Halafu zinalipwaje? Report za CAG hazikuona hilo? Tena Assad!!
Mkuu, mpaka kufikia hii posti yako, hakuna aliyekumbuka kuhusu CAG.
Hakuna sehemu tumesikia CAG kasema mashirika yalikopa ili kutoa gawio kwa serikali.
Mchechu, alilitia shirika hasara kwa kukopa na kujenga majengo yasiyonunulika, nyumba ya bei rahisi unasema unauza sh 170m? Dau na kina Zito, wamegawana NSSF na kutumia ovyo pesa hizo, shirika likawa hoi!
Tanesco, Makamba kaingia tu, wamesaini na kampuni ya kihindi kuweka mifumo ya kununua luku kwa $30m, sijui nani anajua kama imeshafanya kazi au ndo tushapigwa.
Jana wamesema watanunua 1.7MW za Pongwe kwa bilioni 7, ambapo ukilinganisha bwawa la Nyerere, ni sawa na kusema gharama za Makamba ni mara mbili zaidi kwa kila anachoibua sasa!
Mwisho, Tanesco walikuwa wanawalipa Symbion, IPTL, Aggreko, Songas, ALTMAS n.k kuzalisha umeme, hawa wote isipokuwa Songas, waliondolewa. IPP ilikuwa inachukua karibu 80% ya mapato ya shirika hili, sasa kama wameondolea hao, hii pesa ilibaki wapi? Hawawezi kutoa gawio hawa?
ATLC, ndege zimenunuliwa kwa pesa ya serikali, kirusi kilisababisha kusiwe na route za hapa na pale, na hii ni kwa dunia nzima. Leo ndege zinatumiwa vibaya mno, kuanzia mama mipasho mwenyewe mpaka mkata majani, na zimeanza hata kuchakaa. Vision yake ndo tunafaidi sasa, kwanini washindwe ilihali ndege zinaruka kila siku?
Mifuko ya jamii, inachukua fedha za watumishi, wanawekeza, hawawapi watumishi dividends, faida ya uwekezaji huo inaenda wapi?
TAWA, hawatumii gharama kuzalisha wanyama na wakati mwingine hata kuwalinda wao na mazingira yao, ila wanagawa vitalu vya uwindaji na kuuza uza tu mbuga, hii faida ni nani anachukua?
Hakuna huduma usiyolipia pale Immigration, ukisema uzalishaji zero unamaanisha nini?
Mambo ni mengi kweli kweli ila ndo lazima alipie gharama za kuwekwa kitini!