Rais Samia Wachukulie hatua wanajeshi wanaofanyafanya vurugu mitaani-Hii ni aibu isiyokubalika hata kidogo!

Rais Samia Wachukulie hatua wanajeshi wanaofanyafanya vurugu mitaani-Hii ni aibu isiyokubalika hata kidogo!

mwanzo wa ngoma ni lele, na samaki mkunje angali mbichi. Leo hii tukivumilia vitendo vibaya kabisa visivyo na heshima wala Taswira ya jeshi la Wananchi tunalolijua, ipo siku watafanya jambo baya kabisa katika nchi na kutishia amani na utulivu wa Taifa zima
Yote tisa. Nawaona wale waliokuwa kimbelembele kudai Jeshi Liwahamishe ndugu zetu "Wamasai" Ngorongoro, ati kwa hiari zao. Wakikemea kitendo kilichotokea Kawe.

Je hao waliokuwa wanaomficha Jambazi aliymuuwa mwanajeshi hawakufanya hayo kwa hiari zao? Pole zao.

Pointi ni kuwa mliyavumilia matendo ya hovyo na ya kinyama kufanyiwa Wamasai na wengi wenu mlikuwa mnawabeza na kuwadhihaki Wamasai badala ya kukemea maovu ya Jeshi letu.

Hamkunyoosha vidole! kwani, unyambisi ni unyambisi tu

Hata hivyo, siungi mkono kitendo hicho cha polisi wa Kijeshi Kawe.

Tanzania inahitaji mapinduzi ya haraka.
 
Wewe shule imekupita kushoto,hivi kama Kato aliweza kumlaza kanali,unadhani ukikutana namimi,ntakufanyaje...?
Utachezea kichapo cha mbwa koko.
Alimlaza kwa kumvizia, alipopigwa vibao kwa nn hakuzipanga kama kidume kweli. ukikutana na mm ntakutindua mtaro hadharani bila kilainishi, yaan hata mate sintopaka.
 
Mawazo ya baadhi ya wanajeshi kudhani wako juu ya raia ni mawazo potofu. Nguvu ya kijeshi iko ndani ya kamandi na siyo mtu mmojammoja!​
Yaa nafikiri hawana uelewa, mambo ya amri na kuwajibishana kijeshi yanatakiwa yawe ndani ya ranks zao ndani ya jeshi, kwa kuwa wanajeshi wanawatii viongozi wa kiraia hivyo hivyo wanatakiwa kuwatii raia kwa sababu viongozi akiwemo rais wapo hapo kwa matakwa ya raia.

Hii ya kudhani wana mamlaka ya kuwapiga raia ni kukosa uelewa kwa sababu raia ndo wenye mamlaka ya kuwaamuru wanajeshi kufanya hiki au kile kwa sababu hilo jeshi ni la kwao na wao ndo wanaliendesha kwa kodi zao, na hata kama dereva wa bajaj alimwomba mwanajeshi kuweka gari pembeni ili apite alimstahi sana, kimsingi alitakiwa ampe amri aweke gari pembeni ili apite.

Nafikri ni wachache sana wataelewa nilichoandika hapa.​
 
Nashangazwa eti tunamuomba mkulu ashugjulikie jeshi

Jeshi hili hili au lingine? Waliokaa kimya na uuzwaji wa rasimali za nchi?

Actualy kwenye suala hilo even wananchi wamekaa kimya, wote wanalalamikia kwenye social media
Wengine wakageuka kuwa chawa
Hata kama ningekuwa nipo inservice, Siwez tetea kizazi kisichojielewa ,umoja 0
 
UN wanajeshi wa Tanzania tumewarudisha nyumbani Kwa kashfa ya NGONO, TZ,wanajeshi wametangaza kusaka chupi mitaani, Mabeyo apewa V8 iliaendelee Kula na wahuni wa CCM nimeandika haya ili muone kama mna walinzi au wahuniii !!haya ni matokeo ya nchi kuchagua viongozi na jeshi kwa njia za rushwa ,Mimi huku mitaani nawaambia kabisa nyinyi ni wasichana tu wanajeshi wapo Africa magharibi sio nyinyi .

Ni baadhi lakini si wote. Ni wale wenye tuhuma hizo.
Tuwe honest kwenye kundi lolote lile wapo watao misbehave, mtaani hata maofisini lakin haimaanishi jeshi zima ndio liko hivyo
 
UN wanajeshi wa Tanzania tumewarudisha nyumbani Kwa kashfa ya NGONO, TZ,wanajeshi wametangaza kusaka chupi mitaani, Mabeyo apewa V8 iliaendelee Kula na wahuni wa CCM nimeandika haya ili muone kama mna walinzi au wahuniii !!haya ni matokeo ya nchi kuchagua viongozi na jeshi kwa njia za rushwa ,Mimi huku mitaani nawaambia kabisa nyinyi ni wasichana tu wanajeshi wapo Africa magharibi sio nyinyi .
Naunga mkono hoja 👍👏👏👏👏👏👏
 
yaani nalishangaa sana jesh letu sijui wamekuweje tu,
Wewe huenda ni Kizazi kilichozaliwa wakati Nchi hii inaongozwa na Sungusungu ambao ndio walikuwa Polisi na Mahakama.

