Rais Samia: Wakuu wa Mashirika walikuwa wanakopa fedha Benki ili walipe Gawio Serikalini kulinda vibarua vyao

Rais Samia: Wakuu wa Mashirika walikuwa wanakopa fedha Benki ili walipe Gawio Serikalini kulinda vibarua vyao

Halafu Magufuli asijue kama wamechukuwa hela ktk central Bank ? Raisi yuko karibu na Gavana wa Benki anakuwa briefed kila kinachoendelea, asiambiwe kama shirika xyz limekopa ?
Chukua mfano wa TTCL chini ya Waziri Kindamba. Wamewahi kutoo gawio la Tsh 2.1 Billion kwa Serikali mnamo Mei 2019.

Halafu July 2019 walikuwa wamepeleka maombi ya guarantee ya Serikali ili waruhusiwe kukopa Tsh 360 Bilion kwa ajili ya kuimarisha network yao. Na Magufuli alipokea kwa tafrija mubashara kwenye TV. This was sheer madness
 
Rais Samia amesema Mashirika ya Umma hayafanyi vizuri na kuna baadhi ya Viongozi wao walikuwa wanakopa fedha Benki ilu walipe Gawio serikalini kulinda vibarua vyao

Rais Samia amesema Mashirika ya Umma yote yataangaliwa upya

Source ITV
Makande ya mlenda tunalishwa
 
Ninachoangalia ni ufanisi tu,
Maendeleo yalionekana kipindi cha JPM ama hiki,
Maneno ama viswahili vyenye konakona nyingi havinisaidii hvy Sina umhimu navyo.
Huko mbeleni tutaelewa km tuko njia sahihi ama la.
 
Kwa lugha nyingine walikuwa wanajikopa wenyewe na kujilipa wenyewe kutuhadaa wanainchi?
Mungu anawaona mliotawala inchi hii.
 
Records ziko wapi? Unaweza tu kukopa hela Central bank bila ya records zozote mahali na jinsi ya kuzirudisha? Na kama ni kweli kwamba walikuwa wanakopa ktk central Bank ili kumfurahisha Magufuli, je raisi Magufuli angeweza kutoligundua/kuambiwa hilo? I mean, huyo mtu sijui tu kwa kweli kwa maana dah!
Mkuu hii nchi ni kutembea kwa taratibu, ukizidisha mwendo utaachwa siyo wewe kuwaacha, hao ni wanasiasa they use every is in front of him kufikia malengo yake.

Mfano angalia huko Kenya Ruto anavyobwabwaja kuhusu serikali utadhani siyo kiongozi mkubwa serikalini.
 
Ni wazi yeye ndio ameshindwa kua mkali katika kusimamia hayo mashirika kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kupelekea mashirika kuendeshwa kwa hasara ,Magufuli alikua mkali na alikua anajua in and out,yeye awe mkali hizo soga nyingine anazoleta mwisho wa siku wananchi hawatomuelewa
 
Inamaana hawastahili kutoa gawio kwa SERIKALI?
huu utaratibu wa gawio umeanzishwa lini na kwa Nini waliuanzisha wakijua they won't make it kufanya return?
Ulikuwepo ila sasa Jiwe si unamjua? Aliua uchumi then pesa watoe wapi?
 
Halafu Magufuli asijue kama wamechukuwa hela ktk central Bank ? Raisi yuko karibu na Gavana wa Benki anakuwa briefed kila kinachoendelea, asiambiwe kama shirika xyz limekopa ?
Hata akijua kwani wakichukua kwa mgongo wa biashara na kuzileta kwa njia ya gawia utajua?
 
Ni wazi yeye ndio ameshindwa kua mkali katika kusimamia hayo mashirika kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kupelekea mashirika kuendeshwa kwa hasara ,Magufuli alikua mkali na alikua anajua in and out,yeye awe mkali hizo soga nyingine anazoleta mwisho wa siku wananchi hawatomuelewa
Mbona saizi yanaleta faida? Umesikia kuna Mstaafu anashindwa kulipa?

Pia Rais alishasema watayafuta Yale ambayo ni mzigo Serikalini.
 
Halafu Magufuli asijue kama wamechukuwa hela ktk central Bank ? Raisi yuko karibu na Gavana wa Benki anakuwa briefed kila kinachoendelea, asiambiwe kama shirika xyz limekopa ?
Huwezi kuwa raisi bila kufanya siasa. Mtu anayefanya siasa ni mwanasiasa, JPM alikuwa raisi, lolote linawezekana.
 
Na wewe unaamini huu uongo ? ,CEO wa shirika la umma akope zaidi ya 1 billion aliweka Nini huko Bank Kama dhamana, na Jiwe asijue ? Na Kama kweli walikopa while shirika linapata loss pesa ya kulipa ilitoka wapi
Nakujibu hivi,kwani ukikopa kwamba unaenda ku invest then unaileta kama gawio huku deni la shirika likiongezeka na Jiwe akijua umekopa kwa ajili ya biashara then atafanyaje?
 
Siyo swala la kuabudu, ni logic ya kawaida tu, Central Bank hawafanyi kazi kienyeji kama ni kweli walikopa fedha kama hata hilo linawezekana sijui ni lazima raisi angejua!
Ndio, inawezekana pia walikopa kwa maagizo yake kwa sababu za kisiasa.
 
Back
Top Bottom