Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Samia Suluhu Hasssan,ameongea kwa uchungu sana,kwa maumivu makali sana na kwa hisia kali sana zilizogusa mioyo ya watu wengi sana. Pale alipoelezea juhudi zake kubwa za kuliunganisha Taifa na kuwaleta pamoja watanzania tangia pale alipokula kiapo cha Urais wa Taifa letu.
Ameeleza namna alivyokuja na 4R katika kujenga kuaminiana na kuliunganisha Taifa ambalo lilikuwa limegawanyika kutokana na itikadi za kisiasa ,mpaka kupelekea watu wengine kukimbia nchi.na hapa mnaweza kukumbuka Lissu na Lema walivyokimbilia uhamishoni.
Rais wetu mpendwa amesema ni katika hali hiyo aliamua kuja na mpango wa 4R ili watu wote tuishi kama Taifa na tujenge Taifa letu kwa pamoja.amesema lakini kwa bahati mbaya sana kuna watu wamesahau ni wapi tulikotoka,ni wapi na mangapi na magumu mangapi wameyapitia katika maisha yao.lakini leo wameyasahau yote na kuanza kuleta vurugu,lugha za kichochezi, uchonganishi,uzushi na uongo na kupanga mipango ovu.
Amesema hata hivyo haishangazi kwa sababu kuna watu wenyewe hawapendi kuishi katika amani au kuona Taifa na nchi ikiwa katika Amani.ndio maana watu wa aina yao muda wote wanataka mavurugu vurugu tu.amesema hata hivyo hata sita kuwachukulia hatua kali za kisheria watakao jaribu kuchezea amani ya Taifa letu.Na kwamba 4R ni katika kutuungaisha na kutuleta pamoja watanzania na siyo kwa ajili ya kuvunja sheria .amesema sheria zipo palepale na zitatumika kama inavyotakiwa kwa mujibu wa katiba.
Nami Mwashambwa Lucas namuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu mpendwa.Embu fikiria ndugu zangu Mtu kama lissu hivi anaanzia wapi kumtukana,kumbagua ,kumtweza na kumtolea lugha za kumshushia heshima Mheshimiwa Rais wetu? Anaanzia wapi kumdharau Rais Samia ndugu zangu?anaanzia wapi kuona Rais Samia hafai? Anaanzia wapi kuona na kusema Rais Samia ni Dikteta? Lissu anawafahamu madikteta? Anawafahamu viongozi makatili?
Hivi Lissu angeanzia wapi kukanyaga katika ardhi ya Tanzania akiwa hai kama siyo Rais Samia? Angeanzia wapi kuja kupanda katika majukwaa yaliyo katika ardhi ya Tanzania na kutia matusi yake na bado akaachwa tu? Angeanzia wapi kuja hapa Nchini mpaka kupata nafasi ya kuchangiwa pesa za gari ikiwepo kutoka CCM? Angeanzia wapi Lissu kuja kuvuta oksijeni ya Tanzania? Angepata wapi nafasi ya kwenda hadi kusalimia ndugu zake kijijini kwake , kuhudhuria kanisani ,kuonana na rafiki zake ,kushiriki moja kwa moja mikutano ya chama chake?
Angepata wapi nafasi hiyo lissu kama siyo Mama yetu Mpendwa Rais Samia? Nani aliyemrejesha Nchini Kama siyo Rais Samia? Nani aliye mfuata hadi ulaya na kumhakikishia usalama akirejea Nchini kama siyo Rais Samia? Amesahau haya yote? Alikuwa na kesi ngapi mahakamani? Amefunguliwa kesi gani mahakamani wakati huu wa Rais Samia licha ya Lissu kutukana mimatusi yake na kutoa lugha zake za kibaguzi na kichochezi?
Kwanini anakosa shukurani na kutambua mchango na nguvu ya Rais Samia katika kuimarisha demokrasia, utulivu,amani na umoja wa kitaifa? Nani alimtembelea hospitalini kama siyo Rais Samia?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.