Ushauri wako ni sawa na kusema Vituo vya Polisi vifanywe kuwa Migahawa na Mahakama zigeuzwe kuwa Bar na Mahakama kuu ifanywe kuwa 4 star Hotel.

Ni LAZIMA tujiongoze kwa KATIBA na SHARIA tulizojiwekea,laa Nchi itageuka kuwa MONKEY JUNGLE.
 
umesema SHARIA? unajua maana ya SHARIA? Unajua utawala wa SHARIA unavofanya kazi?
 
Wewe huenda ni Kizazi kilichozaliwa wakati Nchi hii inaongozwa na Sungusungu ambao ndio walikuwa Polisi na Mahakama.

Ushauri wako ni sawa na kusema Vituo vya Polisi vifanywe kuwa Migahawa na Mahakama zigeuzwe kuwa Bar na Mahakama kuu ifanywe kuwa 4 star Hotel.

Ni LAZIMA tujiongoze kwa KATIBA na SHARIA tulizojiwekea,laa Nchi itageuka kuwa MONKEY JUNGLE.
hii nchi haijawai kuongozwa na sungusungu we bwege.
 
Yaa nafikiri hawana uelewa, mambo ya amri na kuwajibishana kijeshi yanatakiwa yawe ndani ya ranks zao ndani ya jeshi, kwa kuwa wanajeshi wanawatii viongozi wa kiraia hivyo hivyo wanatakiwa kuwatii raia kwa sababu viongozi akiwemo rais wapo hapo kwa matakwa ya raia.

Hii ya kudhani wana mamlaka ya kuwapiga raia ni kukosa uelewa kwa sababu raia ndo wenye mamlaka ya kuwaamuru wanajeshi kufanya hiki au kile kwa sababu hilo jeshi ni la kwao na wao ndo wanaliendesha kwa kodi zao, na hata kama dereva wa bajaj alimwomba mwanajeshi kuweka gari pembeni ili apite alimstahi sana, kimsingi alitakiwa ampe amri aweke gari pembeni ili apite.

Nafikri ni wachache sana wataelewa nilichoandika hapa.​
huna ulichoandika hapa ni uharo tu, hata wanajeshi wanalipa kodi, wanakatwa paye kwenye mishahara yao. wana uhuru wa kvtumia barabara kama ambavo na wewe una uhuru huo, jeshi la polisi ndo linawajibika kwa raia, ndo walinzi wa raia na mali zao.
 
Soma taratibu kilichoandikwa, acha kuleta mihemuko.
 
Salaamu kwako Mheshimiwa Rais

Mheshimiwa Rais, nianze kwa kusema kuwa mimi raia wa Tanzania, nina heshima kubwa kwa Jeshi letu la wananchi. Kazi waliyoifanya kwa miaka zaidi ya 60 ya ulinzi wa Taifa letu ni njema sana, kwa kweli imekuwa msingi na nguzo kuu ya amani na utulivu wa wa Taifa letu

Hata hivyo, Hivi karibuni zimezuka taarifa za wanajeshi wachache, wasiojua miiko na viapo vya kazi yao, wameamua kuvunja sheria na kuingia mtaani na kuanza kupigapiga watu hovyo.
Tukio hili limetokea baada ya kutokea taarifa za kuuawa kwa mwanajeshi na mwananchi baada ya kinachosemekana ugomvi wa raia na mwanajeshi huyo. Baada ya tukio hilo kundi la wanajeshi limeingia mitaani na kuanza kupigapiga raia hovyo eti "kuwatia adabu".

Mheshimiwa Rais naomba nikueleze mambo yafuatayo:

1. Mosi ni aibu kwa jeshi kuvunja sheria, na kukiuka misingi ya kisheria ya uanzishwaji wake.
Katika nchi yoyote, majeshi yanapaswa kuwa ni vyombo vya kinidhamu, mfano bora kwa wananchi na taswira chanya ya kuonyesha namna gani sheria zinavyopaswa kutiiwa. Kitendo cha Wanajeshi kuvunja sheria waziwazi , kinaidhalilisha serikali yako, na kimsingi kinakudhalilisha wewe Amiri jeshi mkuu ambaye leo hii vijana wako wanaingia mitaani na kubehave kama watu wa fujofujo, badala ya watu sober wenye nidhamu ya hali ya juu.

