Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaa kwa kutulia mkuu[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Nchi ngumu sana hii.Ndio maanaNSSF na PPF wanashindwa kulipa mafao ya wastaafu kwa uwekezaji wa aina hii!
Juzi waziri wa fedha anasema Mama amesikia kilio cha wastaafu - suluhu nikuwekeza katika hati fungani za serikali!
Yaani serikali imekopa fedha za mifuko, imeshindwa kulipa halafu unageuza madeni hayo kuwa hati fungani (deni la aina nyingine kwa serikali) Tena anasema zitaanza kuiva baada ya miaka miwili, So wastaafu hakuna kulipwa hadi miaka 2!
Ushuari wangu, wabunge wakimaliza kipindi cha miaka mitano, hayo mafao yao yageuzwe kuwa hati fungani kama kweli hiyo ni lugha nzuri.
Hata kujenga Majengo sio biashara endelevu. Wizi mtupu. Kuna majengo mengi yako wazi hayana wapangajiHapo awali NSSF na PPF walijikita kujenga majengo na kuyapangisha.
Lakini rais Magufuli mwendazake aliwataka kujikita kujenga viwanda. Matokeo yake ndiyo haya hapa.
Ni mbaya sana na dhulma kubwa kwa wastaafu kuteseka kwa kutolipwa mafao yao kwa wakati, huku wanaoziongoza NSSF na PPF wananeemeka na kushiba.Hata kujenga Majengo sio biashara endelevu. Wizi mtupu. Kuna majengo mengi yako wazi hayana wapangaji
Msukuma mara nyngi huwa anasema ukweli.Kuna kitu huaga sikielewi kabisa, labda na mimi ningekua serikalini huenda ningebweteka hivo. Azania bank inamilikiwa kwa sehemu kubwa na mashirika ya hfadhi ya jamii, NSSF na PPF.
Kiwanda cha sukari (bila kujali kwamba yalikua matamko ya kisiasa au laa) kinamilikiwa na NSSF na PPF, zile ni pesa za NSSF na PPF na hao hao ndio wenye Azania bank, so wanaacha tu kiwanda kife and hence pesa zao zipotee hivi hivi tu kwasababu mwanzilishi wa wazo la kiwanda hicho kafariki?
Msukuma akiwadharau Wasomi anakua kakosea wapi? Anyway, kama match ya Yanga na Simba iliahirishwa kwasababu za matajiri, matajiri hao hao hawawezi kushindwa kuzuia sukari isitengenezwe Tanzania. RIP Magufuli
Sana.
Kitila anakwenda kukagua kiwanda cha Bakhresa Bagamoyo, wakati cha kwao kinaoza.
Ndio maanaNSSF na PPF wanashindwa kulipa mafao ya wastaafu kwa uwekezaji wa aina hii!
Juzi waziri wa fedha anasema Mama amesikia kilio cha wastaafu - suluhu nikuwekeza katika hati fungani za serikali!
Yaani serikali imekopa fedha za mifuko, imeshindwa kulipa halafu unageuza madeni hayo kuwa hati fungani (deni la aina nyingine kwa serikali) Tena anasema zitaanza kuiva baada ya miaka miwili, So wastaafu hakuna kulipwa hadi miaka 2!
Ushuari wangu, wabunge wakimaliza kipindi cha miaka mitano, hayo mafao yao yageuzwe kuwa hati fungani kama kweli hiyo ni lugha nzuri.
Yaaani umemaliza kila kitu hapa. Mtu ambaye yeye hela haimuumi mshahara wake upo pale pale hakuna siku akafanya biashara yenye tijaKila siku nawaambia mtu anaepokea salary yuko kwenye comfort zone hawezi kuja na biashara ikatoa tija,never ever
Yalikuwa maamuzi ya kukurupuka na ya kisiasa sana.Yaani, inasikitisha sana na kiwanda kilianzishwa kisiasa zaidi, kwa kuchukua pesa za mifuko ya pensheni za wazee wetu bila plani makini za uwekezaji, sasa mwisho imekuwa vilio na kusaga meno... kaaazi kwelikweli.
Mwanasiasa ndio alaumiwe. Unataka tulaumu mtaalamu, ungekuwa wewe ungekubali mwili wako kuokotwa kwenye gunia ufukweni?Toka awali walisaini mkataba wa kukopesha hao wakulima. Hakuna asiyefahamu kuwa mambo mengi yalifanywa kwa shinikizo la kisiasa.
Sasa nani alaumiwe, mwanasiasa au mtaalamu anayemsujudia mwanasiasa?
Mkuu hii ni awamu ya 6,awamu inayoijenga nchi kwa msingi wa kisheria na vema tukamsaidia Rais ili tuende mbele na hatuwezi kila kitu tukasukumia kwake pekee.Kiwanda kilianzishwa kwa matamko ya Rais mwendazake, thats why tunaiambia Ikulu ichukue maamuzi.
Ndio maana tunahitaji TAASISI imara sio kuwa na super PresidentKama kiwanda kilianzishwa kwa tamko la Ikulu na Rais ana wasaidizi ambao wanaonekana hawana msaada kwanini asiingilie ?
Hio ndio gharama ya kuwa Supreme Leader.
Sawa,Mkuu hii ni awamu ya 6,awamu inayoijenga nchi kwa msingi wa kisheria na vema tukamsaidia Rais ili tuende mbele na hatuwezi kila kitu tukasukumia kwake pekee.
Hupo sawa lakini haupo sahihi.Hivi Mama mnamuona mwepesiiii, mbona 2020 june kama hii HAMKUTISHIA.
Halafu ile janja ya hapo ya viongozi kujimilikisha vitalu na kuvikodi na mengine msifikiri havijulikani, tunalima nyanya na tunaripoti pia.
Kama kuna kidume aende akabomoe.
Mama hafanyikazi kwa VITISHO bora mungitumia lugha nyingine.
Full stop. Tukutane Dakawa mnadani kuchoma mbuzi