Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,024
- 11,546
Kwani mchungaji Gwaji boy anasemaje
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu acha kuidanganya saikolojia yako.....!Mwisho namalizia kwa kusema kuwa, nina Imani na Mkuu wa Majeshi, nina imani na Mnadhimu wa majeshi na bado nina imani na Jeshi kiujumla. ....
Ndio madhara ya kuwa na jeshi la watu wapumbavu ,wasi na elimu , exposure ,akili wala maadiliKwani mtuhumiwa hajakamatwa?
Huo msako wao wanamsaka nani? Jueni hamko juu ya Sheria sababu nchi hii ni yetu sote hamuwezi kuilinda pekeyenu.
Jeshi lijitahidi kuajiri watu wenyewe shule angalau mambo haya yatapungua.
Ndio madhara ya kuwa na jeshi la watu wapumbavu ,wasi na elimu , exposure ,akili wala maadiliKwani mtuhumiwa hajakamatwa?
Huo msako wao wanamsaka nani? Jueni hamko juu ya Sheria sababu nchi hii ni yetu sote hamuwezi kuilinda pekeyenu.
Jeshi lijitahidi kuajiri watu wenyewe shule angalau mambo haya yatapungua.
Kwanza elezea kwa undani why mwenzao kauliwa,Yani yalioongelewa yote hujaelewa kitu yani umeona wanajeshi wamehujumiwa na wanastahili kupiga watu hovyo mtaani
Hii nchi ni ngumu sana
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Umeona mwenzio alivyorudisha namba kwa kuleta ubabe wa kijinga?- Jifanye mbabe likikukuta unazikwa wewe na ndugu yako peke yako na maisha yanaendelea.Tutazidi kutembeza kichapo kama huwezi ishi kwa nidhamu karibu na utawala zetu nenda kaishi uswahilini, maswala ya ugomvi wa ovyo hatutaki mtakaribisha magaidi wafanye icho mnachokiona ni haki yenu kujibishana na mwanajeshi , leo jumapili mpo nyumbani wote tunakuja tembez rungu kuanzia watoto baba hausigeli adi mifugo na panya wote wa ndani
Salaamu kwako Mheshimiwa Rais
Mheshimiwa Rais, nianze kwa kusema kuwa mimi raia wa Tanzania, nina heshima kubwa kwa Jeshi letu la wananchi. Kazi waliyoifanya kwa miaka zaidi ya 60 ya ulinzi wa Taifa letu ni njema sana, kwa kweli imekuwa msingi na nguzo kuu ya amani na utulivu wa wa Taifa letu
Hata hivyo, Hivi karibuni zimezuka taarifa za wanajeshi wachache, wasiojua miiko na viapo vya kazi yao, wameamua kuvunja sheria na kuingia mtaani na kuanza kupigapiga watu hovyo.
Tukio hili limetokea baada ya kutokea taarifa za kuuawa kwa mwanajeshi na mwananchi baada ya kinachosemekana ugomvi wa raia na mwanajeshi huyo. Baada ya tukio hilo kundi la wanajeshi limeingia mitaani na kuanza kupigapiga raia hovyo eti "kuwatia adabu".
Mheshimiwa Rais naomba nikueleze mambo yafuatayo:
1. Mosi ni aibu kwa jeshi kuvunja sheria, na kukiuka misingi ya kisheria ya uanzishwaji wake.
Katika nchi yoyote, majeshi yanapaswa kuwa ni vyombo vya kinidhamu, mfano bora kwa wananchi na taswira chanya ya kuonyesha namna gani sheria zinavyopaswa kutiiwa. Kitendo cha Wanajeshi kuvunja sheria waziwazi , kinaidhalilisha serikali yako, na kimsingi kinakudhalilisha wewe Amiri jeshi mkuu ambaye leo hii vijana wako wanaingia mitaani na kubehave kama watu wa fujofujo, badala ya watu sober wenye nidhamu ya hali ya juu.
