Rais Samia: Wanaosema tunakopa sana, waseme pia tunalipa sana

Shida gani hiyo? Na reli ya Kati mbona haitumiki pia Ila inajengwa?
 

bado natafakari namna gani Copper ya katanga inafika Kigoma then kwenye reli Dar es salaam..
 
..Raisi anazungumzia deni la taifa kimasihara sana.

..inaelekea hajui hatari ya deni hilo kwa uchumi wa taifa.

..pia haijui historia ya nchi hii na matatizo yaliyowahi kutukuta kutokana na kufumuka kwa deni hilo.

..kauli zake kuhusu masuala ya uchumi, fedha, na deni la taifa, zinathibitisha kwamba hakujiandaa, wala hakuandaliwa, kuwa Raisi.
 
Kikwete hakwepeki katika utendaji wa SSH anategemewa tatizo anao ushawishi wenye kundi kubwa la watu nyuma yake na baadhi yao ni wachafu sana.

..tatizo Dr.Ssh hana uwezo.

..angekuwa strong na muelewa wa kazi yake wasingejitokeza watu wa kutaka kumsaidia.

..Dr.Ssh anazungumzia nchi kukopa halafu anasema, "...kuna wakati tutaomba msamaha wa deni...," unadhani anatosha ktk nafasi yake?
 
Bora mama msema kweli. Kanyaga twende tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 7.




Tunachokijua:
 
..tatizo Dr.Ssh hana uwezo.

..angekuwa strong na muelewa wa kazi yake wasingejitokeza watu wa kutaka kumsaidia.

..Dr.Ssh anazungumzia nchi kukopa halafu anasema, "...kuna wakati tutaomba msamaha wa deni...," unadhani anatosha ktk nafasi yake?
Kauli na vitendo vyake ni vitu tofauti. Ukubwa wa kazi anayoifanya bila ya kutumia nguvu kubwa kuyatangaza matokeo ya kazi ni umahiri alionao ambao marais wengi wanaume huwa hawana.

Tukio la kusaini mkataba wa SGR leo ikulu angekuwa rais wa kiume angehakikisha ardhi yote ya Tanzania mpaka ingetetemeka, lakini kwake ni tukio la kawaida tu lisilo na mbwembwe za ziada.

Namuona anatosha sana kwa mtindo wa kufanya kazi wa serikali alioamua kuja nao awamu ya sita.
 

..kwa hiyo unasema tupuuze kauli au hotuba zake?
 
Kama mnalipa sana mbona linazidi kuongezeka!!?
 
Makalla huwa hana hadhi ya kuwa mwanasiasa. Ana sura na muonekano wa mbeba mizigo wa bandarini. Huwa anaongea ujinga .
Linapokuja swala la kutia shombo basi wewe bi kinara humu, daah😂😂😂.
 
Mabehewa mapya ni kwamba unatoa order na linaanza kutengenezwa toka chasis. Haya makampuni ni kama ndege. Hawatengenezi kitu hadi kwa order, sio kwamba utaenda ukute mabehewa yamepangwa sokoni kama nyanya

Sasa order ya mabehewa mapya inaweza kuchukua miaka mitatu, wakati ya mitumba yanachukua labda kuanzia miezi sita, ndio maana wakaamua tuanze na ya mitumba wakati tunasubiri mapya, na ukizingatia mabehewa yaliyopo ni chakavu sana, yana kunguni na viroboto na breki zake nadhani ulishaona picha mitandaoni. Ukumbuk pia order ya mabehewa ni kwa ajili ya SGR na reli ya zamani.

Na pia kama ambavyo gari used la Mjapan ni sawa na jipya kwa Mtanzania, behewa used la Mjerumani ni sawa na jipya kwa Mtanzania. Wazungu hawana upuuzi wa kukojoa ndani ya behewa au kuchana viti makusudi

Swali ulilopaswa kuuliza ni kwamba - kwa nini hawakufanya timing ya order ya mabehewa na ujenzi wa SGR, ili ujenzi unapokamilika na mabehewa yanakuwa tayari - na jibu ni hapo ni watu wenye akili ndogo kupewa mamlaka makubwa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Makalla huwa hana hadhi ya kuwa mwanasiasa. Ana sura na muonekano wa mbeba mizigo wa bandarini. Huwa anaongea ujinga .
 
Madeni makubwa hayajawahi kuwa kitu kizuri kabisa kwa mataifa maskini.
 
We unategemea mshauri mwenyewe Madelu, atakushauri nini, uchumi kausomea kwenye makaratasi
 
Madeni makubwa hayajawahi kuwa kitu kizuri kabisa kwa mataifa maskini.

Sijui Dr.Ssh alikuwa wapi au akijishughulisha na nini wakati wa awamu ya Rais Mkapa.

Kwasababu kipindi hicho tulikuwa na hali ngumu sana ya uchumi iliyosababishwa na deni kubwa la taifa.

Mwalimu Nyerere na Mzee Mkapa walihangaika kufanya kampeni kuziomba nchi wafadhili zitusamehe madeni hayo.

Leo hii Rais Ssh kutoa kauli zinazoashiria kwamba deni la taifa ni jambo jepesi, nadhani ni kutokujua historia ya nchi yetu na masuala ya kiuchumi, au ni jaribio la kulaghai wananchi.
 
Ingekuwa kuna nafasi ya kuwauliza maswali haya papo kwa papo,hawa viongozi wetu wengi wangeshakufa kwa pressure ya kuulizwa maswali yenye akili wakati huo hawana uwezo wa kujibu kwa ufasaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…