Rais Samia: Wanasiasa mnaowapeleka Watu kwenye Hifadhi ili uchaguzi ukikaribia muwatetee, acheni hizo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WhatsApp Image 2024-08-05 at 07.15.09_c0adfea0.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi na Serikali kutunza na kuyalinda maeneo ya hifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye huku akiwaonya Madiwani na Wabunge wenye tabia ya kuanzisha Vijiji ndani ya maeneo ya hifadhi hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi kuacha tabia hiyo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CCM Ifakara, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro leo Agosti 5,2024.
WhatsApp Image 2024-08-05 at 15.56.43_079aeb6d.jpg
“Inapokaribia kipindi cha uchaguzi hasa Madiwani na Wabunge mtu akiona hayuko vizuri kwenye eneo lake anasogeza watu kuanzisha Kijiji halafu ni haohao wanaokuja kusimama kuwatetea watu walioingia ndani ya hifadhi. Ndugu zangu wanasiasa wenzangu acheni haya,” amesisitiza Rais Samia.

Amefafanua kuwa maeneo hayo yanahifadhiwa kwa makusudi maalum kwa faida na maendeleo ya nchi kwa sababu watu wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki hivyo ni lazima kuwa na ardhi iliyohifadhiwa kwa matumizi ya baadae

Rais Samia ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inahifadhi na kulinda maeneo inayoyasimamia na si kusubiria wananchi wavamie kisha kuwatoa.

“Mpaka wananchi wanahamia wanajenga shule, kituo cha afya bado mnawaangalia baadae wameshatulia ndio mnawaambia watoke wamevamia, hii nayo sio haki,” Rais Samia amesema.

Rais Samia yuko Mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wake pamoja na kuzungumza na wananchi.
 
Anamaanisha hata watumishi wa hifadhi hawaruhusiwi kupiga kura ndani ya hifadhi?

Kwani hizo hifadhi zipo nchini au nje ya Nchi?
 
Hujamwelewa vizuri.

Anamaanisha kuna maeneo ya hifadhi yanavamiwa na wananchi na wanasiasa wanawakingia kifua kwa msemo wa wapiga kura wao.
Na baadhi wanadiriki kuanzisha kijiji ndani ya kijiji (Katika hifadhi) kwa msukumo wa viongozi wao wa kisiasa.
 
Mbona wanawauzia wajomba? Waache janja janja ya sungura hapa!
 
“Inapokaribia kipindi cha uchaguzi hasa Madiwani na Wabunge mtu akiona hayuko vizuri kwenye eneo lake anasogeza watu kuanzisha Kijiji halafu ni haohao wanaokuja kusimama kuwatetea watu walioingia ndani ya hifadhi. Ndugu zangu wanasiasa wenzangu acheni haya,” amesisitiza Rais Samia.
Samia, yule wa Kihonda hapo Morogoro amezuia ujenzi wa barabara kwa kwakuwa yeye mwenyewe amejenga vibanda vyake vya biashara kwenye hivadhi ya barabara ya Kihonda - Tungi - 88
 
Mbona wanawauzia wajomba? Waache janja janja ya sungura hapa!
Wajomba hawauziwi mkuu.

Ni approach ya uhifadhi kwa kuingia makubaliano na Serikali/vijiji husika kwa miaka kadhaa huku pande zote 2 zikinufaika financially.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi na Serikali kutunza na kuyalinda maeneo ya hifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye huku akiwaonya Madiwani na Wabunge wenye tabia ya kuanzisha Vijiji ndani ya maeneo ya hifadhi hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi kuacha tabia hiyo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CCM Ifakara, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro leo Agosti 5,2024.
“Inapokaribia kipindi cha uchaguzi hasa Madiwani na Wabunge mtu akiona hayuko vizuri kwenye eneo lake anasogeza watu kuanzisha Kijiji halafu ni haohao wanaokuja kusimama kuwatetea watu walioingia ndani ya hifadhi. Ndugu zangu wanasiasa wenzangu acheni haya,” amesisitiza Rais Samia.

Amefafanua kuwa maeneo hayo yanahifadhiwa kwa makusudi maalum kwa faida na maendeleo ya nchi kwa sababu watu wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki hivyo ni lazima kuwa na ardhi iliyohifadhiwa kwa matumizi ya baadae

Rais Samia ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inahifadhi na kulinda maeneo inayoyasimamia na si kusubiria wananchi wavamie kisha kuwatoa.

“Mpaka wananchi wanahamia wanajenga shule, kituo cha afya bado mnawaangalia baadae wameshatulia ndio mnawaambia watoke wamevamia, hii nayo sio haki,” Rais Samia amesema.

Rais Samia yuko Mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wake pamoja na kuzungumza na wananchi.
Huyu mama wanamuelewa akina ChoiceVariable na Lucas Mchambwa tu
 
Hujamwelewa vizuri.

Anamaanisha kuna maeneo ya hifadhi yanavamiwa na wananchi na wanasiasa wanawakingia kifua kwa msemo wa wapiga kura wao.
Na baadhi wanadiriki kuanzisha kijiji ndani ya kijiji (Katika hifadhi) kwa msukumo wa viongozi wao wa kisiasa.
Wewe umeelewa alichosema?

Hujui ngorongoro ni Mali ya wamasai kisheria kabisa Kwa miaka mingi?
 
Hujamwelewa vizuri.

Anamaanisha kuna maeneo ya hifadhi yanavamiwa na wananchi na wanasiasa wanawakingia kifua kwa msemo wa wapiga kura wao.
Na baadhi wanadiriki kuanzisha kijiji ndani ya kijiji (Katika hifadhi) kwa msukumo wa viongozi wao wa kisiasa.

..Samia anayetaka kuchimba madini Serengeti ndiye amejigeuza kufundisha wengine kuhusu umuhimu wa hifadhi na rasilimali za taifa?

..halafu wenye mamlaka ya kuanzisha vijiji si serikali, na wana Ccm wenzake? Na yeye si Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa Ccm. Je, amechukua hatua gani toka wananchi wamehamia ktk hifadhi, mpaka wanastahili kijiji?
 
Back
Top Bottom