Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rudia kusoma ulicho andika mkuu.Hawa akina Upepo wa Pesa ndiyo MATAGA ambao bado wako mateka wa Mwendazake. Jamaa alifanikiwa Sana kufanya brainwash kwa wajinga. Yaani tuko shimoni kuanzia 2015 hadi March 2021 lakini yeye haoni
Mimi simjui ila Standards Person analia lia sana hapa JF kuwa aondolewe Tanga na hata TAKUKURU wamkamate. Nyuzi za kulialila ni kama 50 hivi. Ndipo najiuliza Je, alimtaka akamkataa ndo maana ana husda sana naye?DED wa Tanga ni nani Mkuu kolola ? Na je CV yake ikoje? Au ana kashfa?
Mwendazake aacha makada na madiwani waliobebwa naye wakivurugana mfano tukio hili, kila mmoja anaona ni 'mteule' wa JPM, si mwanasiasa wala mtumishi wa halmashauri wote wanaona wameteuliwa na mamlaka moja yaani Rais
19 May 2021
Dar es Salaam, Tanzania
VURUGU ZAIBUKA KINONDONI,MEYA NA MKURUGENZI WASHIKANA
VURUGU ZAIBUKA BARAZA LA MADIWANI KINONDONI,MEYA NA MKURUGENZI WAVIMBIANA
Source : DarMpya TV
Laiti tungekuwa tunatumia verified names ungeshangaa na hiyo comment yako. Sijawahi kufanya kazi Serikalini, mimi raia tu nachambua na kushauriHuyu jamaa aliyeleta huu uzi naona ni mkurugenzi. Kwa taarifa yako wakurugenzi wengi ni walaji kufuru, wapigaji hasa. Naomba Mh. Rais awashirikishe Mh.Jafo na PM wanawajua wakurugenzi wapigaji, PM anawaita mchwa kwenye Halmashauri. Naomba sana Mh.Rais fanya mabadiliko makubwa kwenye hizi Halm maana ndiko unakopeleka fedha nyingi sasa kama hutaweka watu uanaowaamini ni sawa na kuweka hela kwenye mfuko uliotoboka!.
Humu anapitaAs long as hajaapisha kama anapita humu au watu wake wanapita, basi wapate taarifa. Huu ni ushauri tu.
Mkuu pamoja na kuteuliwa na Rais DED&DC wanareport kwa RC na RAS. Hawana Mamlaka ya kuteport kwa Raid direct.Naunga mkono hoja tatizo langu kubwa hizi nafasi kuteuliwa na Rais hizi nafasi walitakiwa wawajibike katika ngazi ya mkoa huwezi kuwa Rais anateuwa PM, sijui waziri wa Tamisemi, RC, Mkuu wa wilaya mpaka mkurugenzi nyote wateuliwa wa mtu mmoja tech nyote level moja ndio maana hakuna uwajibikaji. Hata kama Rais anapitia teuzi hizi akipitisha natolea mfano mkuu wa Wilaya basi waziri husika ndio amtangaze na aape mbele ya mkuu wa mkoa sio kwa Rais hii itafanya Mkurugenzi ku report kwa mkuu wa Wilaya, Mkuu wa wilaya report kwa RC, RC ku report kwa Waziri, Waziri areport kwa PM direct na indirect kwa Rais. Hatuwezi kuwa sote tuna report kwa mtu mmoja au tunawajibika kwa mtu mmoja. Raisi achikilie mpini kuteuwa na kutengua lazima upate baraka zake kwanza lakini maamuzi yatangazwe ngazi tofauti kuepusha chuki binafsi.
Naelewa hilo lakini umesikia jana waziri wa Tamisemi anasema hajui hii jeuri ya wakurugenzi inatokea wapi, hii ni kwa sababu teule zinatoka kwa mtu mmoja na kutenguwa ni Rais. Huwezi kuna na heshima ikiwa wote mmeteuliwa na mtu huyo huyo mmoja. katika kufikiri kawaida utadhani mkuu wa wilaya ana report kwa RC ila mara nyingi unasikia wanafanyiana visa sababu kila mtu kateuliwa na mtu mmoja. System yetu haiko sawa ukisikia mpaka waziri anasema sijui hii jeuri wanaitoa wapi hawa wakurugenzi. Hata waziri mkuu hawezi kumuwajibisha DED, DC wala RC akichukua anapeleka kwa mamlaka tu.Mkuu pamoja na kuteuliwa na Rais DED&DC wanareport kwa RC na RAS. Hawana Mamlaka ya kuteport kwa Raid direct.
