Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!!!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere...

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa..

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.... Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?!
Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu...

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.
Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?!
Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.
Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1...

Asante Mh Rais kwa usikivu wako..
Mkuu umeguswa sana manake hilo neno "asikudanganye mtu" umelitumia sijui mara ngapi!! Hahaaaa....

Nikirudi kwenye mada yako, ni kweli nchi hii ina matatizo mengi na mengine ni sugu haswa mpaka wengine hasa yanaowasibu wameamua tu kutokulalamika tena. Wamepoteza tumaini.

Ila naamini SSH anayajua vizuri tu, cha muhimu tukubaliane mzigo wa matatizo uliopo ni mkubwa kuliko hata uwezo wa nchi. Kwahiyo tusirumie muda mwingi kumlaumu/kumlalamikia Rais. Tunapaswa sote tuyabebe matatizo ya nchi hii na kutapatia ufumbuzi.

Watanzania tuna kasumba ya kutupia viongozi mzigo halafu tayari tunajiona kama tumeshatimiza wajibu wetu.

Kila mtu ana wajibu kwake mwenyewe, familia yake na Taifa lake.
 
Kiukweli li-mfumo hili hata mimi sielewi.
Kila Rais anaonekana eti anaanza. Yani nchi ni kama TUNABAHATISHA.

Sasa je, kama walioko ndani ya mfumo ni wanufaika. Unategemea wataufumua huo MFUMO?!

AU WANASUBIRI SHIDA ZA WANACHI ZIWAPIGE HADI MATAKONI, TUSHIKANE MASHATI...!!
Hapo sasa. Tatizo ni kuwa ubovu wa mfumo ni faida ya walioko kwenye mfumo. Hawawezi kukubali kuachia matonge yaliyoko mdomoni. Juzi juzi waliokuwa hawako kwenye ulaji wakati wa Magufuli walikuwa wanasema tunahitaji katiba mpya. Sasa hivi wameshaona kuna nafasi ya kurudi kwenye mfumo na lugha imebadilika: Tusibiri kwanza!
 
Umenifanya nikumbuke vijiji fulani mkoa wa Morogoro (navihifadhi kwa majina) magari hayafiki huko na watoto wadogo wanasikia tu kuna vitu vinaitwa magari hawayajui. Pia kwenye vijiji vya delta ya mto Rufiji hali ndio hiyo. Kwenda shule na hospitali lazima uvuke mto, hamna umeme pia. Na hawa kipindi cha uchaguzi wanapelekewa masanduku ya kupigia kura.

Tuli Daslma tunaona mambo ni swafi kabisa...!!
Heri na wewe unaweza kusimulia.
Tunayoyashuhudia yanaumiza mioyo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Inasikitisha sana kuona fedha za matumizi ya kawaida kuliko zinazotengwa Kwa miradi ya maendeleo,

Halafu Bado tunawapa maskini hao hao mzigo wa mikopo kwa miradi isiyokuwa na faida za kuonekana.

Nadhani ipo haja Kwa serikali kupunguza Matumizi makubwa yasiyokuwa na tija na kuelekeza fedha kwa miradi itakayolenga kubadili maisha ya watanzania wenye hali za chini.
 
Karibu #Statesman ktk mjadala.

Tuwaulize serikali, kwa nini mfano wanashindwa kusimamia mageuzi ktk kilimo.
Je, hawaamini kitatoa ajira nyingi sana? Shida ni nini ktk nchi hii?!
 
Karibu #Statesman ktk mjadala.

Tuwaulize serikali, kwa nini mfano wanashindwa kusimamia mageuzi ktk kilimo.
Je, hawaamini kitatoa ajira nyingi sana? Shida ni nini ktk nchi hii?!
Watanzania tumebakia kuimba tu mapambio ya kauli mbiu za viongozi wao wakiendelea kurithishana nafasi zenye neema na familia zao.

Tulianza kusikia nyimbo za Kilimo Kwanza, Tanzania ya Viwanda na Sasa 50/50.

Nadhani ni Hofu tu ya watawala kwamba wakitukwamua kiuchumi watakosa wa kuwatawala woga usiokuwa na mantiki yeyote.
 
Mkuu umeguswa sana manake hilo neno "asikudanganye mtu" umelitumia sijui mara ngapi!! Hahaaaa....

Nikirudi kwenye mada yako, ni kweli nchi hii ina matatizo mengi na mengine ni sugu haswa mpaka wengine hasa yanaowasibu wameamua tu kutokulalamika tena. Wamepoteza tumaini.

Ila naamini SSH anayajua vizuri tu, cha muhimu tukubaliane mzigo wa matatizo uliopo ni mkubwa kuliko hata uwezo wa nchi. Kwahiyo tusirumie muda mwingi kumlaumu/kumlalamikia Rais. Tunapaswa sote tuyabebe matatizo ya nchi hii na kutapatia ufumbuzi.

Watanzania tuna kasumba ya kutupia viongozi mzigo halafu tayari tunajiona kama tumeshatimiza wajibu wetu.

Kila mtu ana wajibu kwake mwenyewe, familia yake na Taifa lake.
Nakuelewa vyema.
Ila hii la kila mtu kutimiza wajibu wake ni hoja ya kisiasa sana.
Wajibu mkubwa wa kwanza wa mwanachi ni kulipa Kodi.
Kuchangia gharama, n.k

Nikuulize swali, wewe ukajaze madawa hospital?

Wewe ukajenge shule ngapi?
Waoo si wameuza gesi?
Si wameuza madini?

Si wameuza korosho?