2. Pili, wanajeshi wanaoact kwa utaratibu huu wanaonyesha udhaifu badala ya nguvu, hawatufai, wachukuliwe hatua kali za kinidhamu
Mheshimiwa Rais, nguvu ya jeshi wala siyo uwezo wake wa kupita mitaani na kupiga wanawake,, watoto, wazee na vijana. Bali uwezo wa jeshi unapimwa kwa namna gani unatii katiba ya nchi, mipango madhubuti ya ulinzi wa Taifa na medani. Kama Jeshi la Wananchi linadhani liko Juu ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajindanganya sana. Legitimacy yake kwa umma siyo uwezo wa kufanya vurugu mitaani, bali legitimacy yake na heshima yake itapatikana kwa kulinda uhuru wa Taifa letu na kuwa nguzo ya usitawi, na siyo kufanyafanya fujo mitaani.
3. Mheshimiwa Rais, Hata sisi raia ni jeshi la akiba
Kitendo cha watu wachache wenye uniform kuingia mitaani na kupigapiga watu kimsingi ni kama jeshi kupigana na wenzao tu ambao hawana uniform. Pengine wanajeshi wetu, ambao wewe ni Amiri jeshi mkuu wake inapaswa waelewe kuwa, Uniform hizo wanazovaa ni kwa ridhaa yetu, kwamba tumeamua wachache wawe mbele kwenye ulinzi wa Taifa lakini Pindi Taifa likihitaji ulinzi, sisi sote tutakuja front kulilinda. Sasa kitendo cha wachache walio katika uniform kuingia mitaani na kufanyafanya vurugu, ni kitendo cha aibu, kisichovumilika na cha kukemewa na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa hili.
4. Mheshimiwa Rais, tukilea tabia hizi za hovyo za baadhi ya wanajeshi kupiga na kuonea raia, ipo siku watafanya tukio kubwa zaidi.
Mheshimiwa rais, mwanzo wa ngoma ni lele, na samaki mkunje angali mbichi. Leo hii tukivumilia vitendo vibaya kabisa visivyo na heshima wala Taswira ya jeshi la Wananchi tunalolijua, ipo siku watafanya jambo baya kabisa katika nchi na kutishia amani na utulivu wa Taifa zima. Ni lazima hatua kali zichukuliwe kwa hawa wachache waiojua nini maadili ya kazi yao ili kulinusuru Taifa dhidi ya wanajeshi wenye mentality za vuruguvurugu kama hawa wanaopita mitaani na kufanya fujo.
Mheshimwa wanajeshi hawa wachache wenye kufanya matendo haya ya kihuni siyo aina ya wanajeshi ambao baba wa Taifa alijivunia kuwa tuna JESHI LA WANANCHI. Tunaomba wahusika wote waliohusika wachukuliwe hatua kali kabisa za kisheria na kinidhamu.
5. Mheshimiwa Rais hatuwezi kuvumilia Panya Road wa Kiraia, na kamwe hatuwezi kuvumilia panyaroad wa Kijeshi.
Matendo wanayofanya hawa wanajeshi wachache wasio na nidhamu hayana tofauti na matendo wanayofanya vijana wachache wa kiraia wasio na nidhamu waitwao Panyaroad. Hivi inawezekanaje mwanajeshi unaingia mtaani na kuanza kupigapiga klla mtu apitaye. Sasa unataka kuachieve nini?. Kwamba unataka raia wakuogope?, ili iweje na kwa nini?. Mheshimiwa Rais, ili jeshi lifanikiwe linahitaji mgongo wa Raia. Ni mentality potofu kudhani eti Jeshi liko juu ya raia na kwa hivyo wanajeshi wanaweza kupiga, kujeruhi, kuvunjia heshima watu eti kwa sababu ni wanajeshi. Hili tumelikataa na tunalikataa kwa moyo wetu wote. Tunataka Jeshi liendelee kuwa na sifa ya nidhamu na yeyote atakayejiinua ndani ya majeshi yetu na kujifanya panya road wa kijeshi huyo hatufai, avue uniform aingie mtaani akafanya mambo yake huko akakumbane na mkono wa sheria!
Mwisho namalizia kwa kusema kuwa, nina Imani na Mkuu wa Majeshi, nina imani na Mnadhimu wa majeshi na bado nina imani na Jeshi kiujumla. lakini matendo haya yaliyotokea Kawe yamelitia doa jeshi na ni lazima lichukue hatua. Tunahitaji heshima ya jeshi letu iendelee kuwa palepale, na siyo kuwa na vikundi vya reactionaries, wapenda fujo ndani ya komandi, wanaodhani eti kufanya "zali" au "kulianzisha" ndiyo ukamanda wenyewe. Huo siyo ukamanda, bali ni uhalifu. Hao waliohusika wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria mara moja ili tabia hizi za kupigapiga wanachi zikome mara moja, hazikubaliki hata kidogo!
