Pre GE2025 Rais Samia: Wameishiwa Wanataka Kuharibu Amani Yetu,Tusikubali

Pre GE2025 Rais Samia: Wameishiwa Wanataka Kuharibu Amani Yetu,Tusikubali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Ujumbe umewafikia Chadema na Mabwana zao Mabeberu.👇👇

Ndugu zangu wananchi ili tuendelee kupata tunayoyapata haya miradi ya kila aina, vituo vya umeme na mambo mengine msiende kufanya makosa (kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Novemba 2024), kwanza dumisheni uhuru na utulivu katika wilaya yenu hii. Amani na utulivu ndiyo itakayowawezesha kufanya shughuli zenu za maendeleo, ndiyo itakayowawezesha muweze kwenda shambani kulima vizuri, kuvuna vizuri na kuja kuuza hapa (Kituo cha manunuzi ya mahindi cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)) kwa raha kabisa. Amani na utulivu ndiyo inayotufanya hata majumbani tucheke, tukae vizuri tuangalie michezo ya kwenye runinga, kukiharibika hayo yote hayapo.

Niombe sana, wale wanaokuja kuwashawishi kwa neno lolote lile kwa sababu yoyote ile kuharibu amani na utulivu wa eneo lenu msikubaliane nao, ninataka kuwaambia kuwa wameishiwa, hawana pa kupenya, wameshaona mbele mambo magumu kwao, sasa wanalolifanya ni kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu ili wananchi waishi kwa mashaka, muone nchi yenu siyo njema, ndiyo lengo lao, niwaombe sana msikubaliane nao"- Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hayo mbele ya wakazi wa Mbinga alipotembelea kituo cha manunuzi ya mahindi cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Matika Mbinga Mjini Mkoani Ruvuma, Jumatano tarehe 25 Septemba, 2024.


View: https://www.instagram.com/reel/DAVpMalondE/?igsh=MXcxdGRrcDB1cWhraQ==

My Take: Hakuna Kibaraka ataruhudiwa kuvuruga amani ya Nchi hii,wafikishieni ujumbe waliowatuma.
 
Wasiwafanye watu hatunazo hili la kuvuruga amani ni la Samia mwenyewe na chawa wake,watu wanatekwa wanapotezwa na kuuawa kama rais eti mpaka sasa hajui watu wanaowateka na kuwapoteza wananchi anao waongoza wakati anamiliki vyombo vya dola kila kona,anataka waathirika wakuuliwa na kupotezwa ndugu zao ndio walinde amani lakini yeye na chawa wake wanaowambia polisi wasiwatafute wanaopotezwa wao ni mwiko kulinda amani ya nchi yetu.
 
Nyie na Wao wote ni walewale..., Na nawaomba sana msitake kuharibu Amani yetu sisi Wananchi.....
 
Ujumbe umewafikia Chadema na Mabwana zao Mabeberu.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DAVpwRiiRww/?igsh=MmRmbmpld2Y4bXFs

View: https://www.instagram.com/reel/DAVpMalondE/?igsh=MXcxdGRrcDB1cWhraQ==

My Take: Hakuna Kibaraka ataruhudiwa kuvuruga amani ya Nchi hii,wafikishieni ujumbe waliowatuma.



Kwanini Mama watu wanatekwa na kuuliwa ! Yaani Chadema watu wao watekwe halafu wakilalamika makosa yao!. Mama alisema apewe ripoti haraka je kapewa au au tuletea uswahili na vijimaneno vya kizanzibari kila siku
 
Amani na utulivu itatuwezesha hata tuangalie 👇🐼

1000012721.jpg
 
Back
Top Bottom