Rais Samia Wachukulie hatua wanajeshi wanaofanyafanya vurugu mitaani-Hii ni aibu isiyokubalika hata kidogo!

Rais Samia Wachukulie hatua wanajeshi wanaofanyafanya vurugu mitaani-Hii ni aibu isiyokubalika hata kidogo!

Soma taratibu kilichoandikwa, acha kuleta mihemuko.
huwezi kutetea kibaka/vibaka nikakuelewa, huyo boda/bajaji ni kibaka kama kibaka mwingine yoyote, alifaa kuvisha tairi na kupigwa kiberit hapo hapo.
 
huwezi kutetea kibaka/vibaka nikakuelewa, huyo boda/bajaji ni kibaka kama kibaka mwingine yoyote, alifaa kuvisha tairi na kupigwa kiberit hapo hapo.
Mimi sijatetea kibaka, napingana na wanajeshi kupiga raia bila sababu za msingi.
 
Mimi sijatetea kibaka, napingana na wanajeshi kupiga raia bila sababu za msingi.
mkuu kuna utetezi ulifanya, ulifika mpaka kusema kuwa huyo kibaka alitakiwa amwamrishe mjeshi kutoa gari na si kumuomba, na ukasema wanaishi kwa kodi zetu, hata watumishi wengine wa umma wanaishi kwa kodi zetu pia, ila nao wanalipa kodi hvo wana haki ya kutumia miundo mbinu kama raia mwingine yoyote, hao watu kupigwa ni haki yao kabisa, hao watu wazima waliopigwa lazima walikuwa wanawatetea hao vibaka boda/bajaji, nimeshuhudia magari mawili yanachomwa moto mwanza na hao boda kisa mwenzao kagongwa tena kwa uzembe wake,(kona ya bwiru na nyegezi) hao bado walishamuua ndugu mmoja wa arusha maeneo ya tegeta kisa jamaa alimgonga boda mwenzao, ningekuwa rais ningeamuru adhabu ya viboko 20 hadharani kwa boda wanaofanya makosa barabarani uone kama hawajakoma, hakuna watu wanapewa elimu ya barabarani kama boda/bajaji ila hawasikii, suluhisho kwa hao vibaka ni fimbo tu,
 
Ni typing error
hakuna cha typing error hapo, hujui tofauti ya sharia na sheria, hata hayo maneno typing error hujui maana yake pia, huwezi kuandika neno lenye maana sahihi ukasema ni typing error mkuu, shida yako we ni zao la shule za kata, hapo ndo penye shida kubwa.
 
Salaamu kwako Mheshimiwa Rais

Mheshimiwa Rais, nianze kwa kusema kuwa mimi raia wa Tanzania, nina heshima kubwa kwa Jeshi letu la wananchi. Kazi waliyoifanya kwa miaka zaidi ya 60 ya ulinzi wa Taifa letu ni njema sana, kwa kweli imekuwa msingi na nguzo kuu ya amani na utulivu wa wa Taifa letu

Hata hivyo, Hivi karibuni zimezuka taarifa za wanajeshi wachache, wasiojua miiko na viapo vya kazi yao, wameamua kuvunja sheria na kuingia mtaani na kuanza kupigapiga watu hovyo.
Tukio hili limetokea baada ya kutokea taarifa za kuuawa kwa mwanajeshi na mwananchi baada ya kinachosemekana ugomvi wa raia na mwanajeshi huyo. Baada ya tukio hilo kundi la wanajeshi limeingia mitaani na kuanza kupigapiga raia hovyo eti "kuwatia adabu".

Mheshimiwa Rais naomba nikueleze mambo yafuatayo:

1. Mosi ni aibu kwa jeshi kuvunja sheria, na kukiuka misingi ya kisheria ya uanzishwaji wake.
Katika nchi yoyote, majeshi yanapaswa kuwa ni vyombo vya kinidhamu, mfano bora kwa wananchi na taswira chanya ya kuonyesha namna gani sheria zinavyopaswa kutiiwa. Kitendo cha Wanajeshi kuvunja sheria waziwazi , kinaidhalilisha serikali yako, na kimsingi kinakudhalilisha wewe Amiri jeshi mkuu ambaye leo hii vijana wako wanaingia mitaani na kubehave kama watu wa fujofujo, badala ya watu sober wenye nidhamu ya hali ya juu.

