Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Nilishangaa, halafu anasema eti kidogo kidogo tunaenda.
Na hii ya kujenga shule moja ya Bweni ya Wasichana kila mkoa.
SERIOUS!??
Ni kama anafanya 'favour' au anatoa zawadi.
Tunawezaje kupaka rangi tatizo kubwa tena ktk 'level' ya Urais?!

Mambo mengin hata washauri wake waone aibu.

Hiyo ya mashuka 200 haikutakiwa hata kutangazwa in public.
Suala sio kujenga shule zingine bali ningekuwa mimi ningeanza na kuboresha hizi zilizopo. Shule hizi zilizopo nyingi hazina waalimu wa kutosha, hazina madawati, elimu inayotolewa haina msaada kwa watoto wetu, waalimu waliopo wamekata tamaa.
Rais wetu aachane na kujenga shule zingine tuboreshe hizi zilizopo kitaaluma, na mazingira ndipo tuanze kuongeza shule zingine.
 
Kuna watu ni matajiri wa kukosoa, kulaumu ila masikini wa kutupwa wa utendaji wa manufaa kwa mama Tanzania.

Safari ya maendeleo bado ni ndefu sana hata hivyo siyo ndefu kama ilivyokuwa miaka 10,20, 30...... iliyopita.

Hatua za maendeleo zinapigwa kila awamu. MUNGU na atutangulie mpaka pale mwisho wa binadamu utakapofika.
 
Binafsi hii nchi aliiweza magufuli peke ake, ili maendeleo yawepo uvunjifu wa mfumo wa kidemokrasia lazima uwepo. hivi viatu alivyovaa mama etu mpendwa ni vigumu na vinahitaji utulivu wa mwili na akili, kwa mwanamke ambaye ameumbwa kuongozwa hawezi kutufikisha popote. unajua hayati hakuwa akimsikiliza kila mtu alifanya vile akili yake ilivyomtuma maana alijua miluzi mingi humpoteza mbwa pia alijua kuwa nchi haijengwi kwa siasa bali kwa jasho na damu na ndo maana alikuwa tayari kupoteza damu yake ili kuleta maendeleo yenye tija, tuache kuwa wabinafsi richa ya kuwa wananchi wengi ni fukara ila hayati alipambana kuijenga nchi kuwaacha wananchi wanaumia ili vizazi vyao vije vifurahie matunda ya jasho za baba zao, ila watanzania wengi hatupo tayari kujitoa kwaajili ya future ya watoto wetu, kila mmoja ana roho ya ubinafsi anaona ni bora aje ateseke mtoto wake ila yeye ale matunda ya nchi. na ndo maana hatukusita kumpinga. Ok turudi kwenye mada, katika kitu cha umuhimu ambacho raisi anatakiwa kukifanya ni kuhakikisha anabadilisha mfumo wa elimu na kuongeza idadi ya technical schools and colleges ili kutengeneza watu wanaoweza kujiajili, pia angewekeza katika kuwapa sapoti local inovators ili kuikuza teknolojia yetu maana hili litapunguza cost burden kwenye foreign importation, huenda maraisi waliopita wangewasapoti local inovators sasa ivi tungekuwa tunatengeneza magari yetu wenyewe, viwanda vingekua, un employment rate ingepungua, kilimo kingebadirika na watu wangevuna mpaka wasingekuwa na mahali pa kuvipeleka vyakula, ila kwa sababu mawazo yao yamefungwa ndo maana akitokea mtu amegundua kitu anasainiwa na mataifa ya kibeberu ili wakawanufaishe wazungu waje watunyonye wakati sisi tunamuona mpuuzi eti hakina quality kitahatarisha maisha ya watu ivii mmesahau kuwa hata britain iliyosumbua kuwa na viwanda vikubwa karne ya 16 walianza na mfumo mdogo (stem engine)?. nchi yetu inahitaji raisi mwenye fikra za kujilisha wenyewe na sio kuombaomba maana hata marekani inapasua vichwa kwa kuwa ba uchumi mkubwa duniani kwa sababu ilipata maraisi wenye akili, wenye kushindana kuiondoa nchi kutoka kwenye umasikini na sio kushindana kwa kiki, tukiendelea kukaza vichwa tutabaki nyumanyuma kama koti la babu msizilo, wazungu wataendelea kututafuna vichwa wakati sisi tukiendelea kuwachekea.
yangu ni hayo tu wakuu.[emoji120][emoji120]

Kwani Magufuli alikuwa ana akili au alikithiri kwa kutumia mabavu? Ndani ya miaka 5+ aliyokaa madarakani deni la taifa limepaa kwa 30t+. Ukiambiwa uonyeshe hiyo miradi ya 30t wala hutoweza. Usichanganye akili na kiburi cha madaraka.
 
mkuu hoja yangu inahitaji utulivu wa mwili na akili ili kuielewa kwa maana kiburi cha madaraka ndo kilimfanya Hitler kuipa status Germany akaikwamua kutoka kwenye umasikini. siku zote raisi mpole haifanyi nchi kuendelea badala yake ni kulimbikiza madeni na kukithirisha unyonyaji wa watu weupe maana hata wakisema mweshimiwaa tukujengee bandari harafu tuchimbe madini kwa miaka 100 atakubali huku anachekacheka. nchi ngumu kama hii inahitaji raisi mwenye kiburi cha madaraka. naomba kabla hujajibu hii hoja kaa ufikirie kwa kina then back to reply[emoji120][emoji120]
 
Hapaka, mpaka Juni 2015 deni la taifa lilikuwa 38.2 Trilioni. Magufuli kaondoka deni likiwa 57 Trilioni. Ni ongezeko la 19 Trilioni.

