Rais Samia: Wakuu wa Mashirika walikuwa wanakopa fedha Benki ili walipe Gawio Serikalini kulinda vibarua vyao

Magu alibana mashirika yatoe gawio, mama anabana wananchi ndio wanatoa gawio kama tozo kwa serikali. Nini tofauti sasa.
 
Records ziko wapi? Unaweza tu kukopa hela Central bank bila ya records zozote mahali na jinsi ya kuzirudisha? Na kama ni kweli kwamba walikuwa wanakopa ktk central Bank ili kumfurahisha Magufuli, je raisi Magufuli angeweza kutoligundua/kuambiwa hilo? I mean, huyo mtu sijui tu kwa kweli kwa maana dah!
Dah Rais wangu, hakuna shirika la serikali litakopa bila izini ya wizara ya fedha na mipango. Yaani sijui kwa nini wanamchomekea vitu vya kumdhalilisha.
 
Kwamba Benki kuu itoe mabilioni kwa siri kati ya Mkurugenzi na gavana ama?

Kama hili linawezekana mbona ni zaidi ya hatari hii.

Naomba ufafanuzi maana mimi kama Mwananchi wa kawaida sijaelewa.
 
Kila siku tunamsunta na kumshushua mwendazake ili mradi tuwafurahishe wahisani wa ndani
 
Dah Rais wangu, hakuna shirika la serikali litakopa bila izini ya wizara ya fedha na mipango. Yaani sijui kwa nini wanamchomekea vitu vya kumdhalilisha.
Hajazalilishwa kuna jambo linarekebishwa. Unless mnataka lolote lisirekebishwe maana huwezi rekebisha bila kukosoa.
 
Sukuma gang.😆😆

Ukweli ni kwamba Jiwe alikuwa ni mzigo na ana roho ya uharibifu tuu.

Wapi kamtaja marehemu?
Marehemu hawezi kwepa sababu serikali yake ndiyo ilipokea gawio linalosemekana kuwa si halisi lakini hajashambuliwa yeye kama binadamu ni mashirika ya uma yamekosolewa ili marekebisho yafanyike. Tatizo ni wafanya ibada wanaomuabudu wasiopendezwa na ukosoaji wa aina yoyote unaohusisha serikali yake.
 
Kila siku tunamsunta na kumshushua mwendazake ili mradi tuwafurahishe wahisani wa ndani
Si kweli. JPM alipokuwa anarekebisha makosa ya waliopita hakuzungumza? Kwann hamtaki makosa yaliyofanywa na serikali yake yasahihishwe? Yanasahihishwa vp bila kuyakosoa? Unless ilikuwa serikali tukufu sana isiyo na makosa.
 
Hajazalilishwa kuna jambo linarekebishwa. Unless mnataka lolote lisirekebishwe maana huwezi rekebisha bila kukosoa.
Hivi shirika kama la MSD linaweza kwenda kukopa bank bila idhini ya wizara husika??? Hivi chuo kama UDSM kinaweza kwenda kukopa bank bila idhini ya wizara husika???? Na kumbuka hela zote zinaenda BOT.
 
Sawa kwani serikali kujua kuwa hilo shirika limekopa kunazuia nn shirika kutoa gawio lisilo halisi? Swali sahihi ni ni kweli mashirika yalikopa kipindi wanatoa gawio? Na makaratasi ya mkopo yalionyesha mkopo ni kwa ajili ya nn?

Binafsi hujawahi kukopa pesa ya biashara ila ulipoipata ukagawa kidogo kwenye kurepair nyumba yako? Makaratasi yataonyesha mkopo wa biashara ila sehemu ya hiyo fedha utakuwa umerekebisha nyumba si ndio?

Ishu hapa ni kwamba yale magawio hayakuwa halisi, na yaliwezekana sababu shirika husika lilikopa. Hii haimaanishi kwamba sababu zilizowekwa kwenye makaratasi ya ukopaji ni gawio.
 
Makosa yaendane na ushahidi,unakopa bilion 5 bila kugundulika!!? Haya tuseme wizara ilikua inatoa hiyo idhini je waziri wake wa fedha enzi JPM yupo cheo kipi kwa sasa na kwann kapanda juu zaidi badala ya kutumbuliwa kwa kuficha huo uozo?
Si kweli. JPM alipokuwa anarekebisha makosa ya waliopita hakuzungumza? Kwann hamtaki makosa yaliyofanywa na serikali yake yasahihishwe? Yanasahihishwa vp bila kuyakosoa? Unless ilikuwa serikali tukufu sana isiyo na makosa.
 