Kwan mpaka sasa wako huko Kawe wakiendeleza kipigo?Mkuu acha kuidanganya saikolojia yako.
Mimi sina imani na mkuu wa majeshi, kwa sababu baada ya kusikia haya angeshaamuru vijana wake warudi kambini. Ikumbukwe makazi ya CDF ni pale pale Lugalo.
Tufike mahala hawa watu wabebe dhamana ya utendaji wa watu wao
Huwez kuwa mwanajeshi ww ila una ndoto za kuwa mwanajeshi, ww ni mvuta bangi mmoja anayemtegemea dada yake amfurahishe shemeji Yako ndio upate kula chakulaTutazidi kutembeza kichapo kama huwezi ishi kwa nidhamu karibu na utawala zetu nenda kaishi uswahilini, maswala ya ugomvi wa ovyo hatutaki mtakaribisha magaidi wafanye icho mnachokiona ni haki yenu kujibishana na mwanajeshi , leo jumapili mpo nyumbani wote tunakuja tembez rungu kuanzia watoto baba hausigeli adi mifugo na panya wote wa ndani
[emoji23][emoji23]Tutazidi kutembeza kichapo kama huwezi ishi kwa nidhamu karibu na utawala zetu nenda kaishi uswahilini, maswala ya ugomvi wa ovyo hatutaki mtakaribisha magaidi wafanye icho mnachokiona ni haki yenu kujibishana na mwanajeshi , leo jumapili mpo nyumbani wote tunakuja tembez rungu kuanzia watoto baba hausigeli adi mifugo na panya wote wa ndani
Kwani walipewa ratiba ya kupiga na wakaikiuka?Kwan mpaka sasa wako huko Kawe wakiendeleza kipigo?
Mwenye jeshi lake ni raia, acha kuandika kama vidole havishirikiani na kichwa.Kumuua kanali wa jeshi ni kulitukana jeshi
Kinachofanyika ni kuludisha nidhamu mtaani,zinapigwa virungu adi nzi
Iyo ni oda Toka kwa cdf,ukiona wazee wamezama jua mwenye jeshi lake kajaa sumu,anatamani kutandaza bakora hata kwa raia ote tz
Uhuru ukizidi huzaa ujinga kwenye jamii, demokrasia ikizidi huzaa masuala ya kuchukuliana poa mpaka inapitiliza.Hawa jamaa mbona mtaani tunaishi nao vizuri, shida ni pale mnapotaka kuwahujum lazima wakiwashe
Wajifunze adabu, sio kila mtu unamchukulia poa tu kama vile yupo sawa na abiria anayekulipa shilingi mia saba kwa safari moja unayomsafirisha.Acha kutetea ujinga nchi hii in utawala wa Sheria. Mtuhumiwa wa mauaji kashakamatwa je hawa wanaopigwa Wana kos gani?
Raia ajifunze adabu pia, mwanajeshi analinda mipaka ya nchi wakati raia anakoroma tu kitandani kwake.Mwenye jeshi lake ni raia, acha kuandika kama vidole havishirikiani na kichwa.
Unaowaona wapumbavu ndio wanakulinda usiku huko mipakani mpaka unalala usingizi mzito usiku kucha.Ndio madhara ya kuwa na jeshi la watu wapumbavu ,wasi na elimu , exposure ,akili wala maadili
Vyombo vyote vya dola Tanzania vina ajiri Kwa misingi hiyo , unatarajia kuwa na jeshi la watu gani kama sio vikundi vya wahuni wanaovaa sare za jeshi la kulipwa pesa za walipa kodi watanzania kuwafanyia unyama raia ?
Nani yupo juu ya sheria katika hii nchi?Wajifunze adabu, sio kila mtu unamchukulia poa tu kama vile yupo sawa na abiria anayekulipa shilingi mia saba kwa safari moja unayomsafirisha.