Rais Samia: Wakurugenzi (DEDs) muda wenu wa uangalizi (probation) unaisha 18/02/2022 baada ya hapo tutaamua nani abaki nani aondoke

Rais Samia: Wakurugenzi (DEDs) muda wenu wa uangalizi (probation) unaisha 18/02/2022 baada ya hapo tutaamua nani abaki nani aondoke

Wakurugenzi wangetokea halmashauri husika
Ifike mahali viongozi ngazi wilaya wote watokane uchaguzi wa wananchi ili wakiboronga wanachi wawajibishe. Haya mambo teuzi yamejaa fitna, kujipendekeza, ubabe, upendeleo na upambe. Kuna hitaji la katiba bora na sio bora katiba.
 
Itavunja umoja wa kitaifa na kuleta ukabila
Kivipi?Sema itavunja umoja wa kiCCM,mbona wakati ule walipokuwa wakitesa kwa zamu hamkusema huo ukabila?
Nafasi za kiutendaji kama DEDs zingekuwa za kuomba kazi kwa kuzingatia weledi na siyo siasa uchwara za ukada.
 
Kama umejisevia vijisenti hapa lazima Pressure ikupande...
 
Mkuu kaa karibu na wanasaikolojia ,at any time you gonna hang yourself.!!
Wanaoenda kuhang themselves ni Watanzania baada ya Rais wao kuhamasisha ufisadi waziwazi bila hata aibu wala soni usoni tena kupitia TV ya Taifa🐒🐒🐒
 
Shida ni kwamba wanatumbuliwa kisha wengine wanarudi tamisemi au ofisi ya Ras kusoma magazeti huku mishahara ikisoma kama kawa.

Inapaswa wote wenye tuhuma za wizi..uhujumu na ufisadi wa uchumi na miradi ya wananchi wafunguliwe kesi..wachunguzwe na pccb.

Tofauti na hapo ni kuwadanganya watanganyika..serikali ya kifisadi..wizi na utapeli tu dhidi ya walipakodi wa nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kivipi?Sema itavunja umoja wa kiCCM,mbona wakati ule walipokuwa wakitesa kwa zamu hamkusema huo ukabila?
Nafasi za kiutendaji kama DEDs zingekuwa za kuomba kazi kwa kuzingatia weledi na siyo siasa uchwara za ukada.
Nimejibu kulingana na swali. Wewe umeniuliza ambacho sijakijibu
 
Bora angefanyia kazi kimya kimya maana kuanzia hapo wataanza kupishana kwa kalumanzira!
Kalumanzira yeye ale wapi? Kutamka kwake wanaojijua ni under performers watajipa saa za fungulia mbwa.
 
Anaenda vizuri, itakuwa wale watoto aliowapa kazi ameshaona hawaimudu, vile visichana vidogo aliambiwa havitamudu hayo majukumu akawa mgumu kuelewa.
Na vingi viko likizo ya uzazi.
 
Wengine elimu zao za kuungaunga tu form four failures Eti anakuwa kiongozi wa watu kwa ngazi ya Wilaya au Halmashauri na kuendelea [emoji848][emoji848]

Hata uwezo wa kujenga, kujadili au kupangua hoja hana.

Uwezo wa kuongea mbele za watu hawanaga!

Kinachosukuma kufanya lobbying ni njaa na wala siyo uwezo wa kufanya kazi yenye kuleta matokeo dhahiri yenye tija.
Kwa siasa zetu hizi za kinafiki hata mtu mwenye digrii 8, huwezi kumtofautisha na std 7 b!!elimu kwetu sio hoja, jpm aliingia na staili ya kuteua ma prof, walimsaidia nini?si kila siku alikuwa anawatimua tu!!
 
Ateue malaika wa mbinguni waje kuwa wakurugenzi kama anataka wakamilifu maana hata yeye kiutendaji hana lolote analofanya zaidi ya kurembua tu
 
Ni wakati muafaka sasa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, na Majiji waanze kupatikana kwa kuomba nafasi hizo. Watume barua za maombi na kushindanishwa ili wapatikane watu wenye uwezo na weledi hasa.
Ndo mana tunataka katiba mpya
 
Rais Samia Hassan Suluhu amesema Wakurugenzi wa halmashauri walikuwa kwenye kipindi cha matazamio (probation) cha miezi sita ambayo inakamilika 18/02/2022.

Rais Samia amesema baada ya tarehe hiyo Waziri ataandaa performance report ya wakurugenzi wote ili ijulikane wanaobaki na wale watakaotumbuliwa wakaungane na wale wengine wanne waliotumbuliwa juzi.

Chanzo: TBC
Jicho langu linaona wateuliwa wakiwa wanajiandaa kumvamia waziri ili awapigie deki cv zao,
Kiufupi ugali wao kwa sasa anao waziri
 
Leo ni 23/02/2022,

Probation ilishaisha
 
Back
Top Bottom