Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Mkuu umeguswa sana manake hilo neno "asikudanganye mtu" umelitumia sijui mara ngapi!! Hahaaaa....

Nikirudi kwenye mada yako, ni kweli nchi hii ina matatizo mengi na mengine ni sugu haswa mpaka wengine hasa yanaowasibu wameamua tu kutokulalamika tena. Wamepoteza tumaini.

Ila naamini SSH anayajua vizuri tu, cha muhimu tukubaliane mzigo wa matatizo uliopo ni mkubwa kuliko hata uwezo wa nchi. Kwahiyo tusirumie muda mwingi kumlaumu/kumlalamikia Rais. Tunapaswa sote tuyabebe matatizo ya nchi hii na kutapatia ufumbuzi.

Watanzania tuna kasumba ya kutupia viongozi mzigo halafu tayari tunajiona kama tumeshatimiza wajibu wetu.

Kila mtu ana wajibu kwake mwenyewe, familia yake na Taifa lake.
 
Hapo sasa. Tatizo ni kuwa ubovu wa mfumo ni faida ya walioko kwenye mfumo. Hawawezi kukubali kuachia matonge yaliyoko mdomoni. Juzi juzi waliokuwa hawako kwenye ulaji wakati wa Magufuli walikuwa wanasema tunahitaji katiba mpya. Sasa hivi wameshaona kuna nafasi ya kurudi kwenye mfumo na lugha imebadilika: Tusibiri kwanza!
 
Heri na wewe unaweza kusimulia.
Tunayoyashuhudia yanaumiza mioyo.
 
Reactions: BAK
Inasikitisha sana kuona fedha za matumizi ya kawaida kuliko zinazotengwa Kwa miradi ya maendeleo,

Halafu Bado tunawapa maskini hao hao mzigo wa mikopo kwa miradi isiyokuwa na faida za kuonekana.

Nadhani ipo haja Kwa serikali kupunguza Matumizi makubwa yasiyokuwa na tija na kuelekeza fedha kwa miradi itakayolenga kubadili maisha ya watanzania wenye hali za chini.
 
Karibu #Statesman ktk mjadala.

Tuwaulize serikali, kwa nini mfano wanashindwa kusimamia mageuzi ktk kilimo.
Je, hawaamini kitatoa ajira nyingi sana? Shida ni nini ktk nchi hii?!
 
Karibu #Statesman ktk mjadala.

Tuwaulize serikali, kwa nini mfano wanashindwa kusimamia mageuzi ktk kilimo.
Je, hawaamini kitatoa ajira nyingi sana? Shida ni nini ktk nchi hii?!
Watanzania tumebakia kuimba tu mapambio ya kauli mbiu za viongozi wao wakiendelea kurithishana nafasi zenye neema na familia zao.

Tulianza kusikia nyimbo za Kilimo Kwanza, Tanzania ya Viwanda na Sasa 50/50.

Nadhani ni Hofu tu ya watawala kwamba wakitukwamua kiuchumi watakosa wa kuwatawala woga usiokuwa na mantiki yeyote.
 
Nakuelewa vyema.
Ila hii la kila mtu kutimiza wajibu wake ni hoja ya kisiasa sana.
Wajibu mkubwa wa kwanza wa mwanachi ni kulipa Kodi.
Kuchangia gharama, n.k

Nikuulize swali, wewe ukajaze madawa hospital?

Wewe ukajenge shule ngapi?
Waoo si wameuza gesi?
Si wameuza madini?

Si wameuza korosho?

Si wametoa Ardhi yetu kwa miaka 33, 66 au 99?

Si wameuza vitalu wanyama wetu wanawindwa?

TUNAPATA NINI?

Au Ma VX V8??
 
Mkuu nakuunga mkono kwenye hili dubwasha linaitwa BUNGE!
Kwa sasa bunge ni kama kijiwe tu,halikidhi matakwa ya wananchi na mbaya zaidi linameza pesa ndefu sana lakini tunachokipata toka bungeni ni aibu tu. Idadi ya wabunge ni kubwa sana na posho wanayolipwa iko juu,lakini mijadala yao ni heri hata kutizama katuni za tom n jerry kidogo unapata chakula ya ubongo.
Kabla ya kuanza na katiba mpya,tuanze na kupunguza idadi ya wabunge na posho zao ziwe chini kama watumishi wengine.
Hebu fikiria,seating allowance kama vile walichaguliwa kwa minajili ya kusimama tu.
 
Au alitoa pocket money yake?
 
Tumpe muda gani zaidi? Tangu March Hadi Sasa hajamaliza kuteua . Bado madc,maded wa halmashauri,,makatibu tawala. Speed yake ni ndogo sana sana. Songwe na kigoma atafika lini?
Halafu hili la kuteua mbona kama halimaliziki.?

Au ana muda mwingi sana.

Si ateue aendelee na kazi.

Kisaikolojia mfano ma DC , DAS wapo mguu ndani mguu nje, nani anauhakika?

Ateue, watu wafanye kazi!
 
Halafu hili la kuteua mbona kama halimaliziki.?

Au ana muda mwingi sana.

Si ateue aendelee na kazi.

Kisaikolojia mfano ma DC , DAS wapo mguu ndani mguu nje, nani anauhakika?

Ateue, watu wafanye kazi!
Anavyoendelea kuchelewa kuteua waliopo madarakani ambao hawana uhakika wa kubakia kwenye madaraka wanaendelea kupiga .
 
Mna mawazo mazuri ila mumpe muda.Hata wengine wakati wa John walipotoa mawazo mliwaita majina ya hovyo.Si wao.Ni Mungu anawaonesha ninyi kwamba hamuijui kesho yenu.Muwe wavumilivu mkisimangwa.🀣🀣🀣🀣
 
Hotuba yake siku ya kuapishwa kwake ilinipa matumaini makubwa sana kwake lakini baada ya hii miezi mitatu hitimisho langu ni mtu hopeless tu na ndani ya Serikali bado kuna mvutano mkubwa na wale ambao hawakutaka huyo Mama awe Rais na wale wanaomkubali. Hivyo mimi sitegemei kuona mabadiliko yoyote makubwa kutoka kwa huyo mama kati ya sasa na 2025 na hastahili kuendelea kuwepo Ikulu baada ya 2025, labda atabadilika maana miezi mitatu ni kipindi kifupi mno. Nilisema hapa dhalimu ni bomu tangu 2015 na sikukosea hivyo hitimisho langu huyo mama ni bomu JINGINE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…