Rais Samia: Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria

Rais Samia: Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria

Rais Samia ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Julai 13, 2026

View attachment 3628048

"Kwa upande mwingine, mabadiliko ya sera za kiuchumi, matamko na mwelekeo wa kisiasa duniani unaziweka nchi zetu zinazoendelea katika hali ngumu ya ushindani na pengine kupigwa vita.

Tulishamshikia mtu mmoja mkubwa tu wa nchi moja, anasema, 'Sisi yeyote anayeendelea kimaendeleo kwa kasi, huyo ni adui yetu.' Kwa hiyo, jinsi nchi zetu hizi zinazoendelea tunavyokwenda mbele, wengine wanaangalia njia na mbinu za kutuvuta nyuma ili tusiende kwa kasi ile ambayo tunakusudia.

Tunashuhudia mataifa yakihujumiana. Tunashuhudia vijana kulaghaiwa na kumezeshwa sumu dhidi ya mataifa yao, na kushawishiwa kuhujumu uchumi zao zilizojengwa kwa nguvu kubwa.

Vilevile, kuna wimbi la kuwaaminisha vijana kwamba serikali zao, hasa za Afrika, hazifuati au zinakiuka haki za binadamu. Sasa hapa, nataka tuukumbushe tu ulimwengu, lakini na watu wetu wajue kwamba kwa upande wa Tanzania sisi ni wafuasi wazuri sana wa haki za binadamu.

Mtakumbuka kwamba sisi Tanzania tuliweka kwa mara ya kwanza kwenye katiba yetu ule mtiririko wa haki za binadamu pale tulipobadilisha sheria mwaka gani? 1988? 84? Eeh, tuliweka mtiririko wa haki za binadamu. Na tukatanua uwigo wa haki hizo.

Lakini pamoja na hayo, tumetunga sheria nyingine nyingi ambazo zimekwenda kulinda na kuweka nguvu ya utekeleza haki hizo za mwanadamu. Kubwa zaidi, tumetoa nafasi kubwa kwa wananchi wetu pale wanapohisi haki zao za binadamu zinavunjwa, watumie mahakama kwenda kudai au kutetea haki yao. Kwa hiyo, kwa upande wetu sisi Tanzania, kwa muda mrefu tunazo hizo haki za binadamu.

Sasa haya yanayosemwa na mengine yatakayoendelea kusemwa, sisi we know how best we are. Lakini hata ulimwengu unajua. Hata ulimwengu unajua sisi tuna uzuri gani au kiasi gani katika kuangalia haki za binadamu. Ila, wanasema 'give the dog a bad name' ili ufanyeje? Umuue. Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya. Basi jamii yote itamzunguka ifanyeje? Imuue. Kwa hiyo, lakini vyenginevyo sisi Tanzania tuko vizuri kwenye haki za binadamu.

Na uzuri ni kwamba, hakuna aliye juu ya sheria zetu zilizoweka hizo haki za binadamu—zilizowekwa kwa sheria—na sheria nyinginezo zote. Hakuna aliye juu ya sheria zetu. Anayevunja sheria, atashughulikiwa. Atashughulikiwa.

Kwa hiyo, kwa Tanzania sisi tuko vizuri. Waendelee kusema hakuna haki, tunavunja haki, lakini hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayevunja sheria, anashughulikiwa."
Abdul na Rostam azizi wapo chini ya sheria gani
 
Viongozi wangu wapendwa wa CHADEMA. Natumaini mmemsikia huyo zena alivyotoa uchafu mdomoni kuhusu haki, uongo kuhusu mataifa makubwa eti yanatuonea wivu na vijana kushawishiwa. Katoa uchafu tu. Lakini naamini uelewa wa watanzania bado ni mdogo sana. Maana waliaminishwa kuwa kiongozi ni mtakatifu hasemi uongo. Hili limama linaongea uongo mwanzo mwisho.
Viongozi please do a needful
 
Acheni uongo,Lissu alisema atavuruga uchaguzi,atahamasisha uhasi na kukinukisha. Mnachagua maneno machache..ongeeni yote. Kwanini alipanga na kushawishi wahuni kuvuruga uchaguzi?
Mbona mahakamani amewagaragaza! Hata sasa mnamshikilia gerezani kwa kosa gani? Mbona hizi hoja zenu zote mlizotumia kumshtaki mlishindwa kuzitetea kule mahakamani, ili mumtie hatiani?
 