Samahani sana kwa majibu yangu kuhusu ushauri wako kwa Rais SSH. Ukweli ni kwamba uandishi wako ndo umenibabaisha hadi nikaona umetoa ushauri mbovu.Sijajua ushauri wangu ni mbovu kwa kiasi gani kwa kuwa nimesema Rais auache mchakato wa Sheria ya utumishi wa umma ndiyo uwe mwongozo katika kujaza nafasi za ma DED na ma DAS
Umechelewa.
Orodha mpya iko tayari!ll
usipangue Wakurugenzi wa Halmashauri? Ili muendelee kuona na kuwa miungu watu.tena kupanguliwa ni nafuu, hamtarudi kabisaaa. Mfano DED wa Bahi, same, nyangwale,kahama,igunga,ikungi,songwe,tarime,ilala, Geita vijijini,bukombe,mbongwe,chato,nzega,anayekaimu ukurugenzi kule Moshi manispaa kilimanjaro, mnataka kurudi wapi? Mama India hawa wote na wengine wa Aina hiiMwaka 2015 Magufuli alipoingia madarakani alipanua wigo wa uteuzi na kuapisha. Tulishuhudia akiteua waliokuwa makada wa CCM zaidi ya 200 na kuwapa nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri (DED) na wengine wakiwa na DAS ( maafisa tawala wa wilaya). Na kisha akawaapisha. Hii ilipelekea ma DED wengi waliokuwapo kabla kubakia "Bench" bila kazi
Kabla ya Mwendazake nafasi hizi zilikuwa ni za watumishi waliopo Halmashauri na wilayani walikuwa wanazipata kwa kupanda ngazi kutegemeana na upatikanaji wa nafasi ya wazi (vacant position) baada ya aliyekuwapo kustaafu, kufariki au kuchukuliwa hatua za nidhamu. Ndipo Wizara inafanya mchakato wa ndani na kupeleka majina kwa Rais kwa uteuzi.
Alichofanya Mwendazake ilikuwa ni uvunjifu wa katiba ya JMT kuwaleta kwenye utumishi wa umma watu ambao ni wanachama wa Chama cha Siasa.
Nashauri kwa Rais SSH chonde chonde katika vitu vibaya vya Mwendazake ulivyoamua kuviacha basi na hiki cha kuteua makada kuwa ma DED na ma DAS usithubutu. Acha mchakato wa utumishi wa umma uchukue nafasi.
Mh aiseeee mm sijawah kusikia hikinkitu eti mtumishi anapanda cheo kuwa DEDMwaka 2015 Magufuli alipoingia madarakani alipanua wigo wa uteuzi na kuapisha. Tulishuhudia akiteua waliokuwa makada wa CCM zaidi ya 200 na kuwapa nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri (DED) na wengine wakiwa na DAS ( maafisa tawala wa wilaya). Na kisha akawaapisha. Hii ilipelekea ma DED wengi waliokuwapo kabla kubakia "Bench" bila kazi
Kabla ya Mwendazake nafasi hizi zilikuwa ni za watumishi waliopo Halmashauri na wilayani walikuwa wanazipata kwa kupanda ngazi kutegemeana na upatikanaji wa nafasi ya wazi (vacant position) baada ya aliyekuwapo kustaafu, kufariki au kuchukuliwa hatua za nidhamu. Ndipo Wizara inafanya mchakato wa ndani na kupeleka majina kwa Rais kwa uteuzi.
Alichofanya Mwendazake ilikuwa ni uvunjifu wa katiba ya JMT kuwaleta kwenye utumishi wa umma watu ambao ni wanachama wa Chama cha Siasa.
Nashauri kwa Rais SSH chonde chonde katika vitu vibaya vya Mwendazake ulivyoamua kuviacha basi na hiki cha kuteua makada kuwa ma DED na ma DAS usithubutu. Acha mchakato wa utumishi wa umma uchukue nafasi.
