Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jibu ni moja tu kuwa mkileta chokochoko mtawajibishwa bila hurumaHaki na uhuru ni lazima , asijione kama yeye ndio anazitoa hizo haki, yeye atapita tuu kama wengine, nchi itaendelea kuwepo na wala haitegemei hisani au huruma yake
Wewe endelea kuweweseka chumbani kwako huko huko.lakini ukitoka nje ni lazima utii sheria bila shuruti.ukileta ujuaji ni lazima udakwe na kutupwa ndaniJana ndiyo amethibitisha kwamba wale watekaji wana baraka zote kutoka kwake.
4Rs ya KONYO? Unahubiri amani nyuma umeficha Mapanga?
Hautaki kujifunza kutoka kwa mtangulizi wako ,kuna rais ambaye alikuwa na ulinzi wa hatari kuliko JIWE? Kiko wapi?
Watu wanalalamikia vyombo vyako vya ulinzi vinaua watu ,vinaumiza watu ,wewe unatela tantalila ,ungekuwa unataka kukomesha hayo matukio ungemfunga MAFWELE kiongozi wa wahalifu ,SATIVA amemtambua na kwa records zake huyo mtu hafai ,ameua watu sana MKIRU na ile report ya Azory angeitoa jina lake lisingekosekana.
Acheni Ujinga ,katiba haisemi mwananchi akitoa maoni ambayo serikali haiyapendi auawe!! Siyo lazima tuwe na mawazo yanayofanana ,mawazo mbadala ndiyo yanayoeleta maendeleo ,hao wanaosupport wananufaika so hawawezi kukupinga na ndiyo maana wametenegeza "whatsapp feki" wanayoita mipango ya chadema na wewe ukaikubali...Bibi Chura kiziwi unaingizwa CHAKA.
Wewe endelea kuweweseka chumbani kwako huko huko.lakini ukitoka nje ni lazima utii sheria bila shuruti.ukileta ujuaji ni lazima udakwe na kutupwa ndani
Mama ni msema kweliAysee... Ila mama anajua kuchamba jamani
Anaremba mwandiko kwa taarifa za misiba.Mara aandike hivi,mara vile kizuzuzu tu.
Mwamba anakwama aisee ni hatari kwa taifa kuwa na vijana kama hawaAnaremba mwandiko kwa taarifa za misiba.Mara aandike hivi,mara vile kizuzuzu tu.
Kaa kwa kutulia na acha kuwewesekaMwamba anakwama aisee ni hatari kwa taifa kuwa na vijana kama hawa
Sawa mkuuKaa kwa kutulia na acha kuweweseka
Mlizoea na kutaka kuiingiza nchi kwenye machafuko kwa uroho wenu wa madaraka .sasa mmepewa ujumbe kuwa msichezee amani ya Nchi hiiKwa kauli ya jana, pasi na shaka sasa imethibitika rasmi wauaji na watekaji ndio "wale watu wasiojulikana'
Lema alikuwa anamrushia mawe Mrisho Gambo akiwa ng'ambo, hahahahaha....., Shikamoo Mama Saa100.Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Samia Suluhu Hasssan,ameongea kwa uchungu sana,kwa maumivu makali sana na kwa hisia kali sana zilizogusa mioyo ya watu wengi sana. Pale alipoelezea juhudi zake kubwa za kuliunganisha Taifa na kuwaleta pamoja watanzania tangia pale alipokula kiapo cha Urais wa Taifa letu.
Ameeleza namna alivyokuja na 4R katika kujenga kuaminiana na kuliunganisha Taifa ambalo lilikuwa limegawanyika kutokana na itikadi za kisiasa ,mpaka kupelekea watu wengine kukimbia nchi.na hapa mnaweza kukumbuka Lissu na Lema walivyokimbilia uhamishoni.
Rais wetu mpendwa amesema ni katika hali hiyo aliamua kuja na mpango wa 4R ili watu wote tuishi kama Taifa na tujenge Taifa letu kwa pamoja.amesema lakini kwa bahati mbaya sana kuna watu wamesahau ni wapi tulikotoka,ni wapi na mangapi na magumu mangapi wameyapitia katika maisha yao.lakini leo wameyasahau yote na kuanza kuleta vurugu,lugha za kichochezi, uchonganishi,uzushi na uongo na kupanga mipango ovu.
Amesema hata hivyo haishangazi kwa sababu kuna watu wenyewe hawapendi kuishi katika amani au kuona Taifa na nchi ikiwa katika Amani.ndio maana watu wa aina yao muda wote wanataka mavurugu vurugu tu.amesema hata hivyo hata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria watakao jaribu kuchezea amani ya Taifa letu.Na kwamba 4R ni katika kutuungaisha na kutuleta pamoja watanzania na siyo kwa ajili ya kuvunja sheria .amesema sheria zipo palepale na zitatumika kama inavyotakiwa kwa mujibu wa katiba.
Nami Mwashambwa Lucas namuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu mpendwa.Embu fikiria ndugu zangu Mtu kama lissu hivi anaanzia wapi kumtukana,kumbagua ,kumtweza na kumtolea lugha za kumshushia heshima Mheshimiwa Rais wetu? Anaanzia wapi kumdharau Rais Samia ndugu zangu?anaanzia wapi kuona Rais Samia hafai? Anaanzia wapi kuona na kusema Rais Samia ni Dikteta? Lissu anawafahamu madikteta? Anawafahamu viongozi makatili?
Hivi Lissu angeanzia wapi kukanyaga katika ardhi ya Tanzania akiwa hai kama siyo Rais Samia? Angeanzia wapi kuja kupanda katika majukwaa yaliyo katika ardhi ya Tanzania na kutia matusi yake na bado akaachwa tu? Angeanzia wapi kuja hapa Nchini mpaka kupata nafasi ya kuchangiwa pesa za gari ikiwepo kutoka CCM? Angeanzia wapi Lissu kuja kuvuta oksijeni ya Tanzania? Angepata wapi nafasi ya kwenda hadi kusalimia ndugu zake kijijini kwake , kuhudhuria kanisani ,kuonana na rafiki zake ,kushiriki moja kwa moja mikutano ya chama chake?
Angepata wapi nafasi hiyo lissu kama siyo Mama yetu Mpendwa Rais Samia? Nani aliyemrejesha Nchini Kama siyo Rais Samia? Nani aliye mfuata hadi ulaya na kumhakikishia usalama akirejea Nchini kama siyo Rais Samia? Amesahau haya yote? Alikuwa na kesi ngapi mahakamani? Amefunguliwa kesi gani mahakamani wakati huu wa Rais Samia licha ya Lissu kutukana mimatusi yake na kutoa lugha zake za kibaguzi na kichochezi?
Kwanini anakosa shukurani na kutambua mchango na nguvu ya Rais Samia katika kuimarisha demokrasia, utulivu,amani na umoja wa kitaifa? Nani alimtembelea hospitalini kama siyo Rais Samia?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Leo amesahau kuwa ni mama Samia Rais wetu mpendwa ndiye amefanya arejea Nchini na kuishi kwa amani.Lema alikuwa anamrushia mawe Mrisho Gambo akiwa ng'ambo, hahahahaha....., Shikamoo Mama Saa100.