wako hawajui wanataka nini
 
CWR2016 umetoa hoja nzuri na inayohitaji tafakuri. Mojawapo ya chanzo cha ufukara unaozungumzia na ambao ni kweli kabisa ni UFISADI (sio kwa maana ya 'kamusi' ya CCM) bali katika maana halisi ya dhana ya kleptocracy ('wizi' wa mali ya umma uliohalalishwa na walioshikilia madaraka). Kwa mfano ni mishahara na posho za waheshimiwa wabunge.

BUNGE ni kleptocracy iliyosukwa wakati wa awamu ya Mkapa. Hii ningeiita SUSTAINABLE KLEPTOCRACY ambapo wanasiasa watawala wanajihakikishia wao na familia zao zinaneemekea (chukua mfano wa Jakaya Kikwete, leo hii anapata mafao ya ustaafu wa urais, mtoto ni mbunge, mke ni mbunge,na soon hata mjukuu atakuwa mbunge; Hayati Sitta, alikuwa mbunge na mama mbunge, kama sikosei wanamwandaa mtoto kuja kuchukua mikoba). Haya marupurupu watu wanayolalamikia, hayakutokea kwa bahati mbaya!

Wakati ule wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoambiwa hapa JF kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CDM - TL -aliomba apelekewe maswali ambayo angekuja kuyajibu (hatukupewa mrejesho), mimi nilimuuliza swali moja kuwa je akipata nafasi ya kuwa rais alikuwa na mpango gani wa kufutilia mbali UFISADI unaopitia katika hiki kitu kinaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz? Kinachofanywa na hii institution inayoitwa BUNGE katika dimbwi la ufukara wa waTz ni laana!
RIP Magufuli, not sure if he died of natural causes or he was murdered na wajanja. Tanzania is so rich but the resources are for the benefit of very few families.
 
RIP Magufuli, not sure if he died of natural causes or he was murdered na wajanja. Tanzania is so rich but the resources are for the benefit of very few families.
And the poverty,higher unemployment rate increased a lot in the sessions of JK and SHS[emoji3][emoji3]
 
Hilo la gas wala usizungumze, labda umesahau, tulishaambiwa tulipigwa!! Haina faida yoyote kwetu,
Na tulismbiwa mchana kweupe na hakuna mtu yeyote aliyepinga au kutaka ufafanunuzi wowote,

aliyetuambia alikuwa bungeni wakati huo na ni waziri, ushahidi gani zaidi unataka,
Yeye Ana akili na ndio aliamua ujengwe umeme wa maji.kiufupi (gas tulipigwa).

hivyo viwanda vilikuwepo mkaviua, yeye alikuwa anaanza upya kabisa, maana hatukuwa na nchi wakati huo, ndio maana alianza na umeme wa uhakika kwanza,

kwa akili yako kwa umeme ule wa majenereta ungeweza kuendesha hivyo viwanda?
Kuhusu shule za Veta, unafikiri tuna uhaba wa mafundi kiasi hicho, mbona tunao wengi tu na hawana ajira yeyote, au umeshawaandalia ajira, wengi tu tunao mtaani huku.

kuhusu ndege ndogo, wewe unafsiri vipi ndege ndogo, mbona zito, au Bombardier kwako ni ndege kubwa,

hivi unavyosema zingesubiri kwanza, ulitaka tusubiri mpaka lini mwenzetu, maana tumesubiri miaka 30 hakuna ndege, kwa hiyo neno kusubiri wenzio tulishachoka.

hata kama zidingenunuliwa leo unafikiri hiyo pesa ungeiona, zingekuwa zimeshachotwa, bora ndege zetu tunaziona.
Ooo pole sana MAGUFULI,
Watu wako hawajui wanataka

Alisema tumepigwa, tulipigwa na nani, na ni hatua gani alichukua. Mbona kwenye madini alichukua hatua tukamuona tajiri wa Barrick, huko kwenye Gas alishindwa nini? Alianzisha mahakama ya mafisadi, mbona hakuwashitaki hao wapigaji, zaidi ya yeye kuanzisha mradi wake wa umeme wa maji ili na yeye apige. Watu waliokuwa wanahoji ndio hao alikuwa anaagiza lile kundi lake la watu wasiojulikana waweteke na kuwashambulia kwa risasi.