Huyu hakuwa chaguo sahihi kwa nchi yetu. Baadhi ya mambo anayo yaongelea hata haieleweki anako yatoa
Safari hii kakaa na Kibudu Kalamaganda kuelezwa hayo ya sheria , haki n.k., lakini bado haelewi chochote katika hayo aliyoelezwa; kwa hiyo uwasilishaji wake ndio huo sasa unaoonekana hapa kama makande yaliyochanganywa na utumbo wa samaki na vichwa vya dagaa wa Kigoma.
 
Ni kweli mkuu, uelewa wa wengi wetu bado changamoto hasa vijijini, wanaamini kile wanachoambiwa kama kilivyo, exposure hakuna kwa wengi wetu.

Limama hili ni janga kwa kweli kwetu.
 
Hivi kupima hakuna mtu aliye juu ya Sheria kunapimwaje.

Lissu alisema "tutakinukisha" akafunguliwa kesi ya uhaini. Mwaipopo na wenzake wamesema watakata watu vichwa wapo uraiani. Hapo kuwa juu ya Sheria unakupimaje?

LISSU alichosema kimekuwa watu wamekufa 500+

Tuje kwa Shekhe Mwaipopo wamekufa wangapi wamechinjwa wangapi???

Akili zimemezwa na PEPO chafu la chuki 👈
 
LISSU alichosema kimekuwa watu wamekufa 500+

Tuje kwa Shekhe Mwaipopo wamekufa wangapi wamechinjwa wangapi???

Akili zimemezwa na PEPO chafu la chuki 👈
Lissu ndio aliua watu? Wacha uongo.
 
Lissu ndio aliua watu? Wacha uongo.

Azimio lake Lissu ndio chanzo cha vijana kutaka kuzuiya Uchaguzi!!
No Reform No Election✍️

Kauli ilitoka kwenye mdomo mkubwa wa Lissu👈

Tukumbuke pia ule mdomo ndio chanzo cha Ulemavu wake 👈

Vijana wenye kumfata alichosema wakataka kutafsiri kivitendo kwa kuzuiya Uchaguzi✍️
 
Acheni uongo,Lissu alisema atavuruga uchaguzi,atahamasisha uhasi na kukinukisha. Mnachagua maneno machache..ongeeni yote. Kwanini alipanga na kushawishi wahuni kuvuruga uchaguzi?
Yaani mtu akae ndani miezi mitano kabla uchaguzi, na bado chama chake kimezuiwa kufanya siasi watu wamtii? Kama waliweza kumtii kwa muda wote huo, basi ndio anayekubalika na wananchi, na nyie mko madarakani kwa mabavu.
 
Ukisikia kupatwa kwa uongozi, ndo huku.
Giza totoro

Kwako tu👈

lkn sio Serikali ya Tanzania

mana Serikali imepata kiongozi wa ndoto kubwa👈

kwani kaitoa nchi kwenye Pato la Taifa TRA kutoka Trilioni 17

Mpaka leo tupo Kwenye Trilioni 37 Ongezeko la Trilioni 20 ndani ya miaka 5 tu Imagine✍️

Nyinyi mnaongozwa na chuki 👈
Kumchukia kiongozi

lkn sio mitazamo ya kiuchumi na Maendeleo makubwa ya Ujenzi wa kitaifa 👈

Chuki zenu kwa namma RAIS anapiga kazi kwasasa tunaziona ni Pepo chafu mbele ya jamii ya Watanzania✍️
 
Azimio lake Lissu ndio chanzo cha vijana kutaka kuzuiya Uchaguzi!!
No Reform No Election✍️

Kauli ilitoka kwenye mdomo mkubwa wa Lissu👈

Tukumbuke pia ule mdomo ndio chanzo cha Ulemavu wake 👈

Vijana wenye kumfata alichosema wakataka kutafsiri kivitendo kwa kuzuiya Uchaguzi✍️
Na nyie hamkutaka uchaguzi uzuiwe ili mkae madarakani kwa kupika idadi ya kura.
 
Mwanamke ni Mwanamke tu! Hawezi kujizuia kuropoka!/kama anasuta vile!

Hana hata mshauri mmoja wa mambo ya diplomasia!
Nenda wewe kamshauri sasa acha kubweka kama jibwa koko.
 
huyo na Tundu Lisu inaelekea kabisa kwamba wana ugomvi binafsi, kwa maana kuna kila dalili ya kukomeshana ...
 
Back
Top Bottom