Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Mwaka 2015 Magufuli alipoingia madarakani alipanua wigo wa uteuzi na kuapisha. Tulishuhudia akiteua waliokuwa makada wa CCM zaidi ya 200 na kuwapa nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri (DED) na wengine wakiwa na DAS ( maafisa tawala wa wilaya). Na kisha akawaapisha. Hii ilipelekea ma DED wengi waliokuwapo kabla kubakia "Bench" bila kazi
Kabla ya Mwendazake nafasi hizi zilikuwa ni za watumishi waliopo Halmashauri na wilayani walikuwa wanazipata kwa kupanda ngazi kutegemeana na upatikanaji wa nafasi ya wazi (vacant position) baada ya aliyekuwapo kustaafu, kufariki au kuchukuliwa hatua za nidhamu. Ndipo Wizara inafanya mchakato wa ndani na kupeleka majina kwa Rais kwa uteuzi.
Alichofanya Mwendazake ilikuwa ni uvunjifu wa katiba ya JMT kuwaleta kwenye utumishi wa umma watu ambao ni wanachama wa Chama cha Siasa.
Nashauri kwa Rais SSH chonde chonde katika vitu vibaya vya Mwendazake ulivyoamua kuviacha basi na hiki cha kuteua makada kuwa ma DED na ma DAS usithubutu. Acha mchakato wa utumishi wa umma uchukue nafasi.