2. Pili, wanajeshi wanaoact kwa utaratibu huu wanaonyesha udhaifu badala ya nguvu, hawatufai, wachukuliwe hatua kali za kinidhamu

Mheshimiwa Rais, nguvu ya jeshi wala siyo uwezo wake wa kupita mitaani na kupiga wanawake,, watoto, wazee na vijana. Bali uwezo wa jeshi unapimwa kwa namna gani unatii katiba ya nchi, mipango madhubuti ya ulinzi wa Taifa na medani. Kama Jeshi la Wananchi linadhani liko Juu ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajindanganya sana. Legitimacy yake kwa umma siyo uwezo wa kufanya vurugu mitaani, bali legitimacy yake na heshima yake itapatikana kwa kulinda uhuru wa Taifa letu na kuwa nguzo ya usitawi, na siyo kufanyafanya fujo mitaani.

3. Mheshimiwa Rais, Hata sisi raia ni jeshi la akiba

Kitendo cha watu wachache wenye uniform kuingia mitaani na kupigapiga watu kimsingi ni kama jeshi kupigana na wenzao tu ambao hawana uniform. Pengine wanajeshi wetu, ambao wewe ni Amiri jeshi mkuu wake inapaswa waelewe kuwa, Uniform hizo wanazovaa ni kwa ridhaa yetu, kwamba tumeamua wachache wawe mbele kwenye ulinzi wa Taifa lakini Pindi Taifa likihitaji ulinzi, sisi sote tutakuja front kulilinda. Sasa kitendo cha wachache walio katika uniform kuingia mitaani na kufanyafanya vurugu, ni kitendo cha aibu, kisichovumilika na cha kukemewa na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa hili.

4. Mheshimiwa Rais, tukilea tabia hizi za hovyo za baadhi ya wanajeshi kupiga na kuonea raia, ipo siku watafanya tukio kubwa zaidi.

Mheshimiwa rais, mwanzo wa ngoma ni lele, na samaki mkunje angali mbichi. Leo hii tukivumilia vitendo vibaya kabisa visivyo na heshima wala Taswira ya jeshi la Wananchi tunalolijua, ipo siku watafanya jambo baya kabisa katika nchi na kutishia amani na utulivu wa Taifa zima. Ni lazima hatua kali zichukuliwe kwa hawa wachache waiojua nini maadili ya kazi yao ili kulinusuru Taifa dhidi ya wanajeshi wenye mentality za vuruguvurugu kama hawa wanaopita mitaani na kufanya fujo.
Mheshimwa wanajeshi hawa wachache wenye kufanya matendo haya ya kihuni siyo aina ya wanajeshi ambao baba wa Taifa alijivunia kuwa tuna JESHI LA WANANCHI. Tunaomba wahusika wote waliohusika wachukuliwe hatua kali kabisa za kisheria na kinidhamu.

5. Mheshimiwa Rais hatuwezi kuvumilia Panya Road wa Kiraia, na kamwe hatuwezi kuvumilia panyaroad wa Kijeshi.

Matendo wanayofanya hawa wanajeshi wachache wasio na nidhamu hayana tofauti na matendo wanayofanya vijana wachache wa kiraia wasio na nidhamu waitwao Panyaroad. Hivi inawezekanaje mwanajeshi unaingia mtaani na kuanza kupigapiga klla mtu apitaye. Sasa unataka kuachieve nini?. Kwamba unataka raia wakuogope?, ili iweje na kwa nini?. Mheshimiwa Rais, ili jeshi lifanikiwe linahitaji mgongo wa Raia. Ni mentality potofu kudhani eti Jeshi liko juu ya raia na kwa hivyo wanajeshi wanaweza kupiga, kujeruhi, kuvunjia heshima watu eti kwa sababu ni wanajeshi. Hili tumelikataa na tunalikataa kwa moyo wetu wote. Tunataka Jeshi liendelee kuwa na sifa ya nidhamu na yeyote atakayejiinua ndani ya majeshi yetu na kujifanya panya road wa kijeshi huyo hatufai, avue uniform aingie mtaani akafanya mambo yake huko akakumbane na mkono wa sheria!

Mwisho namalizia kwa kusema kuwa, nina Imani na Mkuu wa Majeshi, nina imani na Mnadhimu wa majeshi na bado nina imani na Jeshi kiujumla. lakini matendo haya yaliyotokea Kawe yamelitia doa jeshi na ni lazima lichukue hatua. Tunahitaji heshima ya jeshi letu iendelee kuwa palepale, na siyo kuwa na vikundi vya reactionaries, wapenda fujo ndani ya komandi, wanaodhani eti kufanya "zali" au "kulianzisha" ndiyo ukamanda wenyewe. Huo siyo ukamanda, bali ni uhalifu. Hao waliohusika wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria mara moja ili tabia hizi za kupigapiga wanachi zikome mara moja, hazikubaliki hata kidogo!
Haya umesikika
 
Back
Top Bottom