Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Aijue Tanzania vizuri,leo hii anataka kurudishia halmashauri suala la ajira za walimu,utadhani hajui kua wakurugenzi na maafisa mbalimbali wataomba rushwa mbalimbali kirahisi.
 
Acha hii usije mharibia na uwaziri wenyewe aukose. Siasa za nchi hii zina wenyewe.
 
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
Katiba yako wewe labda ni ya toka enzi za kinjeketile lakini kama ni hii ya wasakatonge anaweza kula mzigo kilaini
 
Chief Hangaya anawapa matumbo joto tu wapinzani wake, kwa hii miezi mingapi tu unamuona kabisa hadi nuru yake aliyokuwa nayo awali ishaanza kupotea.

Pole kwa kazi MAMA. [emoji484]
Mitano tena.
 
Safi sana mama kuwakata maini wapinzani wako ndani ya ccm!! Nia hiyooo hadharani mwenye kujinyonga mbona kamba zipo!!!! Tuambizane ukweli, ni nani Tanzania hii angepata fursa halafu akaiachia?? Amwachie nani kwa mfano?
 
Nchi hii hakuna mwanamke yeyote kutoka bara ambaye atakuja kupata nafasi ya urais hata awe jembe kiasi gani.

Kuzaliwa zanzibar ndio cv kali ya mwanamke yeyote.

Na hata kwa mwanaume pia ukizaliwa zanzibar una nafasi kubwa zaidi kuliko ukizaliwa tz bara
 
Yeye mwenyewe alikaa miaka 23.Msidanganyike Ikulu ni Paradiso ya duniani. Imagine kuwa number moja wa nchi.
Ni kweli ni paradiso ya duniani lakin yote ni ubatili tu hasa kama hukuipata kwa mapenzi, kwa haki ya KiMungu na kwa ukhalali wa kidunia. Unaweza ukawa namba moja nchini lakin ukawa unaishi kwa mateso, magonjwa na misongo ya mawazo kipindi chako chote. Hata utajiri kuna watu wanapata utajiri batili, mtaani tunaita pesa za mapaka...wanakuwa nazo lakini zinawatesa..
Lakini yote katika yote, vyote tulivyonavyo hapa duniani, hatuondoki na chochote; unatesa wenzako ili wewe uwe namba moja, unabambikia wenzako kesi za uongo ili wewe ukose upinzani, uipate paradiso ya dunia kiulaini kinyume na mapenzi ya Mungu, haki ya KiMungu na kinyume na taratibu za kisheria za nchi..ni laana tu unajitafutia sababu hakuna dhambi isiyolipwa duniani...HAKUNA
Ukipatacho kwa haki, hata kama kidogo, ndicho chenye neema na maana hapa duniani; batili, hata kama kwa wingi, ni laana kwako na kwamba batili huwa na malipizi yake, kama si leo dunian kesho akhera na kama si wewe utakayelipia kitalipia kizazi chako hadi cha nne.
 
Hawa watu ndio maana wanakufaga kibudu. Unahudhuria maadhimisho ya demokrasia gani unayo practice kama sio unafki mkubwa!

Huyo hata ma ccm wenzake wahawezi kukubali arudi madarakani.
CCM wanakuchukia ukiwa umeziba mianya yao ya upigaji lakini kama unakula nao wala hawana shida na wewe,wanakupitisha kwa kula zote za ndiyo nakwa kishindo
 
Hivi gazeti la Uhuru walitoa wapi zile NONDO kuwa kasema hana mpango wa kuwania urais 2025?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3]
Walitumia akili kubwa ili kupata jibu lenye uhakika kutoka kwa mhusika badala ya kuishi kwa mino g'ono tu.
 
Habari,

Muda mrefu nimekuwa nikitamani kuweka uzi hapa wa kumsifia dada huyu kwa uchapakazi wake mahiri na ufuatiliaji wa karibu katika utendaji wake ambao kusema ukweli ni wa kipekee sana.Baada ya kusikia minong'ono ya chini kuhusu mgombea mwanamke 2025 Nikakumbuka kwamba nilitamani kuweka uzi wa kuelezea kwa namna utendaji kazi wa Ummy Mwalimu ni wa kipekee,Ila kutokana na mambo kuwa mengi nilijikuta ninasahau,Lakini leo nimekumbuka baada ya kuona utabiri wa mgombea mwanamke 2025.

Ummy Ally Mwalimu ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama tawala cha kisiasa. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015.

Ummy Mwalimu ameshika nafasi mbalimbali katika ulingo wa siasa. Mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na mwaka 2014-2015 alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mwaka 2015 alikuwa Naibu waziri wa Sheria na katiba, mwaka 2014/5 alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mazingira na mwaka 2010-2014 alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Pia Ummy Mwalimu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili (2010 hadi 2015 na mwaka 2015 hadi 2020) kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi kupitia Viti Maalum kwa Wanawake.

Mwaka 2007-2015 Ummy alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga na mwaka 2008 hadi 2015 alikuwa mjumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) Tanga. Mwalimu ameshika nafasi nyingi za uongozi katika chama na serikali.

Nitarejea kuendelea
Mmeshaanza ujinga..
 
Huyo Ummy umempendea nini ..... kuchekacheka amma!!?
 
Back
Top Bottom