Nipende kumuomba CDF amshauri Rais asijenge Bandari ya Bagamoyo kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuliua Taifa Kabisa.
Nimemuomba CDF kwani yeye ndiye mkuu wa majeshi ya Ulinzi, na ulinzi ni pamoja na kuangalia uhai wa Taifa, sio kwa mtutu wa Bunduki tu na mizinga bali hata kwa ushauri wenye lengo la kuliponya Taifa.
Ikumbukwe kwamba Bandari ya Dar es Salaam, inahudumia zaidi ya asilimia tisini ya biashara za kimataifa kwa taifa letu.
Bandari hiyo hiyo ya Dar inahudumia nchi nyingine sita ambazo zimelizunguka taifa letu ikiwa ni pamoja na Rwanda, Burundi, DRC, Malawi, Zambia na Uganda.
China ni moja wapo ya Nchi zilizoweka nia ya kujenga bandari ya kisasa pale bagamoyo.
Bandari hii itakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa na itakuwa na vifaa vya kisasa kabisa hivyo kuifanya Bandari hii kuwa ya kipekee katika ukanda huu.
Nchi yetu inategemea sana mapato yatokanayo na bidhaa zinazopitia katika bandari yetu.
Kwa mwaka 2018 pekee, China na Tanzania zilifanya biashara ya kiasi cha dola za kimarekani 1.8 Bilioni sawa na Shilingi za kitanzania Trilioni Mbili.
China hiyo hiyo inafanya bishara ya Mabilioni ya Dola kwa nchi zinazozunguka Tanzania na kuitegemea Bandari yetu.
Inasemekana kwamba China watatoa fedha za mkopo ili kujenga bandari hiyo kiasi cha Dola Bilioni 10 za Kimarekani na ili kurejesha mkopo huo Bandari hiyo itakuwa chini ya uangalizi wao kwa miaka 100.
Kama hilo likitokea inamaana kwamba asilimia kubwa ya mapato yatayopatikana na Bandari hiyo yatakwenda kwao ili kulipa deni.
Kwakua China ni mdau mkubwa wa biashara na Tanzania, Kila bidhaa itayoagizwa toka china kuja Tanzania lazima itapitia Bagamoyo.
Automatically ile Biashara ya Dola Bilioni 1.8 inahamia Bagamoyo toka Bandari ya Dar. Na mapato toka nchi za DRC, Zambia , Malawi, Uganda, Burundi na Rwanda.
sitaki kuamini kwamba China atakua mwaminifu sana katika kuweka mapato ya Bandari ya Bagamoyo na kwakua historia ni shahidi tumekuwa na watu ambao sio waaminifu wanaoshirikiana na wageni katika kulitia hasara Taifa, hivyo hakuna namna tutaubiwa tu.
Kwakua bandari ya Dar itakuwa ndogo, yenye vifaa dhaifu na vya zamani hakuna atayepeleka mizigo pale, wote watahamia Bagamoyo.
Na kwakua hatutakua tunaingiza mapato, hivyo hatutaweza kulipa deni na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa wakati, jambo litakalowafanya wachina waextend muda wa kuendelea kuishikilia bandari ili walipe deni lao, jambo hili litaendelea milele.
Hivyo tutakuwa tumepoteza bandari na mapato na bado tunadaiwa.
Mkuu, CDF, Nakuomba sana wewe pamoja na makamanda wengine, mumshauri vyema Rais ili bandari hii isijengwe kwani ni hatari kwa uhai wa Taifa.
Ni hayo tu.
Mkuu 'stroke', naona umerudi kule kwa ID yako iliyozoeleka.
Ile ya 'Statesman' nayo imezoeleka.
Sasa kuhusu mada yako hii naona huitendei haki heshima unayotambulika nayo siku hizi za karibuni.
Nasema hivyo, kwa sababu suala hili la hii bandari sasa siyo geni tena. Pamoja na upotoshaji mwingi unaohusiana na hii bandari, lakini mtu mwenye kutaka kuelewa anaweza kuchambua taarifa zote zinazopatikana sasa na kujua usahihi wake.
Tuchukulie kwanza jinsi ulivyowasilisha mada yako kwa kichwa cha mada ulichokitumia.
Umeandika:
Rais Samia usijenge bandari ya Bagamoyo...".
Lakini taarifa uliyowasilisha chini ya kichwa cha habari hiyo haihusiani na kichwa cha habari hicho. Unazungumzia Bandari ya wachina.
Kwani Samia ni lazima awatumie hao wachina kuijenga hiyo bandari?
Umeeleza vizuri sana umhimu wa hiyo bandari
Bandari hii itakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa na itakuwa na vifaa vya kisasa kabisa hivyo kuifanya Bandari hii kuwa ya kipekee katika ukanda huu.
, kama ionyeshavyo hapa chini.
Nitakubaliana nawe kama ungemsihi asijenge hiyo bandari
kwa masharti tunayosikia wachina wanayataka hapo nitakuelewa; lakini siyo lazima iwe hivyo.
Hiyo bandari tunaweza kujenga wenyewe, au tukakubaliana mkataba tofauti na huo unaosemwa kuwa upo.
Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwa Tanzania ya leo na siku zijazo, hili ni jambo lililo wazi. La muhimu, ni masharti tu ya ujenzi wa bandari hiyo, ambayo ni lazima yawe kwa manufaa ya Tanzania.
Kwa hiyo, badala ya kumsihi asijenge, mimi napendekeza umhimize bandari ijengwe kwa masharti ya kuinufaisha Tanzania.
Jambo jingine ambalo ingefaa ulizingatie na kuachana na mikanganyiko mingi inayojitokeza kuhusu mradi huu ni umhimu wa kutenganisha ujenzi wa bandari na ujenzi wa eneo la viwanda na biashara (Special Economic Zone).
Bandari pekee hajengwi kwa hiyo bilioni $10 zinazotajwa. Mi nadhani, maana nzima ya kuunganisha miradi hii ndiko kunakopitishia upigaji mkubwa, pamoja na kuwafaidisha wachina na wawekezaji wengine.
Kwa mfano; hivi haiwezekani bandari ikajengwa kwa kujitegemea yenyewe bila ya kuunganishwa na huo ukanda wa kibiashara?
Tukisema sisi Tanzania tunajenga bandari, wawekezaji watakaotaka waje kuwekeza kwenye huo ukanda, kuna tatizo gani hapo?