Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Nani kakuambia nchi hii kinachoamua nani awe rais ni sanduku la kura? Wapinzani wenyewe mara kadhaa wameshinda lakini wanapigwa pini. Uchaguzi wa kimagufuli ndio utakuwa fasheni kwa miaka kadhaa. Nani hapendi vya dezo?

,😂✍️
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu


Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Ana uhakika gani na maisha yake?
mimi naona asipopata msaada wa haraka.
hawezi kufika 2025 huyu.

kuna hati hati nchi ikaenda kwa VP
na itakuwa ni historia ambayo taifa itaweka.

marais wawili waliopokezana kufa na makamu zao kuchukua kijiti.

hii comments itakuja kufufuliwa kabla ya 2025.
 
. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015.

nakusahihisha kwamba wabunge wa viti maalumu hawachaguliwi bali wanateuliwa na NEC
 
Back
Top Bottom