Si wametoa Ardhi yetu kwa miaka 33, 66 au 99?

Si wameuza vitalu wanyama wetu wanawindwa?

TUNAPATA NINI?

Au Ma VX V8??
 
CWR2016 umetoa hoja nzuri na inayohitaji tafakuri. Mojawapo ya chanzo cha ufukara unaozungumzia na ambao ni kweli kabisa ni UFISADI (sio kwa maana ya 'kamusi' ya CCM) bali katika maana halisi ya dhana ya kleptocracy ('wizi' wa mali ya umma uliohalalishwa na walioshikilia madaraka). Kwa mfano ni mishahara na posho za waheshimiwa wabunge. BUNGE ni kleptocracy iliyosukwa wakati wa awamu ya Mkapa. Hii ningeiita SUSTAINABLE KLEPTOCRACY ambapo wanasiasa watawala wanajihakikishia wao na familia zao zinaneemekea (chukua mfano wa Jakaya Kikwete, leo hii anapata mafao ya ustaafu wa urais, mtoto ni mbunge, mke ni mbunge,na soon hata mjukuu atakuwa mbunge; Hayati Sitta, alikuwa mbunge na mama mbunge, kama sikosei wanamwandaa mtoto kuja kuchukua mikoba). Haya marupurupu watu wanayolalamikia, hayakutokea kwa bahati mbaya!
Wakati ule wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana tulipoambiwa hapa JF kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CDM - TL -aliomba apelekewe maswali ambayo angekuja kuyajibu (hatukupewa mrejesho), mimi nilimuuliza swali moja kuwa je akipata nafasi ya kuwa rais alikuwa na mpango gani wa kufutilia mbali UFISADI unaopitia katika hiki kitu kinaitwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz? Kinachofanywa na hii institution inayoitwa BUNGE katika dimbwi la ufukara wa waTz ni laana!!!
Mkuu nakuunga mkono kwenye hili dubwasha linaitwa BUNGE!
Kwa sasa bunge ni kama kijiwe tu,halikidhi matakwa ya wananchi na mbaya zaidi linameza pesa ndefu sana lakini tunachokipata toka bungeni ni aibu tu. Idadi ya wabunge ni kubwa sana na posho wanayolipwa iko juu,lakini mijadala yao ni heri hata kutizama katuni za tom n jerry kidogo unapata chakula ya ubongo.
Kabla ya kuanza na katiba mpya,tuanze na kupunguza idadi ya wabunge na posho zao ziwe chini kama watumishi wengine.
Hebu fikiria,seating allowance kama vile walichaguliwa kwa minajili ya kusimama tu.
 
Nilishangaa, halafu anasema eti kidogo kidogo tunaenda.
Na hii ya kujenga shule moja ya Bweni ya Wasichana kila mkoa.
SERIOUS!??
Ni kama anafanya 'favour' au anatoa zawadi.
Tunawezaje kupaka rangi tatizo kubwa tena ktk 'level' ya Urais?!

Mambo mengin hata washauri wake waone aibu.

Hiyo ya mashuka 200 haikutakiwa hata kutangazwa in public.
Au alitoa pocket money yake?
 
Tumpe muda gani zaidi? Tangu March Hadi Sasa hajamaliza kuteua . Bado madc,maded wa halmashauri,,makatibu tawala. Speed yake ni ndogo sana sana. Songwe na kigoma atafika lini?
Halafu hili la kuteua mbona kama halimaliziki.?

Au ana muda mwingi sana.

Si ateue aendelee na kazi.

Kisaikolojia mfano ma DC , DAS wapo mguu ndani mguu nje, nani anauhakika?

Ateue, watu wafanye kazi!
 
Halafu hili la kuteua mbona kama halimaliziki.?

Au ana muda mwingi sana.

Si ateue aendelee na kazi.

Kisaikolojia mfano ma DC , DAS wapo mguu ndani mguu nje, nani anauhakika?

Ateue, watu wafanye kazi!
Anavyoendelea kuchelewa kuteua waliopo madarakani ambao hawana uhakika wa kubakia kwenye madaraka wanaendelea kupiga .
 
Umesema kitu kikubwa sana.
Binafsi sielewi kwa nini ukitoa hoja juu ya Mh Rais,, unaambiwa "Unateseka nini wewe SukumaGang , mara MATAGA".
Watu wafuatilie hata nyuzi zangu na koment zangu, nilimkosoa sana Hayati. Sasa iweje nongwa kumkosoa Rais wetu wa awamu ya sita?!
Mna mawazo mazuri ila mumpe muda.Hata wengine wakati wa John walipotoa mawazo mliwaita majina ya hovyo.Si wao.Ni Mungu anawaonesha ninyi kwamba hamuijui kesho yenu.Muwe wavumilivu mkisimangwa.🤣🤣🤣🤣
 
Hotuba yake siku ya kuapishwa kwake ilinipa matumaini makubwa sana kwake lakini baada ya hii miezi mitatu hitimisho langu ni mtu hopeless tu na ndani ya Serikali bado kuna mvutano mkubwa na wale ambao hawakutaka huyo Mama awe Rais na wale wanaomkubali. Hivyo mimi sitegemei kuona mabadiliko yoyote makubwa kutoka kwa huyo mama kati ya sasa na 2025 na hastahili kuendelea kuwepo Ikulu baada ya 2025, labda atabadilika maana miezi mitatu ni kipindi kifupi mno. Nilisema hapa dhalimu ni bomu tangu 2015 na sikukosea hivyo hitimisho langu huyo mama ni bomu JINGINE.

Back
Top Bottom