Rais Samia usikubali kunasa kwenye mtego wa TFF

Rais Samia usikubali kunasa kwenye mtego wa TFF

Hana haja na kura za wanayanga kwa sababu hategemei kura za wananchi, aliowateua kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi watampa idadi yoyote ya kura kadiri atakavyowaelekeza.
Ikiwa huko kwenye hao wajumbe hakuna Wana Yanga
 
Hii mechi ya simba na yanga imetumika politically trust me.

Imeahirishwa halafu hiyo ya pili mgeni rasmi ni rais???

Mitanzania imeshupaza shingo kwenye mpira aseeeeee!!!

Nyie watu wa mipira mnatufelisha sana.
 
Anavyopenda mialiko, anaanzaje kukataa huo mualiko.

Hata wewe ukiwa na shughuli yako ya jando na ukajuana na watu wawili watatu wenye influence, anakuja.
 
Ligi ya bongo ni ya kihuni na upangaji matokeo. Hasa Yanga ndo wameharibu ligi na genge lao la wanasiasa.
 
Yanga wana kosa gani?
Kuwafanyia ghasia msafara wa simba uwanjani na Kuzuia simba wasifanye mazoezi ambayo ni haki ya simba kikanuni.
Ushahidi wa video za vurugu hizo wote umerekodiwa hakuna kichaka cha yanga kujinasua kwenye ghasia hii.
Hao makomandoo wametumwa na yanga kulinda uwanja kabla ya mechi.
 
Kuwafanyia ghasia msafara wa simba uwanjani na Kuzuia simba wasifanye mazoezi ambayo ni haki ya simba kikanuni.
Ushahidi wa video za vurugu hizo wote umerekodiwa hakuna kichaka cha yanga kujinasua kwenye ghasia hii.
Hao makomandoo wametumwa na yanga kulinda uwanja kabla ya mechi.
Hivi unajua askari wenye mafunzo ya ukomandoo hapa Tanzania wapo wangapi?
Yanga inamiliki vip Askari adimu wenye mazuri magumu kimedani ndani ya Tanzania?
Hivi unaamini Kuna raia wa kuzuia msafara wa Simba uliosindikizwa na police na wao kukubali kurudi nyuma.
 
Hizi ndio ng’ombe CHADEMA inazitafutia Katiba mpya!!! Inasikitisha sana
 
Kaka hii mechi watu wakitaka ichezwe wala hawana shida na rais wa nchi. Simu itapigwa pale Chalinze kwa rais mstaafu, yule Mzee ndo atatoa amri kwa rais wako wa timu apeleke timu uwanjan.
 
Rais Samia wewe ni Rais wetu site.
Mara ya kwanza ulitukwaza wanayanga ulivomaliza suala la Feitoto katika kutoa maagizo.
Na ukijua maagizo yako kama Rais hakuna raia wa nchi hii anaweza kuyapinga, Kwa heshima yako wanayanga tulikubali kulimaliza suala hili mezani japo tulishinda kwenye sheria

TFF na bodi ya ligi baada ya kuharibu na kushindwa kusimamia kanuni, Sasa kimbilio ni wewe Rais Samia kukutumia kubariki uvunjifu wa kanuni ati usuluhishe na mambo yaishie kwenye meza

TFF wamepanga kukualika kuwa mgeni rasmi wa mechi itakayopangwa upya, huku wakijua wakikutumia ww viongozi wa Yanga watakosa nguvu ya kukataa na kutetea haki ya Yanga,
Yanga hatutaki hili litokee

Rais Samia tunakuomba acha masuala ya football yaendeshwe Kwa kanuni sio kukutumia Rais kiongozi wa siasa kuingilia football

Simba aadhibiwe Kwa kanuni zilizo wazi, sio kutumia Rais wa serikali kuikandamiza Yanga

Rais akijiingiza kwenye hili suala sio sawa na oktoba atatugawa wapiga kura wake
Ni heri asionyeshe upande wowote, kanuni zisimame
Vyombo vya usuluhushi wa michezo vitumike na timu zipate haki huko CAS
Kabisa mkuu
Mama kama mkuu wa nchi tunamwamini, akae mbali na hili, hawa wahuni wa TFF na Simba wanaweza kumtumia kufunika upumbavu wao walioutengeneza🚮
 
Kaka hii mechi watu wakitaka ichezwe wala hawana shida na rais wa nchi. Simu itapigwa pale Chalinze kwa rais mstaafu, yule Mzee ndo atatoa amri kwa rais wako wa timu apeleke timu uwanjan.
Hili pia linawezekana
 
Yanga wahujumu vip Simba wasifanye mazoezi kwenye uwanja unaomilikiwa na kulindwa na Serikali?
Yaani watu wa Yanga wazuie msafara wa Simba uliosindikizwa na police?
Simba kwanini hawaku report hii jinai police ili wawakamate hao unaosema ni Yanga
Nimeandika, nimefuta😞
 
Simba aadhibiwe Kwa kanuni zilizo wazi, sio kutumia Rais wa serikali kuikandamiza Yanga
Hivi kuna watu wanaosubiri Simba kuadhibiwa? Iadhibiwe kwa mechi ambayo ilikuwa imeshaahirishwa? Kama uamuzi wa TFF wa kuahirisha mechi ungefanyika baada ya saa 1:15 jioni, Simba ingeweza kuadhibiwa. Lakini kwa kuwa TFF iliahirisha mechi masaa kadhaa kabla ya saa 1:15 muda wa mechi, basi hapo Simba yupo salama maana pengine ingeibuka uwanjani kama sio tangazo la TFF
 
Back
Top Bottom