Rais Samia, wanasiasa wanaishi bila mashaka, hakuna aliyeumwa hata na sisimizi

Sukuma gang watajinyonga walahi. Maana mama amewapiga na kitu kizito kichwani kwa kukutana na kufanya mazungumzo na adui mkubwa wa mzimu wao wa Chato
Sukuma gang nadhali walikukopa kitu huko nyuma na hawakukulipa ndo maana unashinda uki wawaza😁😁😁😁
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Mama kapiga u turn ya maana!

Ila Lisu nae akili zake anazijua mwenyewe, eti "nataka rais atamke hadharani kwamba ananikaribisha nyumbani"

Sijui anajiona nani huyu jamaa!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Confidence from what you know and the way people appreciate you.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya DW amesema wanasiasa wakubwa wa upinzani wako wengi nchini Tanzania na hakuna anayeishi kwa mashwaka kwa kuwa hakuna aliyenyukuliwa hata kuumwa na sisimizi, hivyo Tundu Lissu aulizwe mashaka yake ni yapi.

Aidha kuhusu kauli yake ya awali iliyookana kuingilia uhuru wa mahakama kuhusu kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawezi kuitolea ufafanuzi kwa kuwa watu wanasema mengi hawezi kutolea ufafanuzi kila kitu.

Nafkiri jibu jepesi alilokusudia mama kumwambia Lissu ni kwamba yashayopita yashapita sasa aje tujenge nchi, hii ndio maana halisi ya majibu ya Rais, asingeweza kutamka direct kama yashayopita yashapita kwa vile italeta sura mbaya zaidi kwa mwendazake, lakini mama amekusudia hivyo.
 
Mashaka ya Lissu yanatokana na alichofanyiwa wakati wa mwendazake, na baadhi ya wale wahuni waliomfanyia Lissu ubaya bado wapo kwenye system mpaka leo.

Ni haki kwa Lissu kuwa na mashaka kwa usalama wake, vyema atoe kauli moja kama mkuu wa nchi Lissu na wenzake wawe na amani warudi nchini.

Samia asiangalie wanasiasa wakubwa tu, atazame na wadogo pia, bado polisi wanahangaika kuzuia hata mikutano ya ndani ya Chadema, hawa wanatakiwa kukemewa.

Kuhusu kauli yake anayogoma kuitolea ufafanuzi juu ya kesi ya Mbowe kwa kuogopa watu kusema mengi, hapo ndipo nakubali tuna Rais mwanamke, kama anaogopa hadi maneno ya watu mitandaoni kazi ipo.
????!!!!!!!
 
HAWEZI KUTOLEA UFAFANUZI KESI ILIYOPO MAHAKAMANI. RAIS AMEZINGATIA MATAKWA YA KIKATIBA MSIJARIBU KUMUINGIZA KTK MTEGO ILI MPATE PA KUMSEMA

Nampongeza kwa kukataa kulifafanua jambo la mahakamani
 
Mbona alipohojiwa na bbc alitolea ufafanuzi?
 
Minikajua atajibu Lisu nimemruhu arudi na ntampa ulinzi!
Mama anawapiga watu chenga ya mwili sasa.
Yaani mtu mmoja apewe ulinzi special? Hapana

Watanzania wote tuna haki ya kulindwa na tutatumia mfumo uliopo wa ulinzi

Kama anataka ulinzi special akawarecruit mabodigadi wamlinde awalipe mwenyewe

Nchi yetu ni ya amani na tuko salama.. mama ameshasema hakuna mashaka arudi tu
 
Ndiyo maana amekataa kuingia ktk mtego wenu
Rais anajua aliingizwa mkenge na lile lizee lenye macho makubwa akajikuta anajibu mambo asiyoyajua kuhusu Mbowe.

Kesi ipo mahakamani, mama akaingizwa mkenge kuitolea maelezo halafu akadanganya kwamba kuna wengine walishakamatwa na kufungwa kwa kesi hiyohiyo inayomhusu Mbowe Sasa kwenye hii ameona asiongelee ndio maana akasema hataki kuongelea kwasababu kuna mengi yanaongelewa huko mtaani 😂

She knows better hiyo kesi imemchafua sana na Kuna wahusika wanamdanganya ili achafuke na amegundua nia yao wanafanya ili akwame.

Kuna watu wanahakikisha Lissu harudi na akirudi wanataka wamuue wanajua survival yao ni ndogo sana endapo Lissu na mama wakielewana maana wanajua watakuwa wamekwisha.

Jiulize mtu kama bashite , ndugai, Sirro nk unahisi wanapenda wanaposikia Lissu ameongea na Rais na walikuwa wawili tu nani anajua yaliyoongelewa?

Hao watu ndio wanashinikiza asirudi na ndio waliiba hata passport ya Lissu, sasa unamuibia Lissu mtu mwenye international recognition unadhani utamkomoa? Lissu kwa sasa nadhani atakuwa amebobea kwenye international laws na ndio maana wamemuibia passport na bado anaishi huko kwa special permit.