Shukran X-bar kwa kukosoa na kutoa pongezi kwenye point nzuriSamahani sana kwa majibu yangu kuhusu ushauri wako kwa Rais SSH. Ukweli ni kwamba uandishi wako ndo umenibabaisha hadi nikaona umetoa ushauri mbovu.
Kichwa cha habari kinasomeka "Rais Samia usipangue Wakurugenzi......." yaani ni kama vile unataka wakurugenzi waliopo ambao ni zao la ubatili wa Magufuli waendelee kubaki kwenye nafasi hizo. Zaidi kwenye aya yako ya mwisho " katika vitu ulivyoamua kuviacha viendelee na hili la wakurugenzi usithubutu" yaani kama vile unatia mkazo wa kumtaka Rais asithubutu kuwapangua bali aache kama alivyoacha hayo mengine.
Lakini sasa baada ya kuelewa makusudio yako narudia tena kukupongeza kwa ufafanuzi wako kuhusu ukiukwaji wa utaratibu wa utezi wa watendaji hawa uliofanywa na Hayati Rais Magufuli.
Huu mkeka au PDF itatoka muda wowote, Je washauri wa Rais SSH wamepita hapa wakasoma haya maoni?Mwaka 2015 Magufuli alipoingia madarakani alipanua wigo wa uteuzi na kuapisha. Tulishuhudia akiteua waliokuwa makada wa CCM zaidi ya 200 na kuwapa nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri (DED) na wengine wakiwa na DAS ( maafisa tawala wa wilaya). Na kisha akawaapisha. Hii ilipelekea ma DED wengi waliokuwapo kabla kubakia "Bench" bila kazi
Kabla ya Mwendazake nafasi hizi zilikuwa ni za watumishi waliopo Halmashauri na wilayani walikuwa wanazipata kwa kupanda ngazi kutegemeana na upatikanaji wa nafasi ya wazi (vacant position) baada ya aliyekuwapo kustaafu, kufariki au kuchukuliwa hatua za nidhamu. Ndipo Wizara inafanya mchakato wa ndani na kupeleka majina kwa Rais kwa uteuzi.
Alichofanya Mwendazake ilikuwa ni uvunjifu wa katiba ya JMT kuwaleta kwenye utumishi wa umma watu ambao ni wanachama wa Chama cha Siasa.
Nashauri kwa Rais SSH chonde chonde katika vitu vibaya vya Mwendazake ulivyoamua kuviacha basi na hiki cha kuteua makada kuwa ma DED na ma DAS usithubutu. Acha mchakato wa utumishi wa umma uchukue nafasi.
Kwa hiyo hata kama alifanya vizuri aondolewe tu kwa sababu ana mlengo wa kisiasa? Mkuu hakuna mtu ambaye atateuliwa kuwa mkurugenzi na Rais kama anaona haendani anae katika mfumo wake. Lakini pia kuna vijana wengi wapo kwenye siasa amabao ni wazuri kiutendaji na kiusimamizi so wapewe nafasi suara la siasa ni hoja mfu isiyo na mashiko.Hawa makada walioko huko kwenye halmashauri inabidi waondoke ili waje wataalamu bila kujali misimamo yao ya kisiasa.
Kama Magufuli alivunja sheria kuwateua basi ni muda muafaka wa rais Samia kurekebisha kosa hilo
Jaffo ndo mkamilifu. Mkuu aangaliwe mtu uzalendo na utendaji lakini mambo ya nani awataje wakurugenzi mafisadi haina tija na huyo unayesema wakurugenzi mafisadi anawajua unauhakiaka yeye ni msafi? Kipimo cha mkurugenzi ni CAG report na usimamizi wa mradi ya serkali na wananchi,tofauti na hapo zitakuwa porojo tu.Huyu jamaa aliyeleta huu uzi naona ni mkurugenzi. Kwa taarifa yako wakurugenzi wengi ni walaji kufuru, wapigaji hasa. Naomba Mh. Rais awashirikishe Mh.Jafo na PM wanawajua wakurugenzi wapigaji, PM anawaita mchwa kwenye Halmashauri. Naomba sana Mh.Rais fanya mabadiliko makubwa kwenye hizi Halm maana ndiko unakopeleka fedha nyingi sasa kama hutaweka watu uanaowaamini ni sawa na kuweka hela kwenye mfuko uliotoboka!.