Pre GE2025 Rais Samia: Waacheni wajifunze, muda wao wa kuendesha dola bado

Pre GE2025 Rais Samia: Waacheni wajifunze, muda wao wa kuendesha dola bado

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais Samia akizungumza na wananchi wa kata ya Laela ,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Rukwa mesema leo tarehe 17 Julai 2024 ikiwa siku ya mwisho ya kukamlisha kwa ziara yake ya siku tatu "Wengine waacheni waendelee kujifunza bado wachanga, muda wao wakuendesha Dola bado Kabisa"

"Lazima tuwe na Serikali makini inayowekwa na chama makini, niwaombe sana, mwaka huu mwisho wa mwaka mwezi wa 10 wa 11 kule tunakwenda kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tunakwenda kuchagua viongozi wa mitaa na viongozi wa vitongoji.

Niwaombe sana ndugu zangu, nendeni mkachague chama cha Mapinduzi, nendeni mkatuchague Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndicho chama kilichoweka Serikali makini inayomimina maendeleo kwa watanzania, inayomimina maendeleo kwa watu, wa majimbo ya Tanzania.

Unapozungumza maji, elimu, afya umeme, kilimo na mambo mengine ni chama cha Mapinduzi, naomba sana chagueni chama cha Mapinduzi, tupite vizuri ili maendeleo yaje na mengine na mengine na mengine zaidi.

Wengine waacheni bado waendelee kujifunza, bado ni wachanga ni watoto wetu wa chama cha Mapinduzi, kwa hiyo waachieni waendelee kujifunza muda wao wa kuendesha dola ni bado kabisa kabisa kabisa, kwa hiyo niwaombe sana niwaombe sana ndugu zangu kachagueni chama cha cha Mapinduzi."

Pia soma:LIVE - Rais Samia akizungumza na wananchi wa Rukwa katika Uwanja wa CCM Mandera Mazwi Manispaa ya Sumbawanga, leo Julai 17, 2024

Yaani wapinzani wajifunze kutoka CCM, anataka vyama vyote wawe majizi kama walivyo wao? Watu wanataka chama kilicho tofauti na CCM, kwa sababu CCM kwa sasa ni laana. Hakuna uovu mkubwa nchi hii usioihusisha CCM.
 
Huyo mama ana dharau za kijinga sana. Anaongea ujinga , akisemwa kidogo anaanza kulia.
 
Mama anahangaika na watoto wachanga wa nn si anatakiwa kitokuwaongelea? Au wanamsumbua? Na bado acheze tu Rukwa, Ruvuma, Morogoro na Mikoa mingine. Hao huenda wakamuelewa.
Muda wa uchaguzi bado. Jamani kampeni za nn! Na wengine waanze au? Wakianza mtasema na polisi mtakwenda. Sometimes viongozi Huwa mnawachokoza raia. Si mkae kimya tuheshimu Katiba na taratibu tulizojiwekea kuilinda amani ya taifa hili?

Kila siku msiwachague, msiwachague, wapinzani Wana hili Wana lile si tusibiriane tuanze mbio pamoja? Mbona hamjiamini? Kwani mmekosea wapi mnajihami kila mara? Mara Makalla huku, mara Nape kule, mara mama Samia kule Kwan vp! Akina Nan wanakisumbua chama kubwa hamlali?
 
Rais Samia akizungumza na wananchi wa kata ya Laela ,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Rukwa mesema leo tarehe 17 Julai 2024 ikiwa siku ya mwisho ya kukamlisha kwa ziara yake ya siku tatu "Wengine waacheni waendelee kujifunza bado wachanga, muda wao wakuendesha Dola bado Kabisa"

"Lazima tuwe na Serikali makini inayowekwa na chama makini, niwaombe sana, mwaka huu mwisho wa mwaka mwezi wa 10 wa 11 kule tunakwenda kuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tunakwenda kuchagua viongozi wa mitaa na viongozi wa vitongoji.

Niwaombe sana ndugu zangu, nendeni mkachague chama cha Mapinduzi, nendeni mkatuchague Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndicho chama kilichoweka Serikali makini inayomimina maendeleo kwa watanzania, inayomimina maendeleo kwa watu, wa majimbo ya Tanzania.

Unapozungumza maji, elimu, afya umeme, kilimo na mambo mengine ni chama cha Mapinduzi, naomba sana chagueni chama cha Mapinduzi, tupite vizuri ili maendeleo yaje na mengine na mengine na mengine zaidi.

Wengine waacheni bado waendelee kujifunza, bado ni wachanga ni watoto wetu wa chama cha Mapinduzi, kwa hiyo waachieni waendelee kujifunza muda wao wa kuendesha dola ni bado kabisa kabisa kabisa, kwa hiyo niwaombe sana niwaombe sana ndugu zangu kachagueni chama cha cha Mapinduzi."

Pia soma:LIVE - Rais Samia akizungumza na wananchi wa Rukwa katika Uwanja wa CCM Mandera Mazwi Manispaa ya Sumbawanga, leo Julai 17, 2024
Basi. Kama ni hivyo tusingepata uhuru. Tungesubiri mpaka mwingereza aseme hivo. " It is rediculous"!
 
Bullshit!

Lugha za kikoloni hizo.

Nyerere alikuwa na ukomavu gani alipo chukua nchi toka kwa wakoloni?

Samia ni mweupe sana aisee.

Imagine Samia ana debate na Lissu…..

It would be a massacre!
Umenifurahisa sana uliposema "It would be a massacre!"... kwa kweli itakuwa ni mtafutano, sijui hata kama debate ataikubali...
 
huhitaji kukomaa kuiongoza Tanzania, mtanzania wa kawaida kabisa anaweza kuwa Rais wa Tanzania maana sidhani kama kwasasa inahitajika akili kubwa sana kuwaongoza watanzania.

Unahitaji akili kubwa sana na ukomavu kuwaongoza waKenya.
 
Binafsi sijasoma bali nina elimu ya kitaa jumlisha ujanja ujanja na exposure kila nikijipima najiona kabisa naweza kuwa Rais wa Tanzania na nikafanya wonders ndani ya miaka mitano kuliko hata awamu zote sita kwapamoja.
 
Japo Ukweli huu Wafuasi wa Chadema huwa hawaukubali lakini ndio hali halisi

Kama swala la COVID-19 limewashinda, swala la Mchungaji Msigwa limewashinda ndio wataweza kuongoza DOLA hawa?

Wapinzani wa Tanzania ni afadhali ya Gen Z wanajua wanachofanya

Mlale Unono 🐼
Heri uzi umeupandisha muda wa giza ingekuwa kweupe ufipa wangekuteka wakamsingizia muliro!
 
Na mwakani n mwendo wa hv tuu
FB_IMG_1715771188553.jpg
 
Back
Top Bottom