Wajiandae tu ni sawa na waliokuwa wanasema Rais asikope ilimradi walikuwa wanataka afeli kukamilisha miradi ili wamseme hafai. Jambo la kufurahi ni kwamba Rais anawajua wanafiki wanaotaka afeli anawakaushia tu ndio maana anafanya yale wasiyotegemea.

Lissu, Lema and Wenje watarudi Ila wanaomba ulinzi sababu wale waliokuwa wanawatafuta bado wapo serikalini na hawatakubali wawe exposed watahakikisha wanawaua tu na ndio maana wanaomba ulinzi wa Rais na sio IGP.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya DW amesema wanasiasa wakubwa wa upinzani wako wengi nchini Tanzania na hakuna anayeishi kwa mashwaka kwa kuwa hakuna aliyenyukuliwa hata kuumwa na sisimizi, hivyo Tundu Lissu aulizwe mashaka yake ni yapi.

Aidha kuhusu kauli yake ya awali iliyookana kuingilia uhuru wa mahakama kuhusu kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawezi kuitolea ufafanuzi kwa kuwa watu wanasema mengi hawezi kutolea ufafanuzi kila kitu.

Lissu alivyopigwa risasi 16?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Mama kapiga u turn ya maana!

Ila Lisu nae akili zake anazijua mwenyewe, eti "nataka rais atamke hadharani kwamba ananikaribisha nyumbani"

Sijui anajiona nani huyu jamaa!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Wewe una mshabikia Rais live lakini wewe huwezi kukutana na Rais hata kwa ndoto ndiyo tofauti ya Lissu na sisi choka mbaya
 
Mashaka ya Lissu yanatokana na alichofanyiwa wakati wa mwendazake, na baadhi ya wale wahuni waliomfanyia Lissu ubaya bado wapo kwenye system mpaka leo.

Ni haki kwa Lissu kuwa na mashaka kwa usalama wake, vyema atoe kauli moja kama mkuu wa nchi Lissu na wenzake wawe na amani warudi nchini.

Samia asiangalie wanasiasa wakubwa tu, atazame na wadogo pia, bado polisi wanahangaika kuzuia hata mikutano ya ndani ya Chadema, hawa wanatakiwa kukemewa.

Kuhusu kauli yake anayogoma kuitolea ufafanuzi juu ya kesi ya Mbowe kwa kuogopa watu kusema mengi, hapo ndipo nakubali tuna Rais mwanamke, kama anaogopa hadi maneno ya watu mitandaoni kazi ipo.
[emoji871]Amesema ameiachia Mahakama ifanye kazi yake kwa Uhuru na kwa mujibu wa Sheria.

[emoji871]Akiishamfunga Mbowe ndiyo utauelewa vizuri uanamke wake!
 
Rais anajua aliingizwa mkenge na lile lizee lenye macho makubwa akajikuta anajibu mambo asiyoyajua kuhusu Mbowe.

Kesi ipo mahakamani, mama akaingizwa mkenge kuitolea maelezo halafu akadanganya kwamba kuna wengine walishakamatwa na kufungwa kwa kesi hiyohiyo inayomhusu Mbowe Sasa kwenye hii ameona asiongelee ndio maana akasema hataki kuongelea kwasababu kuna mengi yanaongelewa huko mtaani [emoji23]

She knows better hiyo kesi imemchafua sana na Kuna wahusika wanamdanganya ili achafuke na amegundua nia yao wanafanya ili akwame.

Kuna watu wanahakikisha Lissu harudi na akirudi wanataka wamuue wanajua survival yao ni ndogo sana endapo Lissu na mama wakielewana maana wanajua watakuwa wamekwisha.

Jiulize mtu kama bashite , ndugai, Sirro nk unahisi wanapenda wanaposikia Lissu ameongea na Rais na walikuwa wawili tu nani anajua yaliyoongelewa?

Hao watu ndio wanashinikiza asirudi na ndio waliiba hata passport ya Lissu, sasa unamuibia Lissu mtu mwenye international recognition unadhani utamkomoa? Lissu kwa sasa nadhani atakuwa amebobea kwenye international laws na ndio maana wamemuibia passport na bado anaishi huko kwa special permit.

Wajiandae tu ni sawa na waliokuwa wanasema Rais asikope ilimradi walikuwa wanataka afeli kukamilisha miradi ili wamseme hafai. Jambo la kufurahi ni kwamba Rais anawajua wanafiki wanaotaka afeli anawakaushia tu ndio maana anafanya yale wasiyotegemea.

Lissu, Lema and Wenje watarudi Ila wanaomba ulinzi sababu wale waliokuwa wanawatafuta bado wapo serikalini na hawatakubali wawe exposed watahakikisha wanawaua tu na ndio maana wanaomba ulinzi wa Rais na sio IGP.
Ukweli ni mdogo sana kwenye haya uliyoandika. Kesi kubwa kama hiyo haiwezi kufanyika bila baraka za Raisi.
 
Back
Top Bottom