Ni kweli ndege unaziona, hapo ndio akili yako imeishia, na wala sio tija ya hizo ndege unazoziona. Kimsingi nilijua huna jipya zaidi ya zile propaganda ulizolishwa, lakini hujui uhalisia wowote wa mambo.
 
Hilo la gas wala usizungumze, labda umesahau, tulishaambiwa tulipigwa!! Haina faida yoyote kwetu,
Na tulismbiwa mchana kweupe na hakuna mtu yeyote aliyepinga au kutaka ufafanunuzi wowote,

aliyetuambia alikuwa bungeni wakati huo na ni waziri, ushahidi gani zaidi unataka,
Yeye Ana akili na ndio aliamua ujengwe umeme wa maji.kiufupi (gas tulipigwa).

hivyo viwanda vilikuwepo mkaviua, yeye alikuwa anaanza upya kabisa, maana hatukuwa na nchi wakati huo, ndio maana alianza na umeme wa uhakika kwanza,

kwa akili yako kwa umeme ule wa majenereta ungeweza kuendesha hivyo viwanda?
Kuhusu shule za Veta, unafikiri tuna uhaba wa mafundi kiasi hicho, mbona tunao wengi tu na hawana ajira yeyote, au umeshawaandalia ajira, wengi tu tunao mtaani huku.

kuhusu ndege ndogo, wewe unafsiri vipi ndege ndogo, mbona zito, au Bombardier kwako ni ndege kubwa,

hivi unavyosema zingesubiri kwanza, ulitaka tusubiri mpaka lini mwenzetu, maana tumesubiri miaka 30 hakuna ndege, kwa hiyo neno kusubiri wenzio tulishachoka.

hata kama zidingenunuliwa leo unafikiri hiyo pesa ungeiona, zingekuwa zimeshachotwa, bora ndege zetu tunaziona.
Ooo pole sana MAGUFULI,
Watu wako hawajui wanataka nini
Magufuli was murdered, and they made sure everyone knew he was dead. Lini uliona maiti inapelekwa huko kule na huko. Ilikuwa kutuonyesha amekufa. Maiti huheshimiwa na kuzikwa ASAP. Njoni muone he is in that box. Ni mzima, all of a sudden amekufa! They have blood in their hands, they never told us the truth in the first instance.
 
Kiongozi umesema jambo kubwa sana.

1. Badiliko la fikra.

Linapatikanaje?

Na litaongozwa na nani?

2. Ulinzi na matumizi ya faida kwa rasilimali zetu.

Mifumo ya kusimamia bila kuweka tamaa binafsi, ipo??

1. Fikra ni huweza kubadilishwa kupitia elimu

2. Tukiweza kubadilika hapo kwenye nambari 1, ina maana nambari 2 haitakuwa kikwazo
 
Viwango vya akili vya Watanzania ni vya chini sana!
sisi sio wajinga, tumeona ulichokuwa ukikitetea humu. wewe ulikuwa fan mkubwa sana wa chadema, alipoingia msukuma mwenzako ikulu hukuwahi kuona kasoro zozote juu yake, kila alichofanya ulitetea isipokuwa vichache sana ambavyo ulikosoa kinafiki. msukuma mwenzako (kama ilivyokuwa kwa JK) alifanya mengi mazuri lakini yapo pia mabaya mengi tu aliyofanya; during JK era uliona mabaya tu yake, but was opposite during msukuma's era. so we know who you are.
either, in a rare case, unaweza ukawa mkatoliki uliyepindukia; pale mkatoliki mwenzako slaa alipoondoka chadema na mkatoliki mwengine kuingia ikulu uliambatana nao! (this goes to mwanakijiji pia)

kwa hiyo we kosoa tu (constructive criticism) that's not a problem and we'll still take it, but at least some of us knows your mwelekeo!
 
Back
Top Bottom