2. Pili, wanajeshi wanaoact kwa utaratibu huu wanaonyesha udhaifu badala ya nguvu, hawatufai, wachukuliwe hatua kali za kinidhamu

Mheshimiwa Rais, nguvu ya jeshi wala siyo uwezo wake wa kupita mitaani na kupiga wanawake,, watoto, wazee na vijana. Bali uwezo wa jeshi unapimwa kwa namna gani unatii katiba ya nchi, mipango madhubuti ya ulinzi wa Taifa na medani. Kama Jeshi la Wananchi linadhani liko Juu ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajindanganya sana. Legitimacy yake kwa umma siyo uwezo wa kufanya vurugu mitaani, bali legitimacy yake na heshima yake itapatikana kwa kulinda uhuru wa Taifa letu na kuwa nguzo ya usitawi, na siyo kufanyafanya fujo mitaani.

3. Mheshimiwa Rais, Hata sisi raia ni jeshi la akiba

Kitendo cha watu wachache wenye uniform kuingia mitaani na kupigapiga watu kimsingi ni kama jeshi kupigana na wenzao tu ambao hawana uniform. Pengine wanajeshi wetu, ambao wewe ni Amiri jeshi mkuu wake inapaswa waelewe kuwa, Uniform hizo wanazovaa ni kwa ridhaa yetu, kwamba tumeamua wachache wawe mbele kwenye ulinzi wa Taifa lakini Pindi Taifa likihitaji ulinzi, sisi sote tutakuja front kulilinda. Sasa kitendo cha wachache walio katika uniform kuingia mitaani na kufanyafanya vurugu, ni kitendo cha aibu, kisichovumilika na cha kukemewa na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa hili.

4. Mheshimiwa Rais, tukilea tabia hizi za hovyo za baadhi ya wanajeshi kupiga na kuonea raia, ipo siku watafanya tukio kubwa zaidi.

Mheshimiwa rais, mwanzo wa ngoma ni lele, na samaki mkunje angali mbichi. Leo hii tukivumilia vitendo vibaya kabisa visivyo na heshima wala Taswira ya jeshi la Wananchi tunalolijua, ipo siku watafanya jambo baya kabisa katika nchi na kutishia amani na utulivu wa Taifa zima. Ni lazima hatua kali zichukuliwe kwa hawa wachache waiojua nini maadili ya kazi yao ili kulinusuru Taifa dhidi ya wanajeshi wenye mentality za vuruguvurugu kama hawa wanaopita mitaani na kufanya fujo.
Mheshimwa wanajeshi hawa wachache wenye kufanya matendo haya ya kihuni siyo aina ya wanajeshi ambao baba wa Taifa alijivunia kuwa tuna JESHI LA WANANCHI. Tunaomba wahusika wote waliohusika wachukuliwe hatua kali kabisa za kisheria na kinidhamu.

5. Mheshimiwa Rais hatuwezi kuvumilia Panya Road wa Kiraia, na kamwe hatuwezi kuvumilia panyaroad wa Kijeshi.

Matendo wanayofanya hawa wanajeshi wachache wasio na nidhamu hayana tofauti na matendo wanayofanya vijana wachache wa kiraia wasio na nidhamu waitwao Panyaroad. Hivi inawezekanaje mwanajeshi unaingia mtaani na kuanza kupigapiga klla mtu apitaye. Sasa unataka kuachieve nini?. Kwamba unataka raia wakuogope?, ili iweje na kwa nini?. Mheshimiwa Rais, ili jeshi lifanikiwe linahitaji mgongo wa Raia. Ni mentality potofu kudhani eti Jeshi liko juu ya raia na kwa hivyo wanajeshi wanaweza kupiga, kujeruhi, kuvunjia heshima watu eti kwa sababu ni wanajeshi. Hili tumelikataa na tunalikataa kwa moyo wetu wote. Tunataka Jeshi liendelee kuwa na sifa ya nidhamu na yeyote atakayejiinua ndani ya majeshi yetu na kujifanya panya road wa kijeshi huyo hatufai, avue uniform aingie mtaani akafanya mambo yake huko akakumbane na mkono wa sheria!

Mwisho namalizia kwa kusema kuwa, nina Imani na Mkuu wa Majeshi, nina imani na Mnadhimu wa majeshi na bado nina imani na Jeshi kiujumla. lakini matendo haya yaliyotokea Kawe yamelitia doa jeshi na ni lazima lichukue hatua. Tunahitaji heshima ya jeshi letu iendelee kuwa palepale, na siyo kuwa na vikundi vya reactionaries, wapenda fujo ndani ya komandi, wanaodhani eti kufanya "zali" au "kulianzisha" ndiyo ukamanda wenyewe. Huo siyo ukamanda, bali ni uhalifu. Hao waliohusika wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria mara moja ili tabia hizi za kupigapiga wanachi zikome mara moja, hazikubaliki hata kidogo!
Umeandika vyema.

Binafsi hii tabia ya wanajeshi, askari, police officer kupiga/kupigana na mtu ni udhaifu mkubwa, ni ukosefu wa akili na kutokujua majukumu yake/vizuri.

Inawezekana Je mtu aliyefundishwa na ambaye kazi yake ni kusimamia kufuatwa kwa sheria yeye tena anakuwa anavunja sheria? Hii ni aibu kwetu wote tunaopenda kuona Tanzania ikifanya vizuri kwenye kila nyanja.

Nilishuhudia pia askari akiwa kwenye gari la serikali na kavaa uniform akimpiga kijana anayeendesha bajaji kwa kosa la kugonga gari lake ubavuni. Huyo askari alishuka kwenye gari na kuanza kumpiga dereva wa bajaji. Hata gari lake alikuwa hajaangalia kagongwa au la? Gari halikuguswa hata kidogo.

Tabia ya askari kujichukulia sheria mkononi ni yakukemewa.
 
Kumbe mnaonea raia kwa
Mwanajeshi huwezi kumfanya lolote, watu wakichoka ndio watajibu mapigo ya jeshi, wewe utakuwa unaota.

Sio watanzania hawa tunaowajua labda.
Kumbe mnaonea raia kwa upole wao.
What is important mnapaswa kujua hakuna aliye juu ya Sheria.
Pia jeshi liache kuajiri watu wajinga wasiojua hata utawala wa sheria ni kitu gani.
 
Kumbe mnaonea raia kwa
Kumbe mnaonea raia kwa upole wao.
What is important mnapaswa kujua hakuna aliye juu ya Sheria.
Pia jeshi liache kuajiri watu wajinga wasiojua hata utawala wa sheria ni kitu gani.
Kumchoma mtu bisibisi halafu ukachezea kichapo na kuja kulialia humu JF ni kupoteza muda tu. Nchi hii uhuru umekua mwingi mno kila mtu akishakuwa na simu ya mkononi ya kisasa kisha akajua kuitumia anajiona keshafika mawinguni.

Heshimu kila mtu huko njiani, sio kila mmoja unaweza kutunishiana nae msuli.
 
UN wanajeshi wa Tanzania tumewarudisha nyumbani Kwa kashfa ya NGONO, TZ,wanajeshi wametangaza kusaka chupi mitaani, Mabeyo apewa V8 iliaendelee Kula na wahuni wa CCM nimeandika haya ili muone kama mna walinzi au wahuniii !!haya ni matokeo ya nchi kuchagua viongozi na jeshi kwa njia za rushwa ,Mimi huku mitaani nawaambia kabisa nyinyi ni wasichana tu wanajeshi wapo Africa magharibi sio nyinyi .
209% correct
 
unawaita wanajeshi wanaokulinda usiku na mchana panya road? Naona wanajeshi wamekuwa wamekuwa wapole sana. Ngedere unayejjambia usiku hujui lolote kuhusu nchi hii unawaita wanajeshi panya road? Subiri utafikiwa we mbwa.
Unajua kitu kinaitwa Force Routine Order?
Unajua kitu kinaitwa Defenses Code of Service Discipline, ?
 
UN wanajeshi wa Tanzania tumewarudisha nyumbani Kwa kashfa ya NGONO, TZ,wanajeshi wametangaza kusaka chupi mitaani, Mabeyo apewa V8 iliaendelee Kula na wahuni wa CCM nimeandika haya ili muone kama mna walinzi au wahuniii !!haya ni matokeo ya nchi kuchagua viongozi na jeshi kwa njia za rushwa ,Mimi huku mitaani nawaambia kabisa nyinyi ni wasichana tu wanajeshi wapo Africa magharibi sio nyinyi .
Hii sikuwahi kuisikia ndio nasikia leo
 
Tutazidi kutembeza kichapo kama huwezi ishi kwa nidhamu karibu na utawala zetu nenda kaishi uswahilini, maswala ya ugomvi wa ovyo hatutaki mtakaribisha magaidi wafanye icho mnachokiona ni haki yenu kujibishana na mwanajeshi , leo jumapili mpo nyumbani wote tunakuja tembez rungu kuanzia watoto baba hausigeli adi mifugo na panya wote wa ndani
Military Code of Service Discipline, inakuruhusu kufanya hivi?
FRO Inakuruhusu kufanya hivi?
 
Police wameonyesha weledi kama wamegoma kumkabidhi huyo mtuhumiwa,
Kama vipi nendeni mkawapige police muone mtakavyofukuzwa Kazi
polis ni vibaka waliovaa uniform au hujui hilo? walifanya hvo kumlinda kibaka mwenzao, tulishawai wachakaza polis arusha mpaka wakachakaa, wakaenda kulia kwa rais ndo rais akatuomba tusiwe tunawachakaza.
 
1698770508270.jpeg
 
Back
Top Bottom