Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
NJOMBE
Kijiji cha Mtwango
Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha
Sensa huja kila baada ya miaka kumi. Twendeni tukapate idadi yetu kamili ili Mh. Rais aweze kuwaleta mafungu yanayo endana na idadi yenu.
Tuendelee kuongeza mapato, tumefanya vizuri lakini bado tunaweza kufanya vizuri zaidi ili tuisaidie serikali kuu kutekeleza majukumu ambayo yanaongezeka siku hadi siku kutokana na wingi wa watu na mahitaji yetu katika maisha yetu ya kila siku.Miradi na fedha visimamiwe vizuri ili vilete matunda ambayo Mh. Rais anayotarajia. Watendaji wa serikali wasimamie makusanyo na matumizi ili wanachi waweze kunufaika.
Hussein Bashe - Waziri wa KilimoKesi zinazoendelea kati ya viongozi wa ushirika na "yule mtu anayefanya dili kukifanya chama cha lupembe kuwa ni taasisi yake ya kutengeneza fedha" ziishe ili muwekezaji apewe haki yake chama cha ushirika kiendelee.
Rasilimali za wakulima wa chai zilizohujumiwa sasa zitarudishwa mikononi mwao.
Mbolea itapatikana kwa bei ya ruzuku hata kwa wakulima ambao hawatakuwa wamesajiliwa baada ya muda huo kufika.
Waziri Bashe amewataka wakulima wote, hata wale wasiosajiliwa kufika kwa mawakala watakao orodheshwa hapo baadae ili kupata mbolea kwa bei ya ruzuku kwani serikali itaweka utaratibu wa kuwasajili hapohapo pasipo usumbufu.
Juma Aweso - Waziri wa Maji
Wizara ya maji ilikuwa wizara ya kero na lawama, sasa ni wizara ya matumaini na utatuzi. Miradi ya zaidi ya tsh bil 4.5 imekamilika mkoani humo.
Miradi 232 imetekelezwa nchi nzima, miradi 8 ikiwa mkoani Njombe.
Ummy Mwalimu - Waziri wa Afya
Vifaa tiba vipo tayari kupelekwa kwenye kituo cha afya cha Mtwango kilicho njengwa kwa mapato ya ndani kwa silimia 100.
Kwa kawaida mashine za X rays huwa hazipelekwi kwenye vituo vya afya, lakini kwa kuwa Mtwango ina zaidi ya wakazi 25000, wizara ya afya itapeleka mashine hii.
Steven Kiruswa - Naibu waziri wizara ya Madini
Trh 12 jijini Dodoma, mradi wa makaa mbadala yanayotokana na makaa ya mawe utazinduliwa. Ni mkaa utakaosambazwa nchi nzima utapunguza uharibifu wa mazingira. Hautoi moshi, unadumu kwa masaa mengi na hauna shida kabisa kwa matumizi ya nyumbani.
Wanachi watafute vitalu vya madini hayo, serikali itawapa leseni.
Stephen Byabato - Naibu waziri wizara Nishati
Umeme tunaozalisha kwa kiasi kikubwa unatokana na maji. Tutunze mazingira, tupande miti na tuhakikishe kwamba haikauki tuzalishe umeme wa kutosha.
Samia Suhuhu Hassan - Rais
Serikali imebeba mzigo kwa kushusha bei ya mbolea ili wanachi walime vizuri, mazao yauzwe zaidi na serikali ipate zaidi.
Pongezi kwa madiwani kwa kusimamia utekelezaji wa miradi na fedha nyingi inayotolewa. Mivutano isiwepo, fedha ikija pesa zielekezwe kwenye shida, kero na matatizo ya wanachi yatatuliwe.
Mkoa wa njombe upo salama, upo vizuri. Serikali itaendelea kutoa huduma.
Yote yaliyomo kwenye ilani ya chama cha mapinduzi yatatekelezwa kwa kadri ambavyo uchumi utaruhusu. SAfari ya maendeleo ni hatua.
Fedha bado ipo nyingi na haikusanywi. Juhudi za kuikusanya iongezeke kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.
=========
Makambako
Innocent Bashungwa - Tamisemi
Bajeti ya TARURA sehemu hii imeongezwa kwa asilimia 250, kutoka milioni 800 hadi bil 2.8
Trh 18 august, utiaji saini wa mikataba ili wakandarasi wasambae kote nchini kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijijini utafanyika.
Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha
Fidia za eneo la One Stop Point zinaandaliwa, mambo yakikaa sawa zitalipwa.
Zoezi la sensa lisichukuliwe kama kazi ya serikali. Linahusu watanzania wote hivyo tujitokeze wote kwa kuwa litasaidia kwenye maswala ya mipango na bajeti.
Makambako ni mji wa kibishara, ukusanyaji wa mapato uongezeke.
Juma Aweso - Waziri wa Maji
Mji wa makambako unahitaji maji lita milioni 9 lakini uzalishaji uliopo sasa ni lita milioni 4. Fedha za kutatua upungufu wa lita milioni 5 uliopo sasa zimeshatolewa, mkandarasi tayari kaanza kazi.
Watu wa aina ya Rais. Samia hawapatikani kila sehemu, tumtumie vizuri.
Hussein Bashe - Waziri wa Kilimo
Hadi kufikia mwaka 2025, nchi itakuwa na viwanda vikubwa viwili ambavyo vitakuwa vinazalisha mbolea inayotosheleza mahitaji ya ndani.
Makame Mbarawa - Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Serikali itajenga kituo kikubwa cha ukaguzi wa magari yote yanayowekwenda Mbeya na Songea. Fidia za watu kwenye eneo hili tayari zimeshaanza kulipwa.
========
Nyololo - Iringa
Samia Suluhu Hassan -Rais
Ada ya kidato cha tano na sita haikuahidiwa kwenye ilani lakini imefutwa.
Mbali ya hilo, watoto watakaotoa "shule zetu huku" watakaofanya vizuri kidato cha sita, watakaoenda kusoma uhandisi na utabibu yaani madaktari na mainjinia wanakwenda kusoma bure. Watasomeshwa na serikali bila kuchukua mkopo ule wa elimu ya juu. Serikali itawasomesha.
Lengo ni kuwaongezea watoto hamu na mvuto wa kusoma zaidi ili wafanye kazi kwenye maeneo hayo.
Viwanja vya ndege vitaendelea kujengwa pamoja na kufungua usafiri wa maji.