Rais Samia: Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria

Rais Samia: Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Rais Samia ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Julai 13, 2026



"Kwa upande mwingine, mabadiliko ya sera za kiuchumi, matamko na mwelekeo wa kisiasa duniani unaziweka nchi zetu zinazoendelea katika hali ngumu ya ushindani na pengine kupigwa vita.

Tulishamshikia mtu mmoja mkubwa tu wa nchi moja, anasema, 'Sisi yeyote anayeendelea kimaendeleo kwa kasi, huyo ni adui yetu.' Kwa hiyo, jinsi nchi zetu hizi zinazoendelea tunavyokwenda mbele, wengine wanaangalia njia na mbinu za kutuvuta nyuma ili tusiende kwa kasi ile ambayo tunakusudia.

Tunashuhudia mataifa yakihujumiana. Tunashuhudia vijana kulaghaiwa na kumezeshwa sumu dhidi ya mataifa yao, na kushawishiwa kuhujumu uchumi zao zilizojengwa kwa nguvu kubwa.

Vilevile, kuna wimbi la kuwaaminisha vijana kwamba serikali zao, hasa za Afrika, hazifuati au zinakiuka haki za binadamu. Sasa hapa, nataka tuukumbushe tu ulimwengu, lakini na watu wetu wajue kwamba kwa upande wa Tanzania sisi ni wafuasi wazuri sana wa haki za binadamu.

Mtakumbuka kwamba sisi Tanzania tuliweka kwa mara ya kwanza kwenye katiba yetu ule mtiririko wa haki za binadamu pale tulipobadilisha sheria mwaka gani? 1988? 84? Eeh, tuliweka mtiririko wa haki za binadamu. Na tukatanua uwigo wa haki hizo.

Lakini pamoja na hayo, tumetunga sheria nyingine nyingi ambazo zimekwenda kulinda na kuweka nguvu ya utekeleza haki hizo za mwanadamu. Kubwa zaidi, tumetoa nafasi kubwa kwa wananchi wetu pale wanapohisi haki zao za binadamu zinavunjwa, watumie mahakama kwenda kudai au kutetea haki yao. Kwa hiyo, kwa upande wetu sisi Tanzania, kwa muda mrefu tunazo hizo haki za binadamu.

Sasa haya yanayosemwa na mengine yatakayoendelea kusemwa, sisi we know how best we are. Lakini hata ulimwengu unajua. Hata ulimwengu unajua sisi tuna uzuri gani au kiasi gani katika kuangalia haki za binadamu. Ila, wanasema 'give the dog a bad name' ili ufanyeje? Umuue. Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya. Basi jamii yote itamzunguka ifanyeje? Imuue. Kwa hiyo, lakini vyenginevyo sisi Tanzania tuko vizuri kwenye haki za binadamu.

Na uzuri ni kwamba, hakuna aliye juu ya sheria zetu zilizoweka hizo haki za binadamu—zilizowekwa kwa sheria—na sheria nyinginezo zote. Hakuna aliye juu ya sheria zetu. Anayevunja sheria, atashughulikiwa. Atashughulikiwa.

Kwa hiyo, kwa Tanzania sisi tuko vizuri. Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayevunja sheria, anashughulikiwa."
 
Rais Samia ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Julai 13, 2026

View attachment 3628048
Huyu bibi ni kichekesho yaani Lissu kudai chaguzi huru na haki ni kavunja shero hivyo ashughulikiwe?
Mbona Kizigha katapeli mabilioni badala ya kushughilikuwa kapewa kazi ikulu?
 
Hivi kupima hakuna mtu aliye juu ya Sheria kunapimwaje.

Lissu alisema "tutakinukisha" akafunguliwa kesi ya uhaini. Mwaipopo na wenzake wamesema watakata watu vichwa wapo uraiani. Hapo kuwa juu ya Sheria unakupimaje?
Acheni uongo,Lissu alisema atavuruga uchaguzi,atahamasisha uhasi na kukinukisha. Mnachagua maneno machache..ongeeni yote. Kwanini alipanga na kushawishi wahuni kuvuruga uchaguzi?
 
Acheni uongo,Lissu alisema atavuruga uchaguzi,atahamasisha uhasi na kukinukisha. Mnachagua maneno machache..ongeeni yote. Kwanini alipanga na kushawishi wahuni kuvuruga uchaguzi?
Bishweko kwa kabila letu ni mtu anayefanya ama amefanywa kinyume na maumbile . Au wakati mwingine inatumika kuonesha mtu mwenye disability ya reproductive organs. Samahani kwa hilo. Lakini nahisi you have one of those character
 
Back
Top Bottom