Huu ni upumbavu mwingine kama ule wa Makamba kwamba umeme unakatika sababu ya mitambo kutofanyiwa marekebisho
 
Mfano wako sio halisi. Mfano halisi ni huu una biashara umemuweka mtu akuuzie bidhaa zako kisha kila mwezi anakuletea hesabu za jumla na pesa tele. Huyo mtu aje akukope pesa kisha akulipe kama hesabu kamili za mwezi. Huku unamdai na bado anakulipa kama hesabu za biashara ya mwezi husika je hautamshtukia?
Sawa kwani serikali kujua kuwa hilo shirika limekopa kunazuia nn shirika kutoa gawio lisilo halisi? Swali sahihi ni ni kweli mashirika yalikopa kipindi wanatoa gawio? Na makaratasi ya mkopo yalionyesha mkopo ni kwa ajili ya nn?

Binafsi hujawahi kukopa pesa ya biashara ila ulipoipata ukagawa kidogo kwenye kurepair nyumba yako? Makaratasi yataonyesha mkopo wa biashara ila sehemu ya hiyo fedha utakuwa umerekebisha nyumba si ndio?

Ishu hapa ni kwamba yale magawio hayakuwa halisi, na yaliwezekana sababu shirika husika lilikopa. Hii haimaanishi kwamba sababu zilizowekwa kwenye makaratasi ya ukopaji ni gawio.
 
Makosa yaendane na ushahidi,unakopa bilion 5 bila kugundulika!!? Haya tuseme wizara ilikua inatoa hiyo idhini je waziri wake wa fedha enzi JPM yupo cheo kipi kwa sasa na kwann kapanda juu zaidi badala ya kutumbuliwa kwa kuficha huo uozo?
Hata Mwendazake alikuwa anajua kinacho endelea. Yalikuwaga maigizo
 
Dah Rais wangu, hakuna shirika la serikali litakopa bila izini ya wizara ya fedha na mipango. Yaani sijui kwa nini wanamchomekea vitu vya kumdhalilisha.
Mkuu kwa uelewa wangu ni kwamba ma meneja walikopa wao binafsi ama sikuelewa mimi!
 
Makosa yaendane na ushahidi,unakopa bilion 5 bila kugundulika!!? Haya tuseme wizara ilikua inatoa hiyo idhini je waziri wake wa fedha enzi JPM yupo cheo kipi kwa sasa na kwann kapanda juu zaidi badala ya kutumbuliwa kwa kuficha huo uozo?
Kabla ya utumbuaji lazima ufanye analysis.

Kuna wakati fulani nilipewa scenario ya Mrema na mhasibu fulani wa taasisi(Sina hakika na credibility ya nilichoambiwa). Mhasibu alishauri kuwa hizi pesa hazifai kutumika katika siasa sababu zina wamiliki wake ila Mrema akatoa direct order kuwa zitumike na ikawa hivyo. Baadae katika kutekebisha huwezi mtumbua mhasibu unless hana ushahidi kuwa alikuwa against hizo instructions au utumbuaji ufanyike kwa ajili ya manufaa ya kisiasa.

Kama palikuwa na direct instructions kutoka wizarani au serikali kuu na mkurugenzi alionyesha kuwa si sahihi ila akatii maelekezo anatumbuliwa kwann?

Kukopa sio uozo. Kutoa gawio kama kuna faida pia nibsahihi. Kukopa halafu ukatoa faida huku una hasara hapo ndipo tatizo lilipo.
 
Records ziko wapi? Unaweza tu kukopa hela Central bank bila ya records zozote mahali na jinsi ya kuzirudisha? Na kama ni kweli kwamba walikuwa wanakopa ktk central Bank ili kumfurahisha Magufuli, je raisi Magufuli angeweza kutoligundua/kuambiwa hilo? I mean, huyo mtu sijui tu kwa kweli kwa maana dah!
Alipokuwa makamo wa raisi alilijua hili, halafu hajamwambia bosi wake!?
Au anataka kusema makufuli alilijua hili ila nae alikuwa analinda kibarua chake?
 
Mfano wako sio halisi. Mfano halisi ni huu una biashara umemuweka mtu akuuzie bidhaa zako kisha kila mwezi anakuletea hesabu za jumla na pesa tele. Huyo mtu aje akukope pesa kisha akulipe kama hesabu kamili za mwezi. Huku unamdai na bado anakulipa kama hesabu za biashara ya mwezi husika je hautamshtukia?
Umejificha kwenye kichaka cha kushtukia unasahu kuwa shirika la uma linaweza kufanya kazi kwa maelekezo ya serikali kuu na pia shirika kukopa na kutoa gawio si tatizo.

Tatizo ni kutoa gawio huku una hasara. Na gawio ulilitoa kwa kutumia mkopo ambao huenda uliidhinishiwa kwa malengo mengine.
 
Back
Top Bottom