Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Exactly 💯
 
Kama hujui Hili kundi Lina kura zaidi ya asilimia 60 anzia Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Tabora , Dodoma, Shinyanga,Katavi, kigoma, Morogoro, Kagera unafikili hizo kura ni Chache?
 
Dkt Magufuli aliweza kuongoza vizuri bila kutegemea makundi. Hao wapinzani waliishiwa kabisa sera kwa sababu Dkt Magufuli alikuwa upande wa wananchi. Mama alichokosea kabisa kwanza ni kuafiki kwake bila kukemea Dkt Magufuli kutukanwa (Dkt Magufuli aliwa kukemea na kupiga marufuku kumtukana au kumkejeli Dkt JK). Lakini Mama akaenda mpaka kupiga picha na Mange mtu ambaye system inamchukulia ni msaliti maana hakuwa na jema kwa nchi. Pia Mama kakubali kuingizwa mkenge na wahuni wa kuwatungia jina la SUKUMA gang wale wote wanaoamini ktk uzalendo kwa nchi hii kitu ambacho alipaswa akemee haraka sana hizo kejeli. Alikubali watu wamdhihaki Dkt Magufuli kwa kumuita eti mwendazake etc. labda kama ilikuwa ni mfumo ili kupembua, ila ni muhimu sana tena sana yeye kutambua yeye na Dkt Magufuli ni kitu kimoja, na wananchi walikuwa wanamkubali sana Dkt Magufuli. Yaani ni kama Dkt JK 2005, yaani wananchi walipiga kuta kwa Dkt JK tu. Ndiyo maana Mama anapaswa ausome mchezo mapema maana wahuni wamemtengenezea matukio mabaya mabaya ili aonekane hafai (mfano lile la prof mkenda, machinga, kuchoma masoko, kutaka kulazimisha mgao wa umeme, kulazimisha mgao wa maji, chanjo ya korona na kutaka kulazimisha lockdown). Kikubwa tuungane kumuombea Mama aweze kuendelea na kushinda 2025.
 
Mama atakuwa anafanya kikao labda na waheshimiwa akina Makamba ambao wanachuki binafsi na Dkt Magufuli. Kwa ufupi hilo neno la sukuma gang ni baya sana tena Mama anapaswa apige marufuku lisitumike kwa sababu sukuma gang ni wafuasi wa Dkt Magufuli ambao ni TISS wote, Wanajeshi wote hata yeye Mama ni sukuma gang, ina maana wanapomuambia awaondoe ina maana hata yeye hafai. Yaani utaona tu Makamba alivyoingia na kusema eti TANESCO ilikuwa imechafuka, ndiyo Kalemani alikuwa mkuda maana hata simu za watu alikuwa hapokei, yaani alikuwa anajifanya mbabe kwa kulazimisha vitu vya ajabu ila kuna vitu alifanya vizuri si kwa kiwango cha kudhalilishwa.
 
Kama hujui Hili kundi Lina kura zaidi ya asilimia 60 anzia Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Tabora , Dodoma, Shinyanga,Katavi, kigoma, Morogoro, Kagera unafikili hizo kura ni Chache?
Unajua hawa akina Makamba hawajui walichokianzisha ni kibaya sana. Wasukuma uzuri hawana ukabila ila ukiwazingua wanakuzingua.
 
Suala la ujenzi wa Bagamoyo lenye utata na joto la kisiasa nalo limechangia mno kupunguza umaarufu na kumrudisha Makamba na upunguzaji wa kasi ya miradi km Bwawa la Rufiji nayo inapaswa kuendelezwa kwa nguvu kwa maslahi ya taifa kwa vile ni CCM ile ile ndiyo iliyobariki. Political calculations zinakosekana kwa sasa. Hakuna kitu kibaya kupindua mambo yaliyoanzishwa na marehemu kwa watanzania kimtizamo.
 
Kazi ya kumuombea Hangaya nani afanye?
Huyu anaemdhihaki Magufuli au Hangaya mwingine unamaanisha?
 
Kifo chake kimegubikwa na utata ikiwa wasaidizi wake walijaribu kukificha ficha toka hatua za awali za yeye kupelekwa hosipitali na ikiwa mara ya mwisho alionekana bandarini akiwa buheri wa afya!
 
Umesema ukweli kabisa mkuu. Wabunge wengi walioko mjengoni walipata mteremko ndani ya chama, na kwa wananchi kwa sababu ya Magufuli (rip), hata wao wenyewe wanalijua hilo. Ule upepo wa JPM ulikuwa unavuma kivingine kabisa huko mitaani. Kwa hiyo kumshauri rais Ssh asifanye kazi na watu wa JPM ni kumchimbia kaburi.
Watu wengi huku mtaani wanamnanga kwa sababu wanamwona amejitenga sana na mtangulizi wake, ambaye yeye alikuwa makamu wake. Rais Samia anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu sana na watu aliochaguliwa nao, na kujikita zaidi kwenye kutekeleza ilani yao ya uchaguzi.
 
