Rais Samia waminye Watanzania, hawana shukrani

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hi!

Tulipitia kipindi kigumu kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa miaka 6 mfululizo.

Kila mmoja shahidi, vyuma vilikaza sana. Wananchi hali ngumu, watumishi taabani.

Furaha ya wananchi ilikuwa kusikia kiongozi ametumbuliwa, wananchi waliaminishwa pesa zao zilikuwa zimeibwa na viongozi mafisadi na wafanyabiashara matajiri ingawa kila walipobanwa viongozi hao na wafanyabiashara hali zao wananchi hazijawahi kuwa nzuri.

Amekuja Samia katika kipindi kigumu cha COVID-19 baadaye Ukraine War lakini anajitahidi kuwapigania wananchi.

Kafanya mambo makubwa katika kipindi kigumu lakini shukrani hapewi. Ni Rais ambaye wananchi wamempuuza licha ya utu wake.

Sasa Rais Samia wakazie hawa wananchi. Hawana kumbukumbu za mateso waliyopewa na mtangulizi wako ambayo hayakuwa na sababu.

Waminye vizuri kwenye kodi. Sheria za kodi zizingatiwe. Wafanyabiashara kama hawatoi risiti weka ndani au wapige fidia. Wananchi kama hawadai risit wafungwe.
 
Hii sasa ndio inaitwa Blue Monday kama hujawahi kuisikia au kuifahamu ndio hii sasa
 
Hi!
Tulipitia kipindi kigumu kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa miaka 6 mfululizo.
Sasa RAIS SAMIA wakazie hawa wananchi. Hawana kumbukumbu za mateso waliyopewa na mtangulizi wako ambayo hayakuwa na sababu.
Ni vigumu kuamini kuwa unayemsema alikuwa ni makamu wa Rais. Alijua na kubariki kila kilichokua kikiendelea serikalini. Alikaa kwenye vikao vyote vya maamuzi vya baraza la mawaziri na kupitisha maazimio yote yaliyoletwa mbele yao.

Kama Mungu asingeingilia kati hata leo hii bado angekuwa msaidizi mkuu wa mtangulizi wake. Je ni wapi kwa kumbukumbu zako na jamii ya Watanzania, aliwahi kutoa ushauri tofauti au hata kutokubaliana na mipango ya seriali? Nachoka!

Kwa kumnbukumbu zangu hadi leo hajatuomba radhi wananchi katika ushiriki wake kwa maneno na matendo katika hiyo miaka 6 unayoita ni ya laana. Kazi iendelee!
 
Wananchi walishaga aminishwa na Nyerere kuwa iko siku watanyang'anywa walionacho na kupewa wasionacho.

Na magufuli nae aliwaaminisha kuwa wenye nacho wataishi kama masheta.

Kwahiyo Raisi anaependa kukuza sekta binafsi hapendwi na Walalahoi.

Walalahoi wanataka mtu wa kunyang'anya Wafanyabiashara na wagawiwe wao.

Na huku mtaani zimerudi zile stori za kila Nyumba mpya ni Rizuwani Gari zuri Rizuwani 😁😁😁
 
Ona mbuzi nyingine hata haijui kuwa Rais analipwa 46m per month ,,plus marupurupu ya kila hatua anayokanyaga na sisi wananchi ndio walipa Kodi...
 
Angezingatia sheria za kodi leo tusingekuwa na tozo, maana tozo ni kupora wanyonge pesa zao wasiweze kujiwekea walau akiba kidogo.
 
unaposema wananchi wamempuuza unamaanisha nini? au ulitaka wambebe migongoni mwao?
 
Haina haja mkuu,wanasema hivi kufanya jambo jema halifanyi wewe kupendwa bali linaweza kuletea chuki zaidi..

So haina haja ya kuwaminya bali Rais awe tuu focused kwenye mambo aliyoamua kuyafanya..

Wanasema historia itaandika ukweli na kuweka clear dermacations..

Staili nzuri ya kuwabana angeweza fanya kama Kwa kina Ruto amewaacha ma hustlers wake wakomae hukunakizidi kuwaambia wampe mda wampe muda mana kafuta ruzuku ya chakula,kafuta ruzuku ya mafuta anataka cheo cha PM nk..

So anaweza futa ruzuku ya mafuta Ili miradi iende maana Mwendazake alikuwa anakomesha na anawashushua kwa kuwaambia wapiga dili nk nk.
 
Wanaolalamika kwenye mtandao na kakikundi fulani kadogo kalikuwa na maslahi binafsi na mwendazake!!

Usione thread za malalamiko ukahisi ni watu wote wanalalamika!! Nakuhakikishia hako kakikundi hakana hata watu zaidi 20,000 kati ya watu 60+ Ml ya watanzania!!

Rais aache kuwaangalia watanzania wote hao kwa sababu ya wapuuzi wachache waiokuwa wamezoea kula kwa dhuluma?
 
Wanasumbua sana hawa team Jiwe
 
Rais Samia Suluhu amefanya maendeleo makubwa sana Tanzania anajua wapingaji wapo na sisi tusiopinga maendeleo tupo lakini hawezi kufata mawazo yako ya kipuuzi eti kuwaminya watanzania yeye lengo lake ni kuwainua watanzania kwenye maendeleo na sio kuwadidimiza
 
Sure umenena vyema Rais Samia Suluhu hawezi kutuacha wananchi wake eti kisa kuna wachache tu wanaopinga sisi tunachujua Tanzania ni salama na Samia na Rais hawezi kua na mawazo mganzo kama ya huyu jamaa
 
Magufuli ndie aliyekuwa anatembea na Paiz, kuminya korodani za Watanzania, Wapinzani na Wafanyabiashara

Samia wetu mpendwa ana huruma amewalipa hadi Vyeti feki.

Ukitaka kujua tabia za Original Tanzanians we mwangalie Mama tu.

Sio lile kundi la Wahutu waliowavamia Wasukuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…