Rais Samia usipangue Wakurugenzi wa Halmashauri, ile ni nafasi ya utumishi wa umma

Hawa ndioaina ya wakurugenzi walioletwa kung'ata wapinza sasa walishazoea wanaachaje sasa?
 
Huyu jamaa aliyeleta huu uzi naona ni mkurugenzi. Kwa taarifa yako wakurugenzi wengi ni walaji kufuru, wapigaji hasa. Naomba Mh. Rais awashirikishe Mh.Jafo na PM wanawajua wakurugenzi wapigaji, PM anawaita mchwa kwenye Halmashauri. Naomba sana Mh.Rais fanya mabadiliko makubwa kwenye hizi Halm maana ndiko unakopeleka fedha nyingi sasa kama hutaweka watu uanaowaamini ni sawa na kuweka hela kwenye mfuko uliotoboka!.
 
Laiti tungekuwa tunatumia verified names ungeshangaa na hiyo comment yako. Sijawahi kufanya kazi Serikalini, mimi raia tu nachambua na kushauri
 
Hoja imejengwa vibaya. Kwa kuwa the late JPM alijaza makada wa CCM, huoni sasa huu ni muda sahihi kwa Samia kuwapangua na kusimika watu wanaostahili?
 
Hoja imejengwa vibaya. Kwa kuwa the late JPM alijaza makada wa CCM, huoni sasa huu ni muda sahihi kwa Samia kuwapangua na kusimika watu wanaostahili?
Appreciate your contribution, Asante mkuu
 
Mkuu pamoja na kuteuliwa na Rais DED&DC wanareport kwa RC na RAS. Hawana Mamlaka ya kuteport kwa Raid direct.
 
Mkuu pamoja na kuteuliwa na Rais DED&DC wanareport kwa RC na RAS. Hawana Mamlaka ya kuteport kwa Raid direct.
Naelewa hilo lakini umesikia jana waziri wa Tamisemi anasema hajui hii jeuri ya wakurugenzi inatokea wapi, hii ni kwa sababu teule zinatoka kwa mtu mmoja na kutenguwa ni Rais. Huwezi kuna na heshima ikiwa wote mmeteuliwa na mtu huyo huyo mmoja. katika kufikiri kawaida utadhani mkuu wa wilaya ana report kwa RC ila mara nyingi unasikia wanafanyiana visa sababu kila mtu kateuliwa na mtu mmoja. System yetu haiko sawa ukisikia mpaka waziri anasema sijui hii jeuri wanaitoa wapi hawa wakurugenzi. Hata waziri mkuu hawezi kumuwajibisha DED, DC wala RC akichukua anapeleka kwa mamlaka tu.
 
Sijajua ushauri wangu ni mbovu kwa kiasi gani kwa kuwa nimesema Rais auache mchakato wa Sheria ya utumishi wa umma ndiyo uwe mwongozo katika kujaza nafasi za ma DED na ma DAS
Samahani sana kwa majibu yangu kuhusu ushauri wako kwa Rais SSH. Ukweli ni kwamba uandishi wako ndo umenibabaisha hadi nikaona umetoa ushauri mbovu.

Kichwa cha habari kinasomeka "Rais Samia usipangue Wakurugenzi......." yaani ni kama vile unataka wakurugenzi waliopo ambao ni zao la ubatili wa Magufuli waendelee kubaki kwenye nafasi hizo. Zaidi kwenye aya yako ya mwisho " katika vitu ulivyoamua kuviacha viendelee na hili la wakurugenzi usithubutu" yaani kama vile unatia mkazo wa kumtaka Rais asithubutu kuwapangua bali aache kama alivyoacha hayo mengine.

Lakini sasa baada ya kuelewa makusudio yako narudia tena kukupongeza kwa ufafanuzi wako kuhusu ukiukwaji wa utaratibu wa utezi wa watendaji hawa uliofanywa na Hayati Rais Magufuli.
 
Umechelewa.

Orodha mpya iko tayari!ll

usipangue Wakurugenzi wa Halmashauri? Ili muendelee kuona na kuwa miungu watu.tena kupanguliwa ni nafuu, hamtarudi kabisaaa. Mfano DED wa Bahi, same, nyangwale,kahama,igunga,ikungi,songwe,tarime,ilala, Geita vijijini,bukombe,mbongwe,chato,nzega,anayekaimu ukurugenzi kule Moshi manispaa kilimanjaro, mnataka kurudi wapi? Mama India hawa wote na wengine wa Aina hii
 
Mh aiseeee mm sijawah kusikia hikinkitu eti mtumishi anapanda cheo kuwa DED
Tangia enzi za JK hizi nafasi ni uteuzi wa. Mamlaka ya juu ya nchi.... Yy ndio huteua na jopo lake mara zote makada ndio humulikwa barabaraa tena ukumbuke hawa ndio wasimamizi wakuu wa uchaguzi katika halmashauri zao so strategically wengine huchaguliwa kuzingatia kukinda jimbo au kulinda jimbo fulani .....

Hapa nakupa na mfano mwaka 2010 pale arusha, uchaguzi wa meya ..DED huchezesha michezo,
Na baadhi ya walio wahi kuwa ma DED zaman sasa ivi wapo mjengoni kukitumikia chama.
 
Shukran X-bar kwa kukosoa na kutoa pongezi kwenye point nzuri
 
Huu mkeka au PDF itatoka muda wowote, Je washauri wa Rais SSH wamepita hapa wakasoma haya maoni?
 
Hawa makada walioko huko kwenye halmashauri inabidi waondoke ili waje wataalamu bila kujali misimamo yao ya kisiasa.
Kama Magufuli alivunja sheria kuwateua basi ni muda muafaka wa rais Samia kurekebisha kosa hilo
Kwa hiyo hata kama alifanya vizuri aondolewe tu kwa sababu ana mlengo wa kisiasa? Mkuu hakuna mtu ambaye atateuliwa kuwa mkurugenzi na Rais kama anaona haendani anae katika mfumo wake. Lakini pia kuna vijana wengi wapo kwenye siasa amabao ni wazuri kiutendaji na kiusimamizi so wapewe nafasi suara la siasa ni hoja mfu isiyo na mashiko.
 
Jaffo ndo mkamilifu. Mkuu aangaliwe mtu uzalendo na utendaji lakini mambo ya nani awataje wakurugenzi mafisadi haina tija na huyo unayesema wakurugenzi mafisadi anawajua unauhakiaka yeye ni msafi? Kipimo cha mkurugenzi ni CAG report na usimamizi wa mradi ya serkali na wananchi,tofauti na hapo zitakuwa porojo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…