Amefanya vizuri.Bila ya kulalamika tusingejua kuwa ufisadi mkubwa ulianzia kwenye awamu ya tano ya Bwana Chato😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Hapo kuhusu wapinzni na hasa Mbowe amechemka sana.
Ila wapinzani wa ndani ya chama chake anawanyoosha.
 
watu hatar kwa mama ni sukuma gang. alitakiwa awafagie wote. maana bado hawaamin kama yule Mungu alishakufa. na hawako tayar kuona maono ya mama. wanataka mama aende na mfumo wao.
 
Sehemu kubwa ya matatizo amejisababishia yeye mwenyewe kwa kutokuwa na msimamo unaojulikana, na badala yake akawa anayumbayumba tu kama bendera na upepo.

Alipoanza, akawa anajitambulisha yeye na mtangulizi wake ni kitu kimoja kwa maneno, huko vitendo vikionyesha tofauti. Hii ilionyesha alitamani kurekebisha yale aliyoona hayafai katika yale yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake. Hili lilipelekea baadhi ya watu waanze kumtazama kwa karibu zaidi na kuwa na matumaini juu yake.

Wakati hajatulia vizuri ili atekeleze hayo aliyotaka kurekebisha, kama kufuta mashtaka kwa watu ambayo kesi zake hazikueleweka; mara ghafla kisharukia kwenye yale yale ambayo watu walidhani yanamchukiza. Mbowe kawekwa gerezanikihuni kihuni, pengine kuliko hata ilivyokuwa ikifanyika wakati wa dikteta Magufuli.

Watu wakawa wamechanganyikiwa na hawajui Samia anasimamia wapi.

Kuna mambo mengine yaliyoambatana na safari yake ya Kenya yaliyofanya watu wengine kumtazama kwa jicho la wasiwasi kutokana na aliyokuwa akitamka wakati wa ziara hiyo. Kiongozi mgeni, na hasa anayepokea uongozi ambao hakujinadi yeye mwenyewe kwa wananchi hupashwa kuwa na subira nayo. Huwezi kuingia mara moja na kutaka ubadili kila kitu kufuatana na matakwa yako.

Samia kajitambulisha yeye ni rais anayejali maslahi ya walanguzi/madalali na wapigaji kuliko maslahi ya wananchi wa kawaida. Hili nalo limestua watu na kuanza kuwa na wasiwasi juu yake.

Rais Samia Suluhu Hassan, kaingia akiwa na haraka ya kufanya yake ambayo ni tofauti na yale ya mtangulizi wake. Sijui haraka hii ni ya nini, na haieleweki itamfikisha wapi.

Sasa itabidi achague, ili kurudisha matumaini ya watu kwake. Akichagua kupambana kwa dhati na hawa wanaotafuta kila njia ya kuzoa mali za waTanzania, na akaonekana kweli kasimama kidete bila kujali muhusika, watu watarudi kwake. Na kama atataka kuwa Rais wa hilo kundi linalotumia kila mwanya wa kuwadumaza wananchi katika vipato vyao, sina shaka yoyote hapo atakutana na mapambano mazito zaidi katika miaka hii michache kabla ya 2025.
Mimi namuomba asimame na wananchi, asimamie kwa dhati kabisa juhudi za wananchi kuleta maendeleo ya nchi hii. Wawekezaji wenye hadhi zaidi ya wote ni wananchi wenyewe, hao wanaompapatisha ni kuunga tu juhudi za wananchi wetu.

Yeye anasema: "Tanzania inahitaji zaidi Wawekezaji wa nje, kuliko Wawekezaji wanavyoihitaji Tanzania"
? Nadhani haelewi umuhimu wa Tanzania ulivyo kwa wawekezaji hao. Ndiyo, ni sawa kuweka mazingira mazuri ya kuwavutia waje, lakini hii haina maana ya kwamba thamani ya Tanzania kwa wawekezaji hao ni ndogo kuliko uwekezaji wanaouleta wao.
 
Umeandika uzuri cc Erythrocyte chukua notes
 

Samia mwenyewe ni chaguo la Magufuli na ni mtu wa awamu ya 5 kuhusu awamu ya 6 kajitungia mwenyewe kwa malengo yake binafsi. Yeye ni Rais wa 6 sio awamu ya 6, Usaliti kwa Magufuli ndio unaomtesa ajue hilo Mungu habagui. Unaweza kuwa snitch kisha ukafanikiwa, ni aibu sana akome tena wambomoe kweli hadi amkumbuke Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…