BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Takwimu zinaonyesha wanawake milioni 44 wamepoteza ajira barani Afrika hadi kufikia mwaka 2021, huku idadi ya wanawake kwenye vyombo vya maamuzi Tanzania ikiongezeka kutoka asilimia 21.5 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 37 mwaka 2020.
Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Desemba 3, 2022 na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kongamano la nne la wanawake vijana wa mtandao wa viongozi Afrika lililofanyika visiwani Zanzibar.
“Tuko hapa kutekeleza ahadi zetu kwa wanawake vijana, mkutano huu ulikuwa ni jukwaa ambapo wanawake viongozi wakubwa wanaweza kuwasaidia viongozi vijana dhidi ya mustakabali mwema,”amesema Rais Samia.
Amesema mkutano huo pia unatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Taifa yaliyopo kwenye ajenda ya mwaka 2060 ili kujenga Afrika inayotakiwa.
“Kupitia kusanyiko hili tunaweza kuhakikisha maendeleo endelevu 17 ya Dunia yanatekelezeka kwa kutegemea wanawake kwa viwango mbalimbali katika nyanja zote za maisha na hilo ni lengo la msingi kujenga dunia yenye Amani na mafanikio,”amesema.
Kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake Rais Samia amesema zipo za kihistoria ikiwa ni pamoja na kutopata rasilimali, kutengwa, kutopata haki zao na wakati mwingine wanakuwa hawana mzunguko katika sekta mbalimbali hivyo kupelekea kukosa nafasi za maamuzi.
“Hii inafanya wanakuwa wahanga ndio maana wanakosa nafasi na kuwekwa pembezoni hadi leo shughuli za nyumbani zimekuwa ni jukumu la mwanamke tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa mwanamke.
“Hadi leo imefanya kumekuwa na migogoro mikubwa ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, Uviko 19, lakini pia migogoro ya nishati na chakula ambayo yote inarudisha nyuma maendeleo ya Afrika na mwanamke kwa ujumla,”
Amebainisha kuwa katika nchi mbalimbali isipokuwa zile zenye migogoro idadi ya wanawake kwenye vyombo vya maamuzi imeongezeka ikiwemo Tanzania ambapo wabunge wanawake wameongezeka kutoka asilimia 21.5 2005 hadi kufikia asilimia 37 mwaka 2020.
“Majaji wa mahakama kuu, mahakama za rufaa wamefika asilimia 47 na mahakimu wa mahakama za mwanzo na wilaya kutoka asilimia 25 hadi 35, mabalozi wanawake kutoka asilimia 3 mwaka 2005 hadi asilimia 25 mwaka 2020,” amesema.
MWANANCHI