Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Rais Samia akizungumza na wananchi wa kata ya Laela ,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Rukwa mesema leo tarehe 17 Julai 2024 ikiwa siku ya mwisho ya kukamlisha kwa ziara yake ya siku tatu "Wengine waacheni waendelee kujifunza bado wachanga, muda wao wakuendesha Dola bado Kabisa"
"Lazima tuwe na Serikali makini inayowekwa na chama makini, niwaombe sana, mwaka huu mwisho wa mwaka mwezi wa 10 wa 11 kule tunakwenda kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tunakwenda kuchagua viongozi wa mitaa na viongozi wa vitongoji.
Niwaombe sana ndugu zangu, nendeni mkachague chama cha Mapinduzi, nendeni mkatuchague Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndicho chama kilichoweka Serikali makini inayomimina maendeleo kwa watanzania, inayomimina maendeleo kwa watu, wa majimbo ya Tanzania.
Unapozungumza maji, elimu, afya umeme, kilimo na mambo mengine ni chama cha Mapinduzi, naomba sana chagueni chama cha Mapinduzi, tupite vizuri ili maendeleo yaje na mengine na mengine na mengine zaidi.
Wengine waacheni bado waendelee kujifunza, bado ni wachanga ni watoto wetu wa chama cha Mapinduzi, kwa hiyo waachieni waendelee kujifunza muda wao wa kuendesha dola ni bado kabisa kabisa kabisa, kwa hiyo niwaombe sana niwaombe sana ndugu zangu kachagueni chama cha cha Mapinduzi."
Pia soma: