Rais Samia, Waeleze Watanzania ukweli juu ya ulichokikuta Hazina

Jamani hakukuta kitu pia hata kama hasemi. Kama kungekuwa na kitu wastaafu, wakandarasi wa ndani, suppliers, wanafunzi,walimu, wafanyakazi wangelipwa madeni Yao, kupandishwa vyeo na nyongeza za mishahara. Mifuko ya hifadhi ya taifa isingeporwa hela zao, beuros zisingeporwa, wafanyabiashara wasingeingiliwa accounts zao na kuporwa pesa zao, muhimbili isingeambiwa atoe gawio pia.

Namshauri Mama tena na tena aachane na baadhi ya miradi mikubwa kwa kuanzia na ujenzi wa Dodoma, vinginevyo 2025 itamkuta akiwa amesimama.

Asione haya kuzirejesha Dar es Salaam baadhi ya wizara, nyingine azipeleke Mwanza, Arusha, Morogoro, Tanga ili kuwasongezea karibu wananchi huruma badala ya kwenda kuzirundika zote Dodoma tena kama ilivyokuwa Dar es salaam.
 

FACT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…