Naomba kuchukua nafasi hii kuandika kwa kifupi kabisa ombi moja kwa niaba ya watanzania.
Nakuomba Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia tafadhali wachukulie hatua za kisheria wote wanaohusika na ufisadi wa kutisha unaoendelea katika nchi yetu.
Tunakopa matrilioni, lakini tunapoteza matrilioni kizembe sana kila mwaka. Ukienda kwenye vituo vya afya utaumia sana kuona watu wakiachwa wafe kisa wamekosa shilingi laki 6 za kufanyiwa upasuaji mdogo. Akina mama wanajifungulia nyumbani kwa kukosa fedha za kulipia hospitali. Ni mengi mno ya hovyo yanaendelea.
Maofisini watu wanatamka waziwazi wanasema; wakati wa “kupiga” hela ni huu, mtu ashindwe mwenyewe tu.
Niombe tena kurudia ombi langu kwamba mheshimiwa Rais chukua hatua kali kwa wasaidizi wako la sivyo nchi hii itatafunwa kama kitumbua na kumalizwa na wachache wanaojipendekeza kwako! Kataa kusifiwa kinafiki!
Hali ya ubadhirifu sio nzuri hata kidogo chukua hatua kali! Walioiba fedha za umma sio tu waachishwe kazi ili wakatulie na kula walichoiba, bali pia warudishe fedha hizo kwa namna yoyote na kwenda jela!
Ahsante.