Bado najiuliza sipati majibu, ...kama tumeamua kujenga reli ya kisasa, SGR_TZ .... Pembeni ya reli ya zamani MGR_TZ:
1.Reli inakamikima, Kwa nini tuliamua kununua mabehewa ya mitumba badala ya mapya? Kulikuwa na haraka gani ya kuagiza mitumba badala ya kutoa order yanunuliwe mapya?
2. Kama zimeagizwa Rolling Stock 5 mpya za kutumika kwenye reli mpya, kwa nini chaguo letu lilijikita kwenye treni zenye speed ya hadi kilometra 160 kwa saa? Kwa nini hatukuchagua kilometa 250-300 au hata zaidi, kwa maana ya kisasa zaidi, ukizingatia ukubwa wa nchi yetu yenye zaidi ya kilometa 900 elfu za mraba?
3. Wametumwa vijana wa kitanzania kwenda Korea ya kusini kujifunza namna ya kuendesha na kuhudumia wasafiri wa reli na treni yetu ya kisasa, Je,ni teknolojia ipi wanaenda kujifunza? ni hii ya MGR au SGR ?
Baada ya miaka kumi tutawatuma kujifunza tena baada ya hii teknolojia ya sasa tuliyochagua kuwekeza kupitwa na wakati?.
Maswali niliyonayo ni mengi mno kwenye uwekezaji huu....natamani kusoma maoni ya wengine kwenye uzi huu kwanza! [emoji848]