Umenena vema kabisa, kwa VP alikosea sana, lakini wakati ule alikua bado hana mamlaka kwenye chama. Sasa anayo, ayatumie kwa manufaa ya nchi. Kinyume chake tutakuwa na rais kivuli.
Huo ndio ukweli .
Mungu Mama Samia akumbuke kuwa aliyemuinua toka chini mpaka juu ni Mungu wa Haki sio CCM ya awamu ya Tano .
Aliyempa nafasi hiyo kwa ghafla ni Mungu aliyempa Uhai yeye na kumchukua aliyekua juu ili Mama achukue nafasi.
Genge la Mafisadi na Mabeberu weusi wanaojiita CCM wamekua wakijiona kuwa wao ndio walioumba Rasilimali za nchi hii ,genge la wezi wanaojiita CCM wamekua wakiwaaminisha watu kuwa wao ndio walioweka amani ya nchi hii wakati watoto wao hawajawahi kulala nje wakilinda mipaka na doria ndani ya nje usiku kucha ni kazi za watoto wa maskini na wakulima. Genge la walevi wanaojiita CCM wanaopunguza kodi kwenye pombe na kuweka mawaziri walevi na wahuni kwa kodi za watanzania wamekua wakiwaaminisha watanzania kuwa wao ndio waliowaunganisha watanzania wakati wanawagawa watanzania kwa makabila yao kwenye teuzi na hata kutaka kumuua Mbowe kwa kumnyima matibabu ni kutokana na Genge la S. Gang kuona nafasi zao zitapungua endapo katiba mpya itapatikana.
Katiba iliyopo inawapa watu waovu nafasi ya kufanya kazi kwa hisia badala ya sheria.
Nchi hii ina dini zinazomtaja Mungu wa Haki kwa 90% ,yaani dini ya Ukristo na Uislam . Nchi hii ina mawaziri na wakubwa wao wanaomtaja Mungu wa Haki aliyeumba vitu vyote duniani na anaamua kumuinua nani na kumshusha nani.
Imani hizo kwenye mioyo ya watu ni hukmu Kali sana.
Mama Samia Rais aliyeinuliwa ghafla na Mungu atafakari sana hilo na ajiulize Kuwa ni kwa nini Familia za wale MARAIS wapole na wavumilivu kama Kikwete,Mwingi na Karume zinainuliwa na Mungu. Japo walikumbwa na madhila makubwa ya kutukanwa na kudhalilishwa. Mwinyi alitukanwa sana Lakini akavumilia na akatenda kwa utu kwa watu wake na hakuumiza watu kwa sababu ya kulinda jina CCM lililopo kwenye Makaratasi na lililoanzishwa na kikundi cha watu kwa sababu za wakati huo kwa manufaa ya wakati huo na mbinu za wakati huo . Hata hivyo tunaona jinsi Mungu alivyomlipa mema Mzee Mwinyi kwake na kwa vizazi vyake. Mama Samia ajifunze kuwa Mungu anafurahishwa na Haki kuliko Kujenga Maminara(madaraja) kama yale ya babeli kwa damu za wapinzani. Mh.Rais Samia asome katiba vizuri na Kitabu Chake cha dini alivyovishika wakati wa kuapa ili asimamie Haki hata kama haki hiyo italisambaratisha lile kundi lililokua linanufaika awamu ya Tano. Mama Samia aangalie asije akapoteza thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwafurahisha wahuni na watu waliojaa ukabila na ukanda na ulafi na uroho wa madaraka ndani ya CCM kwa manufaa yao huku akimuudhi Mwenyezi Mungu
Ni wazi kuwa dunia imeingiwa na hofu kubwa na ugonjwa wa korona wakati ambao dunia ilikua inatawaliwa na viongozi Katili.
Viongozi katili wanatawala kwa damu na vifo vya wanadamu.
Viongozi katili wanajaza watu magerezani huku wakiacha mayatima na wajane wengi mitaani. Mungu kamwe hajawahi kupendezwa na viongozi katili,wahuni,walevi, walafi ,wanafiki, wenye kujivuna ,wasiojali maumivu ya wanadamu wenzao.