Kambuka juzi tu World Bank wamekubali kitukopesha 2.3 Trilioni wakati mama ana miezi 3 tu. Kama tunaangalia ukuaji wa deni, tusibiri miaka 5 tuone.
 
"Ask not what your country can do for you-Ask what you can do for your country".
Hii hai aplly kwa Tanzania na watanzania.??
 
Wengine tuliyasema haya haya wakati wenye nchi yao wananunua madege lukuki kwa cash......tuliambiwa sio wazalendo! Baadae tukaambiwa tupo uchumi wa kati.....tulipouliza mbona wananchi wengi bado ni masikini....tukaambiwa sio wazalendo!
 
Nukuu ya Hayati Magufuli;
"Nchi yetu ni Tajiri sana tena sana......."
ila wanchi wake ndio masikini, kwa nini?
Hayati Magufuli alishatuonyesha njia ya jinsi ya kulinda rasilimali za nchi yetu, kubana matumizi ya serikali n.k.
ili kufikia lengo la kuondoa umasikini ni lazima viongozi wetu wote waliopewa dhamana waamue kwa dhati kupambana na kuzitumia rasilimali zetu kwa manufaa ya watanzania.

viongozi hawapaswi kuhadaika na starehe walizo nazo, vyeo, mishahara, nyumba, ulinzi n.k, halafu wakasahau wananchi wao kuwa wapo ktk dimbwi la ufukara.
 
mkuu hoja yangu inahitaji utulivu wa mwili na akili ili kuielewa kwa maana kiburi cha madaraka ndo kilimfanya Hitler kuipa status Germany akaikwamua kutoka kwenye umasikini. siku zote raisi mpole haifanyi nchi kuendelea badala yake ni kulimbikiza madeni na kukithirisha unyonyaji wa watu weupe maana hata wakisema mweshimiwaa tukujengee bandari harafu tuchimbe madini kwa miaka 100 atakubali huku anachekacheka. nchi ngumu kama hii inahitaji raisi mwenye kiburi cha madaraka. naomba kabla hujajibu hii hoja kaa ufikirie kwa kina then back to reply[emoji120][emoji120]

Inaonyesha hujui hata unaongea nini, kama kiburi cha madaraka na ukatili ndio unaleta maendeleo, basi Afrika ndio ingekuwa na maendeleo sana, maana viongozi wenye viburi vya madaraka ni kibao. Nimekuambia kipindi cha miaka mitano ya Magufuli deni la taifa limepanda kwa 30t, sasa nitajie miradi iliyofanya deni kuwa kubwa kiasi hicho.
 
siku moyo wako ukikubali kuupokea uzalendo rudi hapa tuje tuongee lugha inayofanana.[emoji120][emoji120]
 
Hapaka, mpaka Juni 2015 deni la taifa lilikuwa 38.2 Trilioni. Magufuli kaondoka deni likiwa 57 Trilioni. Ni ongezeko la 19 Trilioni.

Kambuka juzi tu World Bank wamekubali kitukopesha 2.3 Trilioni wakati mama ana miezi 3 tu. Kama tunaangalia ukuaji wa deni, tusibiri miaka 5 tuone.

Mkuu sitaki kupinga ulichoeleza hapa. Hilo deni la taifa ukitaka kusikia raha sikiliza waziri Mkuu akilisema atataja figure yake, waziri wa fedha atataja figure yake na rais pia atataja figure yake. Ngoja tubaki kwenye hiyo figure yako ya 57t. Ukiangalia vizuri, hilo deni 1/3 ni kipindi cha miaka mitano tu, linganisha na miaka 54 ya marais wengine wote wanne waliopita. Je unaweza kunitajia miradi iliyopelekea deni kuwa kubwa hivyo, wakati serikali ya Magufuli ilikuwa inajinasibu kukusanya 1.3t@month?
 
Inaonyesha hujui hata unaongea nini, kama kiburi cha madaraka na ukatili ndio unaleta maendeleo, basi Afrika ndio ingekuwa na maendeleo sana, maana viongozi wenye viburi vya madaraka ni kibao. Nimekuambia kipindi cha miaka mitano ya Magufuli deni la taifa limepanda kwa 30t, sasa nitajie miradi iliyofanya deni kuwa kubwa kiasi hicho.
harafu mimi sikuzungumzia ukatili. go and skim the thread again.
 
siku moyo wako ukikubali kuupokea uzalendo rudi hapa tuje tuongee lugha inayofanana.[emoji120][emoji120]

Sasa hivi ni vigumu kutofautisha uzalendo na ujinga. Sema hivi, siku nikikubali kuwa mjinga kama utakavyo, nije unilishe Matango pori. Kimsingi nilijua huna jipya zaidi ya kuleta mawazo ya fuata mkumbo.
 
harafu mimi sikuzungumzia ukatili. go and skim the thread again.

Kwenye post zako ulimtaja Hitler kama mfano wa aina ya kiongozi anayeweza kuleta maendeleo. Ama hukumbuki mifano yako? Sasa unapomtaja Hitler unatengaje kauli zako na kuabudu ukatili?
 
Kwenye post zako ulimtaja Hitler kama mfano wa aina ya kiongozi anayeweza kuleta maendeleo. Ama hukumbuki mifano yako? Sasa unapomtaja Hitler unatengaje kauli zako na kuabudu ukatili?
alikuwa mkatili kwa nataifa ya nje. ila kwa nchi yake alikuwa mzalendo the same kwa hayati, aliwatimua wapiga bingo mjini ili aijenge nchi watu wake waje wafaidi.
 
Ukiutaja umasikini wa watanzania,itaonekana unawatetea masikini ,matajiri hawapendi hiyo , sababu serikali ya awamu ya tano iliwapenda Sana masikini..na kuwatengezea Njia
 
Back
Top Bottom