Dunia ilikumbwa na korona wakati ambao dunia ilikua na watawala katili na wababe kuanzi kule China,Marekani,Korea,Urusi, Irani, Israel, Tanzania( nchi ambayo ni kimbilio la watu wenye upole na umoja,utu,usawa) n.k. Dunia ilikumbwa na korona wakati ambapo watawala walikua wanawaza mamlaka yao tu huku damu za watu zikiwa zinamwagwa kwa risasi kila mahali bila kuchukua hatua. Taifa kubwa kama China limekua msaada mkubwa sana kwa Madikteta duniani . Na mafikteta wamekua wakitumia China na urusi kama ngao yao ya kuwaua na kuwaumiza watu kwenye nchi zao.
Tramp naye akahitoa kwa kuwaita Watawala wasiojali watu wao kuwa ni watawala wa Shithole countries . Matokeo yake dunia nzima ikaanza kuwa na watawala katili wanaolenga kufia madarakani na kurudisha tawala za kifalme.
Korona ikaibuka ili kila mtu ajue kuwa dunia sio Mali ya kikundi cha watu. Sasa kila mtu ana hofu .
Ni wapumbavu peke yao ndani ya CCM na baadhi ya makada wao ndani ya vyombo vya dola wasioona huo upanga ulioinuliwa juu ya dunia nzima( korona) ndio wanaowaza kujilimbikizia mali kwa dhulma na madaraka badala ya kutafakari hatima ya maisha yao watakaporejea kwa Muumba wa vitu vyote. Wanaona hata Korona inawaogopa kama walivyokuwa wanasema kuwa Korona iliondolewa na Mwendazake. Kwa uovu wao na kiburi chao walisahau kuwa maombi na dua za watanzania zilielekezwa kwa Mungu na sio kwa Mwendazake.
Mama yetu Samia Suluhu afahamu kuwa kama Mungu alikua ametuleta duniani ili baadhi waumizwe kwa ajili ya kile kilichoitwa maendeleo basi bila shaka Awamu ya tano isingekoma ghafla mana yule Mwendazake alikua na kasi zaidi kwenye ujenzi wa nchi kama alivyokua mwasisi wa Freemason ,Mfalme Nimrodi aliyejenga Mnara wa Babeli na kujiinua kwa kutukuzwa na kuonekana kuwa yuko juu ya kila kitu.
Mungu alikua na sababu zake kumwinua Mama Samia na alikua na sababu tofauti hivyo Mama atoke hadharani ajipambanue kwa kuunda serikali inayoendana na dhamira yake. Bila shaka Mungu atamlinda na hakuna atakayeweza kumdhuru wala kumtoa madarakani. Lakini kwa sasa hao watu walioanza kutengeneza filamu za kigaidi watamletea jambo baya sana mana ni genge baya sana lililokua limepandwa kikanda na kikabila na kidini. Ndio maaana lilikua limeshajiona lipo juu ya kila kitu.
Mama asiogope kupiga chini mtu yeyote. Mkaa unawaka ukiwa na mikaa mingine tena kwa kuwashwa. Yeyote akiwekwa pembeni anazimika tu wala hana nguvu. Asimuogope yeyote yule.
Haya yanayotokea ni aibu kwa Taifa zima mana vitabu vya dini vinatufundisha kuwa HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE.
Hivi Mbowe angekua gaidi angemwacha Sabaya aliyemfanyia kila aina ya ukatili na dhulma ?
Sijawahi kumuunga mkono Mbowe lakini najua uchungu na maumivu anayoyapitia kifamilia kwa sababu tu kuna watu wanalinda vyeo vyao na uovu wao. Waliopaswa kufungwa ndio wanaofunga watu.
Mungu anachukizwa sana na dhulma.
Kabla ya kukataa chanjo ya Korona Gwajima akatae dhulma na ahubiri juu ya Toba na kuacha dhambi. Vinginevyo wakichanjwa watakufa na dhambi zao , wasipochanjwa watakufa na dhambi zao pia.
Naichukia sana dhulma.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app